Habari za muda huu Wakuu,
Wakuu mimi leo nina swali hapa maana nimekutana na kitu nimeshindwa kuelewa cha kufanya.
Nimemwomba mpenzi wangu shilingi 50,000 ila akasema hana na ana 20,000/- hivyo ananitumia lakini katika kutuma amenitumia 200,000/- 😊
Unashauri nifanye nini?
Papua New Guinea imekusanya vikosi vya usalama baada ya uporaji na ghasia nchini kote. Ufinyu wa ajira na kupanda kwa gharama ya maisha kumezua hali ya kufadhaika katika taifa hilo la Pasifiki Kusini
Waziri Mkuu wa Papua New Guinea James Marape alitangaza hali ya hatari ya wiki mbili katika mji...
Vituo vya Mafuta vinajengwa kila sehemu hadi kwenye makazi ya watu. Kwanini Serikali inatoa vibali kwa sehemu hatarishi?
Kuna vituo vingi sana vya mafuta vinajengwa katika maeneo hatarishi kwa jamii na Serikali sijui inaridhia ujenzi huu kwa namna gani? Sijui kwanini haifikirii?
Nakumbuka...
Maadhimisho ya Siku hii hufanyika kila Juni 05, na kwa mwaka 2023 yanaangazia zaidi Uchafu wa Mazingira unaotokana na Taka za Plastiki, na jinsi ya kukabiliana nao
Zaidi ya Tani Milioni 400 za Plastiki zinatengenezwa Duniani kila mwaka. Inakadiriwa kuwa, Tani Milioni 19 hadi 23 huishia...
Kwa Mujibu wa Takwimu za Umoja wa Mataifa (UN) kufikia Novemba 2022, idadi ya Watu Duniani inakadiriwa kuwa Bilioni 8. Ongezeko la Watu katika Nchi nyingi zenye Uchumi wa Chini linakadiriwa kuongezeka mara mbili zaidi kati ya Mwaka 2022 na 2050
Kufikia Mwaka 2022, idadi ya Wanaume Duniani...
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Michezo kwa Maendeleo na Amani ni fursa ya kutambua mchango chanya wa Michezo katika Jamii na Maisha yetu
Michezo ina nguvu ya kuimarisha uhusiano katika Jamii, na kukuza Maendeleo endelevu, Amani pamoja na mshikamano wa watu wote
Mbali na Michezo kuwa na...
Stress kwasababu ya Kazi inapokuwa kubwa kupita kiasi, inaweza kukuathiri kimwili na kihisia
Kwa watu wengi, sio rahisi kuepuka 'Stress' hata kama unapenda kile unachofanya
Unarudi vipi kwenye mstari mambo "yanapokuwa mengi" kazini?
=====
Work-related stress can get the best of us all...
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, 7% ya Watanzania wanaathiriwa na Ugonjwa wa Figo na idadi ya Wagonjwa inaongezeka
Inashauriwa kuzingatia Lishe Bora, kula Matunda/Mbogamboga, kupunguza kiasi cha Chumvi pamoja na Matumizi ya Pombe na Tumbaku
Mtindo wa Maisha na Vyakula tunavyokula vinaweza...
Ili kuongeza Ushiriki wa Wanawake Mtandaoni, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Nathan Belete amesisitiza umuhimu wa Mafunzo ili kuwapa Wasichana Ujuzi wa Kidigitali
Ameshauri wigo wa upatikanaji wa Intaneti uongezeke, na gharama ya Huduma hiyo iwe nafuu ili kuwafikia Wanawake wengi zaidi...
Kufikia Mwaka 2022, 48% ya Vijana (Miaka 15 hadi 24) katika Nchi zinazoendelea walikuwa wanatumia Mitandao.
Hii inatoa taswira kuwa Vijana wengi wanajitahidi kukumbatia Teknolojia kama nyenzo muhimu katika Maisha yao, lakini huenda Mazingira yaliyopo si rafiki kwao.
Kama Kijana, vitu gani...
Kwa mujibu wa Ripoti ya Statista, Waafrika wengi wanashindwa kutumia Intaneti kutokana na gharama ya Huduma hiyo kuwa kubwa
Wananchi kutoka Mataifa mbalimbali Barani humo wanategemea Mtandao ili kupata Huduma muhimu, lakini wanatumia gharama kubwa ili kuweza kupata Intaneti
Gharama zinapokuwa...
Watendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EC) wametakiwa kuondoa TikTok katika Vifaa vyao kufikia Machi 15, 2023
Mtandao huo Maarufu umehojiwa mara kadhaa kuhusu Usalama wake kutokana na madai unavuna Taarifa Binafsi za Wateja na kuzitoa kwa Serikali ya China
Nini maoni yako kuhusu hatua hii...
Seneta Gloria Orwoba wa nchini Kenya amesema anafikiria kuachana na Mtandao wa Twitter kutokana na Unyanyasaji wa Kimtandao. Ameeleza, "Hili suala la kuwa na ngozi ngumu HAPANA! Sisi ni Binadamu"
Kwa Mtazamo wako, Unyanyasaji/Uonevu ni sababu mojawapo inayopelekea baadhi ya Viongozi kuepuka...
Leo Februari 15 ni Siku ya Kimataifa ya Saratani kwa Watoto
Inakadiriwa Watoto na Vijana wa hadi miaka 19 wapatao 400,000 hugundulika na Saratani kila mwaka.
Ugonjwa huo ni sababu kuu ya Vifo licha ya Saratani nyingi za Watoto kutibika.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), baadhi...
Ripoti Mpya iliyochapishwa na Shirika la Top10VPN inasema kukosekana Mtandao huko Tigray, Ethiopia Mwaka 2022 kumezigharimu Biashara Nchini humo Dola za Marekani Milioni 145.8
Kuzuia Intaneti pamoja na kuweka vikwazo katika Upatikanaji wake huwaathiri Wananchi Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa...
Siku hii inaadhimishwa kila Oktoba 5 kama ishara ya Heshima na Shukrani kwa Walimu kutokana na Mchango walionao katika Ustawi wa Wanafunzi, Jamii na Nchi kwa ujumla.
Ili kuleta Mabadiliko katika Sekta ya Elimu, ni muhimu Walimu wasikilizwe, na mazingira yao ya kazi yaboreshwe. Bila Walimu Bora...
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu mnamo mwaka 2019 kilifungua shauri dhidi ya Serikali ya Tanzania kwa niaba ya wasichana wa Tanzania katika Kamati ya Afrika ya Wataalamu ya Haki na Ustawi wa Mtoto
Shauri hilo lililenga kuwatetea wasichana wa Tanzania wanaopata ujauzito wakiwa bado shuleni...
Miongoni mwa misingi muhimu ya Demokrasia ni Uhuru wa Kujieleza, Uchaguzi Huru na wa Haki, na kuheshimu Haki za Binadamu
Demokrasia ni pamoja na Vyombo vya Habari kuwa Huru na Wananchi kushiriki kikamilifu katika Masuala yanayogusa Maisha yao. Hii hujenga Jamii yenye kuiwajibisha Serikali...
Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) unalenga kutambulika kama moja ya Nchi zenye Ubunifu wa Hali ya Juu zaidi duniani, na hilo kimekuwa likidhihirishwa kupitia Majengo yake ya kuvutia
Hoteli ya Kitalii ya 'Moon Dubai' inatarajiwa kugharimu Dola Bilioni 5 (Tsh. 11,585,000,000,000). Itakuwa na urefu...
Kujiua ni suala la Afya ya Umma linaloathiri watu duniani kote. Kwa mujibu wa Shirika la Afya (WHO) katika kila sekunde 45, mtu mmoja hukatisha uhai wake.
Inakadiriwa Watu 703,000 Duniani hujiua kila mwaka. Mamilioni ya watu huathiriwa na tabia za kutaka kujiua kutokana na sababu mbalimbali...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.