Jamii Check

Jukwaa maalum la wananchi kushiriki mchakato wa kuthibitisha taarifa wanazokutana nazo mtandaoni au nje ya mtandao
Mdau mmoja wa JamiiForums.com analalamika kuwa alitumia dawa za kutibu Ugonjwa wa Malaria zinazoitwa EKELFIN ambazo baadaye zilimsababishia kupatwa na mchubuko sehemu za siri na midomoni. Anashangaa kwanini Serikali haitoi taarifa kwa watumiaji juu ya madhara ya dawa hizi kwa binadamu. Ni kweli kuwa dawa hizi zinaweza kusababisha athari tajwa?
MADAI Kisayansi na kibaiolojia virusi wanasifa ya kutokuwa hai pale wanapokuwa nje ya seli ya kiumbe mwingine(host) na wanaweza kukaa muda mrefu bila kuwa na dalili zote za viumbe hai mpaka pale watapoingia kwenye seli ya kiumbe. Inakuwaje sasa tunaambiwa HIV haambukizwi kwa mashine za kunyolea saloon kwa kigezo cha kwamba hawawezi kuishi katika mashine na ilihali wao ni vijidudu visivyo hai wanapokua nje ya host?
Asali ni chakula kinachotumika kama dawa ya magonjwa mengi. Hutibu vidonda, kikohozi, huondoa sumu mwilini, ni chanzo bora cha nishati pia hutumika kwa kazi nyingi za urembo. Ukipita mtandaoni utaona baadhi ya makala zikiweka marufuku ya kuwapatia watoto wachanga asali. Jambo hili linaleta ukakasi mkubwa wa jamii kwa kuwa asai imekuwepo kwa miaka mingi, na karibia kila jamii huitumia. Katazo hili lina ukweli gani kisayansi?
Kuna mijadala mingi inayosema kuwa Passport yetu ya Tanzania haikubaliki kama proof of ID je ni kweli?
Nimepokea hivi karibuni voice note kutoka kwa Mtanzania anayeishi Afrika Kusini. Sauti hiyo ya Dudula Master ambaye ni mhamasishaji mkubwa wa Xhenophobia ametoa onyo dhidi ya wageni wote kuondoka Afrika ya Kusini kuanzia tarehe 02 Septemba 2022 hadi Machi 2023. Nchi zetu hususan Tanzania zinapaswa kuhakikisha usalama kwa raia wao wanaoishi kule kihalali na ikiwezekana kuweka utaratibu wa kuwaondoa raia wake Afrika ya Kusini. Matishio haya yamekuwa yakifanyika bila hatua zozote kuchukuliwa, hivyo inawezekana baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola vya Afrika ya Kusini ni wahusika wa hizi operesheni dhidi ya wageni. Hatulipi ubaya kwa ubaya bali kumtenga mtu mbaya ni sehemu ya kumpa fundisho dhidi ya mtenda ubaya. Ni wakati sasa wa Nchi...
MADAI Kwa mujibu wa mdau mmoja, Disemba 12, 2019 aliona kwenye taarifa ya habari wakitangaza kuwa familia moja imepoteza watoto wao wanne kwa kile kinachodaiwa kuwa walikula mihogo yenye sumu. Aidha, mada hii imekuwa inazungumzwa sana mitaani, huku ikiacha mashaka makubwa kwa kuwa mihogo ni chakula kinachotumika kwa kiasi kikubwa, kama kingekuwa na sumu basi watu wengi wangekuwa wamepoteza maisha. Tuelewe nini kuhusu madai haya? Ni kweli kuwa mihogo huwa na sumu, au ni uzushi tu unaopaswa kupuuzwa?
Nanasi ni tunda lenye faida lukuki kwa afya. Miongoni mwa faida za tunda hili ni kuongeza kinga ya mwili, kutibu mafua, kupambana na saratani, kuondoa maumivu pamoja na kulinda moyo. Pamoja na uwepo wa faida hizi kwa afya, nanasi huhusishwa na changamoto ya kubaribika kwa ujauzito kwa wanawake, hivyo baadhi ya jamii huwashauri wasitumie tunda hili kama njia ya kulinda ujauzito wao. Ukweli upoje?
Naona mambo ni moto kweli kweli, inasemekana Ndugai aliwekwa kizuizini na barua yake ya kujiuzulu Uspika hakuiandika yeye ni kwa mujibu wa hii tweet. Sisi yetu mambo, maana malipo ni hapa hapa. Hakika muosha huoshwa.
Wataalamu wa afya huelezea umuhimu na faida za kufanyika kwa tendo hili kwa wanaume. Baadhi ya sehemu wanaume huwa hawatahiriwi kabisa, na wengine wanaotahiri husubiri hadi mtoto afikishe walau miaka 12 ndipo afanyiwe tendo hilo kwa uoga wa kupunguza ukubwa wa viungo hivyo. Madai haya yamekuwepo kwa muda mrefu, na majibu sahihi bado hayajatewa. Ni kweli kuwa tohara hupunguza ukubwa wa via vya uzazi vya mwanamme?
Madai: Yapo madai kutoka katika jamii mbalimbali yakihusisha rangi nyekundu na radi. Baadhi ya jamii zinaamini kwamba kuvaa mavazi yenye rangi nyekundu wakati wa mvua ni hatari kwa sababu yanaweza kusababisha ukapigwa na radi. Sambamba na hilo jamii nyingine zinaamini Mjusi kafiri na Kondoo wana uwezo wa kupambana na radi. ---
MADAI Mabehewa 30 na vichwa 2 vya treni za SGR mali ya TRC vinapigwa mnada 25/11/2022, nchini Germany kufuatia mgogoro wa TRC na EUROWAGON Railways Limited (Turkey), iliyopewa kazi ya kukarabati na kutia nakshi. TRC wamelipa Sh. 23 bilioni (35% ya kazi). Inadaiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalçın Aydemir amesema wataanza na mnada wa mabehewa 17 ya awali katika mnada huo (hadi sasa wateja wawili wamepatikana kutoka Serbia), na mabehewa 13 na vichwa 2 vya treni za mwendokasi vitasubiri hadi mteja apatikane na kisha watavipiga mnada. Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kampuni ya EUROWAGON ya kutoka Turkey ziliingia makubaliano Oktoba 2020 kwa ajili ya ujenzi (ukarabati na utiaji nakshi) wa vichwa viwili vya treni ya umeme na...
MADAI Zipo taarifa zinadai kuwa Jeshi la Tanzania katika wilaya ya Nangade, Cabo Delgado waliingia kwenye mtego wa Magaidi katika kijiji cha Vondanhar, eneo la Palma. Aidha inadaiwa Jeshi la Tanzania lilikuwa likisafiri kwa magari ya kivita sambamba na jeshi la Msumbiji. Magari matatu ya jeshi la Tanzania yamechomwa moto na baadhi ya Silaha kuharibiwa. Taarifa iliyotolewa na kikundi cha Kigaidi cha IS, imedai wamekamata baadhi ya Silaha ikiwemo Chinese Type 81-1 assault rifle pamoja na 12.7x108mm Type 54 HMG ya kwenye gari. Zaidi inaelezwa kuwa haya ni magari ya JWTZ yapo chini ya himaya ya magaidi.
Peace be upon ya' all, Hili swala limezua mjadala wa mda mrefu sana baina ya madaktari wao kwa wao wakivutana kwa hoja kuntu kabisa. Je ni kweli UKIMWI hausababishwi na HIV kwamba agenda nzima ni scam na kuwa hakuna kipimo cha kupima HIV bali vilivyopo hupima tu kushuka kwa kinga?
MADAI Thomas Lungu Sweswe ni mchezaji wa zamani wa Zimbabwe, beki wa kati anadaiwa kushikiria rekodi ya kucheza dakika 90 dhidi ya Keiza Chiefs bila kugusa mpira.
MADAI Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo katika jukwaa la JamiiForums.com, kumekuwa na majadiliano na maswali yanahoji au kutoa taarifa ambazo wengi hawana uthibitisho nazo kuhusu dawa za kuzuia maambukizi ya VVU ambazo muhusika anatakiwa kutumia ndani ya masaa 72. Je, hili lina ukweli? Na inakuaje kwa muhitaji ambaye si muhanga, na gharama zake zikoje? JE, KUNA UKWELI KWENYE HILI?
MADAI Kumekuwa na mtazamo kuwa maziwa ya kwanza ambayo mama huyapata mara baada ya kujifungua si maziwa yafaayo kwa mtoto. kutokana na mtazamo huu wanawake wengine huyakamua na kuyamwaga mpaka yanapotoka maziwa ya rangi nyeupe.
MADAI Kuna magonjwa mengi yanayosababisha upungufu wa Kinga mwilini ikiwemo maambukizi ya VVU. Kumekuwa na mijadala mingi pamoja na tetesi zinazohitaji majibu ya kina kuhusu uwezekano wa kupata VVU/UKIMWI kutoka kwa mtu aliye athirika hasa ikihusisha ushiriki wa tendo la ndoa pasipo kutumia kinga hata kama ni mara moja tu. Ukweli upoje na majibu ya kisayansi yanatoa picha gani? Baadhi hudai hauwezi kupata VVU/UKIMWI kwa kufanya tendo moja tu la ngono na muathirika pasipo kutumia kinga kwa kuwa maambukizi hayaji kirahisi hivyo kama tunavyodhani.
MADAI Yapo maoni ya watu mbalimbali kuwa vyakula vilivyobadiliwa vinasaba GMO ni hatari kiafya na vimetengenezwa mahususi kwa ajili ya kuua kizazi cha watu weusi. Je ukweli upoje kuhusu jambo hili?
Jamii inaamini kuwa kila Mtu anayeugua ugonjwa wa Kifua Kikuu huwa ana maambukizi ya VVU jambo ambalo limekuwa chanzo cha unyanyapaa kwa waathirika Je, ni kweli kila Mtu mwenye kifua kikuu ana maambukizi ya VVU?
MADAI Yapo madai ya kuwa dawa za asili kama ndulele, alovela na vitunguu swaumu ni dawa ambazo huweza kutibu tatizo la mdudu wa kidole. Aidha, wengine wanadai mafuta ya taa au maji ya betri pia huweza kutibu mdudu wa kidole. Ukweli ni upi?
Top Bottom