Mwigulu aanza tena kampeni zilizomfukuzisha uwaziri awamu ya 5

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Yani huyu waziri bwana, sijui huwa anafanya maigizo ili kumfanya nani mjinga!

Alipokuwa waziri wa kilimo alikutana na watu waliozuia msafara wake huko Iringa wakimsifu. Ila kwa kuwa Magufuli hakutaka hivyo akamuonya akamuhamisha na wizara.

Alipoenda mambo ya ndani napo akawa vile vile na maigizo yake hatimaye Magufuli akaona isiwe tabu. Akamfukuza uwaziri.

Sasa leo eti kule Tunduma napo wamesimamsha msafara wake huku wakimuhimiza azidi kukusanya kodi ili wananchi wapate maendeleo! Imagine igizo kama hili anaenda kuthubutu kulifanyia Tunduma. Eti wanatunduma wanamlalamikia kuwa hawana maji. Ha! Ha! Ha!

Mwigulu yani bado tu hujaachaga ile misifa isiyokuwa na mashiko. Tunduma na wewe wapi na wapi bwana?

Ile tozo ni uwizi wa mchana hilo kaa ufahamu kabisa. Hizo sarakasi zako za kuusaka urais utaishia kuwa Rais wa Kiomboi football club!
itvtz_20210724_190636_0.jpg
 
Tunduma hakuna Wananchi wajinga wa kiwango hicho. Maigizo yake tu kuhalalisha wizi wa Tozo.
Huyu jamaa huwa ana sifa za kishamba kishamba sana. Yani ni yeye tu utasikia maigizo kama haya.
 
ITV ilikuwaga zamani ila Sasa ivi nawaona ni Kama online tv au jumalukole hawana habari za maana. Tunduma ninayoijua kuna watu wamepigwa tozo za mafuta wanaenda kununua Zambia waongee utopolo sio kweli hii habari watafute namna nyingine kuwashawishi watu sio kwa hizi cheap propaganda 🤣🤣 acheni comedyw
 
E7EXvFtWYAUPxYt.jpeg

Wananchi wenye mabango Tunduma mkoani Songwe wamezuia msafara wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Nchemba, wakiitaka serikali kudhibiti ukusanyaji wa kodi ili kupata fedha nyingi zitakazosaidia kukamilisha miradi ya maendeleo.

My Take
Haya ni maigizo kama maigizo mengine,maigizo yenye lengo la kujipigia debe kuelekea 2025.
 
View attachment 1866636
Wananchi wenye mabango Tunduma mkoani Songwe wamezuia msafara wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Nchemba, wakiitaka serikali kudhibiti ukusanyaji wa kodi ili kupata fedha nyingi zitakazosaidia kukamilisha miradi ya maendeleo.

My Take
Haya ni maigizo kama maigizo mengine,maigizo yenye lengo la kujipigia debe kuelekea 2025.
Rubbish, nani ampe urais shetani, Idd Amin mkubwa
 
Back
Top Bottom