Kukumbukia ukatili kumetufanya tusahau matatizo mengine yote kwa muda. Watanzania tujifunze

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Hakuna ubishi kuwa enzi ya utawala wa awamu ya tano wa hayati John Magufuli kulikuwa na vitendo lukuki vilivyokuwa na ukatili mkubwa dhidi ya binadamu. Kuanzia watu kuokotwa fukweni, kupotea, kupigwa risasi, kutishiwa wahame vyama, kunyamazisha vyombo vya habari, kutaifisha, kwenda kinyume na uelekeo wa kimataifa kwenye majanga, wafanyakazi kukosa haki zao za msingi. Haya yote yametufanya watanzania kuugua ugonjwa mbaya wa kuyakumbuka kumbuka tena kwa nguvu ya ajabu.

Leo hii Rais yupo nje ya nchi ila kila analofanya linajibiwa kwa yaliyotokea ya kikatili. Hatuhoji tena mambo mengine na kwa kiasi kikubwa ni kuathiriwa na ukatili uliopita hapo kabla. Kama siyo hayo basi leo ingekuwa ni stories za Rais kuwa nje ya nchi kwa wiki sasa. Tungehoji mengi kweli kweli.

Watanzania tujifunze kikubwa, tujifunze kuwa kamwe watu wetu hawapendi ukatili. Ukiwafanyia ukatili kisha ukakosa muda wa kutosha wa kutubu basi kwa hakika hutoiona mbingu maana utakumbana na machozi kila utakapoamka kwenye nyumba yako ya milele. Kwa hakika hayati huko alipo anapitia magumu sana? Kwanini? Kwasababu hakupata muda wa kukaa pembeni na kuona mwenzake akirekebisha makosa yake huku akitubu. Zingatia makosa yake ni tofauti kabisa na ya watangulizi. Mbaya zaidi alikuwa akiambiwa huku akawa hasikilizi, kosa kubwa sana hili! Kuna watanzania katu hawatokaa wamsamehe Magufuli na hii ni kutokana na jinsi alivyoondoka, kwa hakika tujifunze.

Kwa kila nafasi uliyo nayo jitahidi sana kuepuka ukandamizaji. Ukandamizaji ni mauti kwako kwa siku za mbeleni ikiwa utaondoka kwa staili ya mwenda zake! Tujifunze kweli kweli. Watanzania wanaonekana katu hawajali pale wanapoonbelea ukatili wa mwenda zake. Wanauongea kwa herufi kubwa, mbaya zaidi ni mpaka watu wake wa ndani ya mfumo. Hapo utapata vipi msamaha?

Magufuli pengine angepata nafasi akastaafu kisha akaona jinsi mwenzake anavyoenda basi angekuwa na unafuu mkubwa hata angepata toba ya kweli. Ila ndiyo hivyo, sisi tuliobaki tujifunze. Ukatili dhidi ya mwenzako ni dhambi yenye uzito mkubwa sana na inahitaji muda mrefu wa toba ya kweli ili upate msamaha. Tujitahidi kuuepuka na hata ikitokea basi iwe ni bahati mbaya sana.
 
Chadema haifungamani na awamu yoyote hadi sasa!

Iko kkmaslahi zaidi kama fisi anayenyemelea mkono wa binadamu skiamimi utasnguka aule.
 
Back
Top Bottom