Ushiriki wa Wanawake Mtandaoni: Ujuzi na Gharama zatajwa kukwamisha wengi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Ili kuongeza Ushiriki wa Wanawake Mtandaoni, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Nathan Belete amesisitiza umuhimu wa Mafunzo ili kuwapa Wasichana Ujuzi wa Kidigitali

Ameshauri wigo wa upatikanaji wa Intaneti uongezeke, na gharama ya Huduma hiyo iwe nafuu ili kuwafikia Wanawake wengi zaidi

6FD431CC-ADFF-4942-9282-0A78EB1B5DA1.jpeg


Ameeleza hayo katika Kongamano la Wanawake na Teknolojia leo katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC Machi 07, 2023 Jijini Dar es Salaam

Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi ya LP Digital kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali. Mgeni rasmi ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye

Akizungumza katika Kongamano hilo Waziri Nape Nnauye amesema Matumizi ya TEHAMA yameongezeka duniani, lakini ushiriki wa Wanawake na Vijana bado upo chini

Amesema licha ya idadi ya Wanawake kuwa kubwa hapa Nchini kama ilivyobainika katika Sensa ya Mwaka 2022, Sekta ya Teknolojia bado ina pengo kubwa la kijinsia

20C6DDFF-D30B-461B-A1E3-1E7556370EAE.jpeg


D9651B10-6891-452B-B8EF-E883CD2BE3F9.jpeg
 
Sio kwamba hawana opportunities za kutangaza ila mitaji midogo. Serikali ukieakopesha wanawake mikopo ya riba ndogo watafanya vyema. .

Na wale wanaouza telegram, badoo, twitter, Facebook basi watozwe kodi serikali iingize mapata
 
Back
Top Bottom