G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Niliposoma gazeti la MWANANCHI la leo ni kuwa yupo DC mmoja mteule ambaye anatokea kwenye tasnia ya wasanii ambaye alienda nchini India kwenye chuo kikuu cha Bangalore akisomea shahada ya kwanza kwenye mambo ya sanaa huku matokeo yake ya kidato cha sita yakiwa hayajatoka.
Kwa mujibu wa gazeti hilo ni kuwa Mchopanga huyo alipata udhamini na moja kwa moja kwenda kwenye masomo hayo kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2009 ambapo aliondoka nchini na kudahiliwa chuoni hapo bila ya kuwa na matokeo hayo.
Upo uwezekano kuwa kwenye elimu ya huyu DC mteule kuna utata na usanii na hata shahada yake ni ya mambo ya usanii.
Anajisemea kuwa anatarajia kwenda chuo kikuu cha Dar es Salaam kusomea shahada ya pili kwenye mahusiano ya umma.
NB: Wapo marafiki zangu kibao waliotokea hapo Bangalore na kujitapa kuwa wana shahada ila walipoambiwa kuleta vyeti wengi wao ni ukweli walitunukiwa shahada zao za kwanza kwa kutumia matokeo ya vyeti vya kidato cha nne kama "Direct entry qualifications" na huenda Mchopanga ni mmoja wao. Je, NACTE wameanza lini kuthibitisha kuwa shahada za aina hii ni credible kwa nchi yetu?