Search results

  1. G Sam

    CDF mstaafu Mabeyo amelikoroga, Makamu wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais

    1. Aliyestahili kumpatia taarifa Makamo wa Rais juu ya kifo cha Rais Magufuli ni daktari wa Rais. 2. CDF Mabeyo alikuwa mkuu wa majeshi ndiyo, yeye pamoja na viongozi wengine wa vyombo vya usalama walitakiwa pia kupatiwa taarifa na Makamo wa Rais (Baada ya yeye kuwa mtu wa kwanza kabisa...
  2. G Sam

    Kinana: Nakemea viongozi wa chama wanaowadhalilisha viongozi na watendaji wa serikali hadharani

    Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara ndugu Abdulrahaman Kinana amekemea baadhi ya viongozi wa CCM wanaowadhalilisha viongozi na watendaji wa serikali hadharani. Kinana amesema badala yake wanatakiwa kutumia vikao halali vya chama kufikisha ujumbe wao. Jiwe hili limerushwa.
  3. G Sam

    Charles Kitima una hoja za kujibu tena haraka iwezekanavyo

    Naomba nikuulize maswali yafuatayo: 1. Kilichosainiwa kwenye HGA kati ya DPW ulikifahamu kabla? Kama jibu ni ndiyo 2. Kwanini hukurudi kwetu waumini kutueleza yatakayojiri ili kusikia jamii yako ina hoja gani? 3. Kwanini ufanye siri? Kama jibu ni hapana, 3. Ulienda Ikulu kufanya nini? 4...
  4. G Sam

    Rais Samia, hiyo nchi inayoitwa Tanzania uliyoiuza kwa DP World ni hii hii The United Republic of Tanzania? (Angalia kifungu nilichoweka)

    Kwa mujibu wa kipengele hiki kilichopo kwenye IGA kati ya Tanzania na Dubai Ports kuna nchi inayoitwa "Tanzania" ambayo Rais Samia ameuza special economic areas zake zote kwa DP World. Sasa naomba kukuuliza Rais Samia. Hiyo nchi inayoitwa Tanzania uliyouza operations zote za special economic...
  5. G Sam

    Wanaotetea mkataba kati ya Tanzania bara na DP World wanasumbuliwa na udini!

    Niseme wazi kabisa wabaotetea huu mkataba wa kipuuzi kati ya Tanzania bara na DP World kuwa wamilikishwe bandari zote za Tanzania bara kwa mkataba usiokuwa na ukomo wanasumbuliwa na udini. Hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kuthubutu kuungana na huu upuuzi zaidi tu ya udini wao. Wana...
  6. G Sam

    Tetesi: Inadaiwa uchunguzi juu ya kupotea kwa Ben Saanane unaendelea

    Kupotea kwa Ben Saanane ni moja ya mambo ambayo yalitokea enzi za utawala wa awamu ya tano na hakuna aliyethubutu kuanzisha uchunguzi juu ya hilo kutokana na maelekezo maalum. Sasa nawataarifu kuwa uchunguzi juu ya kupotea kwa kijana huyo unaendelea na ni moja ya ajenda muhimu zilizojadiliwa...
  7. G Sam

    Nikikutana na Majaliwa aliyejinadi kufungua mlango wa ndege ya Precision namcharaza viboko kweli kweli! Watanzania ifikie pahala tutumie akili

    Naam, imefikia pahala watanzania tunajitumbukiza kwenye vijistori vya hovyo hovyo na kuvinadi pasipo kufanya utafiti wa kina. Hili mimi naliona kama tatizo kubwa sana kwetu kama watanzania. Hivi karibuni ameibuka kijana mmoja ambaye alidai kuwa alifungua mlango wa ndege iliyopata ajali huko...
  8. G Sam

    Wale Askari polisi na Wanajeshi waliokuwa wamesiama pembeni wakiwaangalia wananchi wakivuta ndege kwa kamba ni Watanzania?

    Nimeona video ya wananchi wakivuta ndege ya PW huko ziwani Bukoba kwa kutumia kamba huku wakiimba na kuhamasishana. Nimeangalia hiyo video na kuwaona askari kadhaa wa Jeshi la Polisi pamoja na Wanajeshi wakiwa wamesimama pembeni "Wanaangalia" tukio. Swali langu ni moja tu: Je, wale ni Watanzania?
  9. G Sam

    Kazi nzuri sana mkuu wa wilaya ya Temeke

    Nimeona uchapakazi wako japo unaonekana una uchovu fulani (lakini ni wa baraka) Unapambana kweli kweli hongera sana kwa uchapa kazi. Mabilioni yamemwagwa Temeke DC wa Temeke Jokate Mwegelo akiwa na waziri Bashungwa kwenye kuchapa kazi Mabadiliko ni muhimu. Hongera sana Pascal Mayalla aone...
  10. G Sam

    Nasimama na William

    Hata kama ni wewe ungeoa kweli. Zigo kama hili ni la ku-buy time ili maisha yaendelee.
  11. G Sam

    Kukumbukia ukatili kumetufanya tusahau matatizo mengine yote kwa muda. Watanzania tujifunze

    Hakuna ubishi kuwa enzi ya utawala wa awamu ya tano wa hayati John Magufuli kulikuwa na vitendo lukuki vilivyokuwa na ukatili mkubwa dhidi ya binadamu. Kuanzia watu kuokotwa fukweni, kupotea, kupigwa risasi, kutishiwa wahame vyama, kunyamazisha vyombo vya habari, kutaifisha, kwenda kinyume na...
  12. G Sam

    Kama Hayati Magufuli alikuwa anaipeleka nchi shimoni tujuzwe. Watendaji wengi aliowafurumusha wamerejeshwa huku wake wakifurumushwa

    Watendaji wengi ambao hayati Magufuli alikuwa akiamka ama usiku wa manane akiwafurumusha hatimaye wengi wanarejeshwa kwa kasi tena wakipanda vyeo maradufu. Kwa uchache 1. Lawrence Mafuru alifurumushwa kutoka msajili hazina kwa kupinga kuwa hakuna mkurugenzi anayelipwa milioni 15. Leo...
  13. G Sam

    Kikao cha Kamati zote za Bunge kilichokuwa kiongozwe na Spika Job Ndugai leo chaahirishwa

    Leo kilikuwa kifanyike kikao maalum cha wawakilishi wa kamati zote za bunge chini ya uongozi wa Spika Job Ndugai. Kikao hicho ambacho kilikuwa kifanyike huko Unguja kimeahirishwa. Sababu za kuahirishwa kwake hazijawekwa wazi ingawa zipo taarifa za ndani kuwa tayari Job Ndugai ameshajiuzulu...
  14. G Sam

    #COVID19 Askofu Gwajima anavyoongea na waumini wake ni kama muhuni wa kijiweni anayepiga stori za kijinga

    Nashangaa sana kuona wale wanaoitwa waumini wa Gwajima wakijiinua inua kutoka vitini huku wanaitika Haleluya pale mchungaji wao bwana Gwajima anapowapigisha stori za kijinga na kuwapotezea muda wao. Gwajima anaongea mambo ya uongo, yasiyo na ushahidi na mbaya zaidi anayapeleka madhabahuni na...
  15. G Sam

    Ni suala la muda tu jimbo la Kawe kutangazwa kuwa lipo wazi

    Kwa wataalam wa siasa tunasema kuwa Mbunge wa Kawe bwana Gwajima ameshavuka red line na kinachofuata ni kutangazwa tu kuwa Jimbo lipo wazi. Huenda hata asimalize huu mwezi akiwa mbunge kwani amepitiliza kuwa na sifa kuu za usaliti. Yani amepata mpaka sifa za ziada. Gwajima kwa sasa ni ama...
  16. G Sam

    Mwigulu aanza tena kampeni zilizomfukuzisha uwaziri awamu ya 5

    Yani huyu waziri bwana, sijui huwa anafanya maigizo ili kumfanya nani mjinga! Alipokuwa waziri wa kilimo alikutana na watu waliozuia msafara wake huko Iringa wakimsifu. Ila kwa kuwa Magufuli hakutaka hivyo akamuonya akamuhamisha na wizara. Alipoenda mambo ya ndani napo akawa vile vile na...
  17. G Sam

    #COVID19 Napendekeza mkoa wa Kilimanjaro uwekwe "lockdown"

    Kiukweli kama tunahitaji usalama basi mkoa wa Kilimanjaro uwekwe lock down. Hali huko ni mbaya kuliko inavyoelezwa. Serikali kama hamtachukua tahadhari mapema msije kusema hamkuambiwa. Wageni wanoingia na kutoka kila siku ndani ya mkoa huo na kusambaa mikoa mingine ni kiama kwa wengine...
  18. G Sam

    Mwenyekiti wa BAVICHA taifa John Pambalu naye aanza safari na jeshi la polisi kutoka Mwanza kwenda Dar usiku wa leo kwa ajili ya upekuzi

    Taarifa za uhakika ni kuwa, mwenyekiti wa BAVICHA taifa John Pambalu naye usiku wa leo ameanza safari ya kusafirishwa na jeshi la Polisi kupelekwa Dar kwa ajili ya upekuzi. Kiongozi huyo pamoja na msaidizi wake wa idara ya uenezi wanatuhumiwa kumiliki mitambo ya kufyatua katiba.
  19. G Sam

    Rais Samia asihurumiwe kwakuwa ni mwanamke; kiongozi wa nchi lazima awe na ngozi ngumu. Wapambe acheni kulialia

    Kama kuna mtu anadhani kuwa kwa sababu tu Rais Samia ni mama basi atahurumiwa pale anapovurunda kutokana na jinsia yake basi anajidanganya. Siasa ni ngumu na unatakiwa kuwa himilivu kweli kweli. Ukitaka kujua hilo angalia siasa za wenzetu kama Kenya ama Marekani. Kiongozi anaangaliwa kama...
  20. G Sam

    DC mteule ndugu "Mchopanga" alisoma shahada ya kwanza bila kuwa na matokeo ya kidato cha sita licha ya kuisoma kwa miaka mitatu

    Niliposoma gazeti la MWANANCHI la leo ni kuwa yupo DC mmoja mteule ambaye anatokea kwenye tasnia ya wasanii ambaye alienda nchini India kwenye chuo kikuu cha Bangalore akisomea shahada ya kwanza kwenye mambo ya sanaa huku matokeo yake ya kidato cha sita yakiwa hayajatoka. Kwa mujibu wa gazeti...
Back
Top Bottom