magufuli

 1. Dam55

  Magufuli ni Rais anayekumbuka ahadi zake na kuzitimiza bila unafiki

  Kama uko makini kuangalia anayo yafanya Rais Magufuli utagundua kuwa ni Yale aliyo yasema kwenye ahadi zake wakati wa kampeni. Mfano: 1. Aliahidi kufufua shirika la ndege (watu walishangilia nadhani hawakujua madhara yake na labda hawakujua ni kwa namna gani atafufua hilo shirika), ahadi hii...
 2. Hivi punde

  Waziri Jaffo: Mwezi April 2020 nitamkabidhi Rais Magufuli orodha ya Wakurugenzi wavivu

  Waziri wa nchi Tamisemi, Seleman Jafo amesema ana majina ya wakurugenzi wasiokwenda na kasi ya utendaji kazi wa Serikali ya Tanzania, atayakabidhi kwa Rais John Magufuli Aprili, 2020. Jafo ameeleza hayo leo Jumatano Januari 22, 2020 mjini Dodoma wakati akikabidhi mashine 7227 za kukusanyia...
 3. technically

  Kituo cha kazi cha Rais Magufuli ni Chato, Magogoni au Dodoma?

  Maana akikaa Dodoma wiki anaenda Chato anakaa mwezi anakuja Dar kuapisha mabalozi anakaa wiki 3. Hivi pesa za walipa kodi kiasi gani zinapotea kwa huu uzembe wa kuishi ikulu tatu kwa wakati mmoja? Watanzania waambiwe ukweli kama pia Ikulu ya Dodoma haikaliki maana huu ni kama utapeli na...
 4. figganigga

  News Alert: Rais Magufuli amteua tena Lyatonga Mrema kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Parole

  Rais Magufuli ateua wenyeviti 5 wa bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa. Mara kwanza Mrema aliyeteuliwa na Rais John Magufuli kuongoza bodi ya Parole Julai16, 2016, na muda wake kuisha Julai 16, 2019 baada ya kutimiza kipindi cha miaka mitatu cha kuongoza bodi hiyo. Na leo 20 January...
 5. idawa

  Rais Magufuli abatilisha muda wa usajili wa laini za simu kwa kutumia Vitambulisho vya NIDA kama ilivyotangazwa awali na TCRA

  Amesema watanzania wapo milion 55 lakini waliosajiliwa NIDA ni million 15 tu. Hivyo tangazo la TCRA kuwa mwisho tarehe 1 mwezi wa tano itapelekea watanzania zaidi ya milioni 25 kukosa haki ya kumiliki mawasiliano. Ameongeza muda mpaka tarehe 31 mwezi wa kumi na mbili, hata hivyo muda utakuwa...
 6. J

  Rais Magufuli amualika Sultan mpya wa Oman kutembelea Tanzania wakati wowote

  Rais Magufuli amemualika Sultan mpya wa Oman kuitembelea Tanzania wakati wowote. Salamu za Rais Magufuli zimetolewa na Waziri wa mambo ya nje Prof Kabudi aliyeko nchini Oman alikotumwa na Rais Magufuli kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha Sultan wa nchi hiyo. Source: Channel ten
 7. J

  Umoja wa Afrika ( AU) wampongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo ndoto za mwalimu Nyerere za kuiunganisha Afrika

  Kamishna wa AU mh Bade kwa niaba ya Umoja wa Afrika amempongeza kwa dhati Rais wa Tanzania Dr Magufuli kwa kuzitekeleza kwa vitendo ndoto za mwalimu Nyerere za kuiunganisha bara la Afrika. Bade ametoa pongezi hizo jijini Arusha wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la makao makuu ya...
 8. technically

  Anguko la Rais Magufuli litakuwa na mshindo mkubwa sana

  Uchaguzi unakaribia watu hawataki kuvunja katiba wanamsubiri alivunje bunge waanze kumrarua kutoka pande zote. Sio ndani ya vyombo vya usalama, Sio ndani ya ccm wala ndani ya upinzani wote watapeleka mashambulizi juu ya hoja za Usalama wa taifa na utekaji wa watu, kuanguka kwa Uchumi, Ajira...
 9. Mzee Mwanakijiji

  Swali la Ugomvi: Injinia Kamwelwe mnataka Rais Magufuli awabebeje ATCL?

  Hili ni swali ambalo linahitaji kujibiwa kwa usahihi, kwa haraka na kwa umakini. Ni kitu gani ambacho Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linahitaji kufanyiwa na Rais Magufuli ili liweze kutengeneza hadhi inayostahili shirika la kitaifa? Huku ndiko ninakokuita kubebeka. Hadi hivi sasa Magufuli...
 10. G Sam

  Nani atakuja kutufidia sisi kama nchi kutokana na mradi usio na tija wa SGR?

  Kwakweli huu mradi kila nikiuangalia na complications zake huwa nakuna kichwa sana na kujiuliza kina nani walipendekeza mradi wa aina hii? Pamoja na usanifu wake kujikita kwenye gharama za juu bado sijawahi kuona faida ya mradi huu na sijui kama utakuja kukamilika. Mbaya zaidi umeshatushinda...
 11. KAWETELE

  Mbeya: Agizo la Rais Magufuli la kugawa eneo la Airport ya zamani kwa wamachinga latekelezwa

  Ikumbukwe eneo hilo liliombwa kwa Mh. Rais na Naibu spika Dr. Tulia siku ya tarehe 26 April 2019. Zaidi soma https://www.jamiiforums.com/threads/mbeya-rais-magufuli-ahutubia-wananchi-uwanja-wa-ruanda-nzovwe-agusia-usajili-wa-laini-na-machinga.1577226/ Tangu juzi wafanyabiashara wadogo wadogo...
 12. S

  Dar es Salaam: Rais Magufuli aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumanne Januari 14, 2020 ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
 13. M

  Mzalendo wa kweli wa Tanzania hawezi kamwe kumuunga mkono Rais Magufuli

  Mzalendo wa kweli kwa Tanzania yetu hii (bila kujali msimamo wake kisiasa au kidini) ni lazima atatetea haki, atapinga uonevu na kukataa ubadhilifu, rushwa na ufisadi. Magufuli anafanya yote yaliyo kinyume na sifa zinazotakiwa kwa mzalendo. 1. Ni mtu asiefuata sheria (unless sheria hiyo...
 14. Patriot

  Mtindo wa Magufuli ni moja ya dawa ya matatizo yetu

  Kwa maoni yangu, tuliposhindwa kuunda katiba mpya ilikuwa ni ishara ya utawala mbovu kabisa! Kwamba Bunge na Serikali vyote vilikuwa viko taaban! Yawezekana biashara ya Ndege ni mbaya lakini kila taifa hutamani kuwa na ndege chache. Treni ni muhimu pia. Tujiulize Ilikuwaje kwa miaka yote hiyo...
 15. J

  Sherehe za Mapinduzi uwanja wa Amani Zanzibar Rais Magufuli na Dr Shein kuhudhuria

  Sherehe hizi zitarushwa mubashara kupitia TBC, Channel ten, Azam tv, ITV nk Rais Magufuli wa JMT na Rais Shein wa Zanzibar watawaongoza maelfu ya watanzania katika maadhimisho hayo. Karibuni! Up dates; Viongozi wastaafu wameshaingia ukumbini wakiwemo mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Sumaye...
 16. J

  Rais Magufuli: Wasukuma na Wanyamwezi wengi walikuja Zanzibar na kutorudi tena usukumani akiwemo baba yangu mkubwa

  Rais Magufuli amesema Zanzibar ni kisiwa cha raha hata watanzania bara wengi wanapohitaji kupumzika huja Zanzibar. Rais Magufuli amesema hata kaka wa baba yake alikuja Zanzibar na kubakia huko huko kama ilivyokuwa kwa wasukuma na wanyamwezi wengi. Chanzo: Channel ten
 17. J

  Live ITV: Rais Magufuli anafungua Hotel ya Verde Azam Luxury Resort & SPA mtoni jijini Zanzibar inayomilikiwa na S S Bakhresa

  Ni tukio kubwa na la kihistoria kwani hii ni hoteli ya kipekee kabisa nchini Tanzania, Afrika mashariki na kusini mwa jangwa la Sahara. Karibuni!
 18. beth

  Rais Magufuli: Ni aibu Shule za Zanzibar kuwa za mwisho, Wakandarasi wakikupa 10% kula ila simamia Sheria

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema ni sa aibu kuona shule za Zanzibar zinakuwa miongoni ambazo hazifanyi vizuri pindi inapofika wakati wa kutangaza matokeo ya Shule za Sekondari. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye uwekaji wa jiwe la...
 19. miss zomboko

  Rais Magufuli kuanza ziara Visiwani Zanzibar

  Rais John Magufuli leo anatarajiwa kuanza ziara yake ya kikazi visiwani Zanzibar baada ya jana kuwasili Dar es Salaam akitokea chato kwa mapumziko. Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ilieleza kuwa Rais Magufuli leo ataanza ziara ya kikazi...
Top