Mwenyekiti wa BAVICHA taifa John Pambalu naye aanza safari na jeshi la polisi kutoka Mwanza kwenda Dar usiku wa leo kwa ajili ya upekuzi

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Taarifa za uhakika ni kuwa, mwenyekiti wa BAVICHA taifa John Pambalu naye usiku wa leo ameanza safari ya kusafirishwa na jeshi la Polisi kupelekwa Dar kwa ajili ya upekuzi.

Kiongozi huyo pamoja na msaidizi wake wa idara ya uenezi wanatuhumiwa kumiliki mitambo ya kufyatua katiba.
 
Inashangaza sn,halafu watu si wajinga sikuhizi.Kumbambikia mtu kesi kijinga hivi ni ushamba.

Watakufa et hawa watu jamani,mbona hawajifunzi?

Watanzania sikuhizi maombi yao ni makali wakiamua kumshitakia Mungu
 
Swali fikirishi!

Je Polisi wanafanya kazi ya Siasa au kulinda amani na mali ya watu.?

Kitendo cha kuwachukua watu wakiwa wamelala usiku wa manage kabla ya tukio. Je kulikuwa na uvunjifu wowote wa hali ya amani?

Kuwasafirisha watu Mwanza Dar Mwanza ni utopolo wa aina gani huu wakati mitandao watu wanafanya zoom na hata Rais SSH majuzi aliongeleshana na mkuu wa WHO kuomba msaada na kila kitu kilienda.

Polisi wetu mnaonyesha udhaifu wa hali ya juu mno kama hamkwenda shule vile.!!!
 
Huo sio ujanja
Polisi wajanja sana, hawa watu hawana makosa yoyote wanachofanya ni kuwavuruga wasahau malengo yao ya kupigania Katiba Mpya, Chadema waje na plan A+ kukabiliana na hali hii badala ya kuendelea kushangaa huu usanii wa polisi.
 
Back
Top Bottom