intaneti

Intaneti (kutoka Kiingereza Internet) ni mfumo wa kushirikiana kwa tarakilishi nyingi unaowezesha watu mbalimbali duniani kuwasiliana baina yao. Kupitia mtandao huo, watu huweza kutembelea tovuti mbalimbali, kupiga gumzo, na kuandikiana barua pepe.

Intaneti ni mfumo wa kimataifa wa mitandao ya tarakilishi inayotumia itifaki inayokubalika ya intarnet Suite (TCP/IP). Intaneti hubeba safu kubwa ya huduma na rasilimali za habari hasa hati za HyperText zilizoshikanishwa za wavuti wa ulimwengu mzima (www) na miundombinu ya kusaidia barua pepe.

Mbinu nyingi za jadi za mawasiliano ya habari, kama vile huduma za rununu na runinga, zimeundwa upya kutumia teknolojia za tovuti, na kusababisha huduma kama vile itifaki ya kupitisha sauti kwa kutumia tovuti (VoIP) na IPTV. Uchapishaji magazeti umeundwa upya katika tovuti, ubadilishanaji maoni, na kupatikana habari zinapotokea tu. Intaneti imewezesha au kuharakisha uundaji wa aina mpya za mafungamano za kibinadamu kupitia ujumbe mbashara, majukwaa ya tovuti na mitandao ya kijamii.

Kuna mawasiliano ya tarakilishi pamoja na habari zinazotunzwa kwenye mashine na kupatikana kwa programu za kutafuta wavuti (kama google) au kwa kamusi elezo kama wikipedia.
  1. M

    JamiiForums Tanzania Pongezi kwa Mkurugenzi wa TTCL, Moremi Marwa, kwa juhudi kubwa za usambazaji wa fiber internet mitaani, yenye bei nafuu na kasi kubwa

    Sasa TTCL wameamua kuingia mazima kwenye huduma za intaneti ya kisasa. Usambazaji wa fiber internet unaendelea kwa kasi kubwa, hasa maeneo ya mijini ambako huduma hii inazidi kuwafikia wananchi wengi zaidi. Tofauti na zamani, sasa wanafika hadi mitaani, wakizungumza na wakazi moja kwa moja ili...
  2. Dalton elijah

    JamiiForums Tanzania Wadau wajadili hasara kuzimwa intaneti wakati wa uchaguzi

    KUZIMWA kwa intaneti wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kumelisababishia Taifa hasara ya dola za Marekani milioni 238, sawa na takribani Sh. bilioni 560, kwa mujibu wa ripoti mpya ya utawala wa kidijitali. Takwimu hizo zimetolewa na Ofisa Sera na Teknolojia wa Tech, Media Convergency (TMC)...
  3. eli -DEFIANT- cohen

    JamiiForums Tanzania Sidhani kama kuna mtandao mbovu katika huduma za intaneti kama walivyo Airtel

    Na ukongwe wote huu intaneti tunapata ya bra bra . Sio tu routers zao hata simu pia.
  4. R

    JamiiForums Tanzania Mbunge Devotha Mburarugaba: Wanawake wakienda kuomba mkopo wanaaambiwa intaneti ipo chini

    Mbunge viti Maalum wa Kagera Devotha Daniel Mburarugaba kwenye kipindi cha maswali na majibu bungeni leo Februari 5, 2026 amehoji Serikali imeweka mikakati gani kuhahakikisha maafisa wanapata vitendea kazi kwani wanawake wakienda kuomba mikopo wanaambiwa intaneti ipo chinihawawezi kupata huduma...
  5. M

    JamiiForums Tanzania, JamiiForums Uganda Wananchi: Kuzimwa kwa intaneti kote nchini wakati wa uchaguzi mkuu kumeathiri vibaya uchumi na maisha

    Kuzimwa kwa intaneti kote nchini Uganda wakati wa uchaguzi mkuu kumeathiri vibaya uchumi na maisha ya wananchi, hususan wafanyabiashara na vijana wanaotegemea huduma za mtandaoni. Biashara za fedha kwa njia ya simu zilisimama, waendeshaji bodaboda waliopata wateja kupitia programu walipoteza...
  6. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania, JamiiForums Uganda Waziri Balaam amesema intaneti kutopatikana Uganda ni baada ya Meli kuharibu Nyaya (fibre optic) Mombasa

    Kituo cha Televisheni cha Taifa (UBC) kimemhoji Waziri wa Nchi, Masuala ya Vijana na Watoto, Balaam Barugahara Ateenyi, kuhusu tatizo la mtandao nchini Uganda. Waziri alieleza sababu za kufungwa kwa intaneti. Waziri amesema kuwa awali, Kamisheni ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) ilifunga intaneti...
  7. Nyani Ngabu

    JamiiForums Tanzania Unawaomba radhi wageni kwa kuwakatia intaneti kwa siku 6 halafu wazalendo uliowaua hata majina yao unajifanya hauyajui!

    https://www.washingtonpost.com/world/2026/01/15/tanzania-samia-suluhu-hassan-internet-shutdown-october-election/21b8d8a0-f24f-11f0-a4dc-effc74cb25af_story.html Huyu Samia ni kiumbe wa ajabu sana. Katika busara zake kaona ni sahihi kuwaomba radhi mabalozi kwa kuzima intaneti wakati ule wauaji...
  8. Mafyangula

    JamiiForums Tanzania, JamiiForums Uganda kupambana na Upotoshaji na Vurugu, UCC yazuia baadhi ya huduma Intaneti kwa muda

    Kufuatia mapendekezo mazito kutoka Kamati ya Usalama ya Taasisi za Serikali (Inter-Agency Security Committee), Tume ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) siku ya Jumanne ilitoa maelekezo kwa waendeshaji wote wenye leseni wa mitandao ya simu (MNOs) na watoa huduma za intaneti (ISPs) kusitisha kwa muda...
  9. R

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Waziri Simbachawene: Hadi sasa hakuna tishio TCRA kuzima internet

    Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema uamuzi wa kuzima mtandao wa internet ni chaguo la mwisho kabisa pale ambapo hali ya kiusalama inakwa mbaya ambapo amesema hadi kufikia sasa hali ya Tanzania bado ipo shwari na hakuna tishio la kuwafanya TCRA wazime internet kesho December...
  10. Mafia Island Boy

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Kuzimwa kwa Intaneti wakati wa uchaguzi wa 2025, kuliumiza wengi, haki ya kupata taarifa iliminywa

    Tarehe 29 Oktoba 2025, Tanzania iliingia kizani kimawasiliano baada ya Mamlaka kuzima Mtandao wa intaneti (internet), upande wa pili Serikali ikidai kufanya hivyo kumeweza kuwadhibiti waandamanaji kuhamasishana kuandamana. Kuzimwa kwa Mtandao kulisababisha madhara mengi kwa Wananchi ikiwa...
  11. JanguKamaJangu

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 TCRA: Hatukuzima intaneti Oktoba 29, 2025

    Wakati kukiwa na malalamiko ya wananchi na jumuiya ya kimataifa kuhusu hatua zilizochukuliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima intaneti intaneti siku ya uchaguzi Oktoba 29, 2025, mamlaka hiyo imekanusha ikisema, “TCRA haikuzima intaneti bali ilichukua hatua za...
  12. R

    JamiiForums Tanzania GE2025 Netblocks: Mitandao ya kijamii bado Inakabiliwa na vikwazo licha ya Intaneti kurejeshwa Tanzania

    Kwa mujibu wa taarifa za NetBlocks, takwimu za moja kwa moja zinaonyesha kuwepo kwa vikwazo vikubwa kwenye mitandao ya kijamii na programu za ujumbe nchini Tanzania, hata baada ya huduma za intaneti kuanza kurejea taratibu kufuatia kukatikwa kwa mtandao kwa zaidi ya siku tano tangu Oktoba 29...
  13. M

    JamiiForums Tanzania GE2025 Waangalizi wa Uchaguzi wa Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika: Serikali ya Tanzania isitishe amri ya kutotoka nje na kurejesha huduma za Intaneti

    TAARIFA YA AWALI KUHUSU UCHAGUZI MKUU WA TAREHE 29 OKTOBA 2025 KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Leo, tarehe 31 Oktoba 2025 - Sambamba na dhamira yake ya kukuza chaguzi za kuaminika, amani, huru, na haki kupitia uangalizi wa kikanda usio na upendeleo na uchambuzi kote Afrika Mashariki na...
  14. JanguKamaJangu

    JamiiForums Tanzania TCRA: Watumiaji wa Huduma ya Intaneti wameongezeka kutoka Milioni 54.1 (Juni 2025) hadi Milioni 56.3 (Septemba 2025) sawa na 4.1%

    Huduma ya intaneti inaonesha kuongezeka utumiaji kutoka milioni 54.1 mwezi Juni 2025 hadi kufikia milioni 56.3 mwezi Septemba 2025 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 4.1. Kwa mujibu wa ripoti ya takwimu ya sekta ya Mawasiliano ya robo mwaka inayoishia Septemba 2025 inaonesha idadi ya...
  15. S

    JamiiForums Tanzania Unachangamoto ya kompyuta kutumia bando la Intaneti sana? Suluhisho ni data saver

    Unachangamoto ya kompyuta kutumia bando la Intaneti sana? Suluhisho ni data saver, Bei 30,000 Tsh. Programu ya data saver itakusaidia kuepusha Windows OS kujiupdati na kuzuia background usage la bando lako. Napatikana mkoa wa Dar es salaam, Mbezi. Mawasiliano: 0756704145
  16. S

    JamiiForums Tanzania Unahitaji kupunguza matumizi ya kifurushi Cha Intaneti kwenye PC kompyuta Yako?

    Unahitaji kupunguza matumizi ya kifurushi Cha Intaneti kwenye PC kompyuta Yako? Jipatie Data saver programu. Utaokoa matumizi ya kifurushi Chako Cha Intaneti Eneo: Dar es salaam, Mbezi Gharama: 10,000 Tshs Mawasiliano: 0756704145
  17. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Mbunge Nollo: Kuna Intaneti ya Mitandao ya Simu inasumbua kama kuni mbichi

    Mbunge wa Bahi, Kenneth Ernest Nollo amesema kuna mazingira kadhaa yanayosababisha Watu wengi kutotumia intaneti ikiwemo baadhi ya Mitandao ya Simu kuwa na huduma mbovu ya intaneti.
  18. Mtoa Taarifa

    JamiiForums Tanzania Waziri Jerry Silaa: Watumiaji wa Intaneti wamefikia Milioni 49.3 kutoka Milioni 37

    Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari , Jerry Silaa amesema Watumiaji wa intaneti nchini wameongezeka kutoka milioni 37.3 April, 2024 hadi milioni 49.3 April, 2025 sawa na ongezeko la asilimia 32.3. Waziri Silaa amesema hayo leo May 16,2025 wakati akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma...
  19. Teknolojia ni Yetu sote

    JamiiForums Tanzania Elon musk kuzindua huduma ya intaneti satellite ya Starlink nchini Uganda

    Katika kuhakikisha Mtandao wa Starlink unazidi kushika Kasi ulimwenguni Tajiri Elon Musk ameamua kuongeza nguvu zaidi kwa kuleta huduma hii nchini Uganda. Mtandao wa Starlink ambao unasifika kwa kutoa intaneti yenye Kasi na usio na wasiwasi Hatimaye wameomba leseni Rasmi ya kufanya kazi nchini...
  20. S

    JamiiForums Tanzania Windows 7,8, 10, 11. Okoa kifurushi Cha Intaneti na data saver 99%

    Data saver 99% software inasaidia kudhibiti matumizi ya kifurushi Chako Cha Intaneti kwa kuchagua programu gani itumie intaneti kwa wakati unaotaka kwenye kompyuta (Windows OS 7, 8, 10, 11) yako. Programu inauzwa 30,000 Tsh. Kumbuka bila kuwa na hii programu kifurushi Chako Cha Intaneti...
Back
Top Bottom