Haki za Wasichana: LHRC yashinda kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu mnamo mwaka 2019 kilifungua shauri dhidi ya Serikali ya Tanzania kwa niaba ya wasichana wa Tanzania katika Kamati ya Afrika ya Wataalamu ya Haki na Ustawi wa Mtoto

Shauri hilo lililenga kuwatetea wasichana wa Tanzania wanaopata ujauzito wakiwa bado shuleni na kunyimwa nafasi ya kuendelea na masomo. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kiliwasilisha masuala matano ambayo yanavunja haki za wasichana ikiwemo:

1) Vipimo vya mimba vya lazima kwa wasichana mashuleni
2) Kufukuzwa kwa wasichana wanaopata ujauzito na walio kwenye ndoa mashuleni
3) Kuwazuia wasichana wanaopata ujauzito kurudi shule hata pale wanapojifungua
4) Kuwafunga watoto wanaopata ujauzito na kuendelea kuwahukumu watoto ambao wamenyayaswa na kufanyiwa ukatili
5) Kutokuwa na elimu na taarifa sahihi ya afya ya uzazi mashuleni

Sababu hizo zinapekela uvunjifu wa haki za wasichana wa Tanzania kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto kama ifuatavyo:

1) Haki ya elimu
2) Haki ya usawa na kutobaguliwa
3) Haki yakulindwa dhidi ya masuala ya kijamii yenye madhara
4) Maslahi mapana ya Mtoto
5) Haki ya Afya Pamoja na upatikanaji wa afya ya uzazi
6) Haki ya Faragha
7) Haki ya kuwa huru dhidi ya ukatili, unyanyasaji namateso

Ndani ya muda wakati shauri likiendelea katika Kamati, Serikali ilitoa tamko kurudisha watoto shule hapo mwaka 2021 pamoja na kutengeneza mwongozo wa jinsi ya kuwarudsha shule mnamo Februari mwaka 2022.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinapenda kuutarifu umma wa Tanzania kuwa kimeshinda kesi hiyo na kuwa Kamati katika kikao chake cha kawaida cha 39 imeamua kuwa hata mwongozo ulioandaliwa na Serikali haukidhi vigezo vya ulinzi wa haki za wasichana kama ilivyoainishwa kwenye Mikataba wa Afrika wa haki na ustawi wa mtoto ambao Tanzania imeridhia. Kamati wametoa sababu kama ifuatavyo:

- Mwongozo haujazungumzia masuala ya muhimu yaliyowasilishwa ikiwemo upimaji mimba wa lazima, kufukuzwa kwa wasichana shuleni wanapopata ujauzito

- Mwongozo haujaweka wazi kuhusu wasichana waliofukuzwa shuleni bali umeelezea wazi kuhusu wanafunzi wanaoacha masomo kwa sababu mbalimbali ukizingatia kanuni za elimu zinazoruhusu ufukuzwaji wa wasichana kwa kigezo cha maadili bado zinaendelea kutumika

- Mwongozo una ukomo wa muda kwani unaruhusu wanafunzi walioacha shule miaka miwili kabla ya mwongozo na haki za wasichana waliowakilishwa katika kesi hii kuendelea kuvunjwa

- Mwongozo haujasema lolote kuhusu kuhusu kufutwa kwa sheria ya elimu na sheria nyingine kandamizi ikiwemo pia utungwaji wa sheria au sera ya kuwaruhu watoto kurudi shule

Kupitia hayo Kamati hiyo imemuru yafuatayo;

1. Serikali ya Tanzania kukomesha upimaji wa ujauzito wa lazima mashuleni

2. Kupitia sheria ya elimu, 2002 pamoja na kanuni zake na kuondoa mimba pamoja na ndoa za utotoni kama vigezo vya kuwafukuza watoto shule

3. Kuchukua hatua stahiki kuzuia watoto wa kike kufukuzwa shule pale wanapoingia kenye ndoa au kupata ujauzito bali kuweka sheria mahususi na sera kuwalinda watoto dhidi ya ndoa na mimba

4. Kufuta sera zinazozuia watoto kurudi shule ikiwemo kwa sababu za mimba au ndoa

5. Kuwaruhusu watoto walionyimwa nafasi ya elimu kwa sababu hizo kurudi shule haraka iwezekanavyo na kuwafidia kwa muda wote waliopoteza

6. Kutoa mwongozo kwa wakuu wa shule na wasimamizi wa elimu kuwa wasichana wanaoacha shule sababu ya mimba au ndoa wanaruhusiwa kurudi shule

7. Kufanyia uchunguzi kesi za watoto wa kike waliowekwa gerezani kwa sababu ya mimba na kuhakikisha wanaaachiwa haraka na pia kuacha mara moja kuwaweka ndani wasichana wanaopata ujauzito

8. Kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana balehe na kutoa huduma rafiki za afya ya uzazi.

9. Kutoa elimu kwa walimu, wahudumu wa afya, polisi na watendaji wengine kuhusu wasichana wanaopata ujauzito au walioongia kwenye ndoa

10. Kuchukua hatua za muhimu kuondoa ndoa za utotoni nchini Tanzania na mila nyingine zilizopitwa na wakati

11. Kuchukua hatua stahiki kuhusu ukatili wa kijinsia, ubaguzi, umasikini na mila na desturi zilizopitwa na wakati

12. Kuweka mifumo ya utoaji taarifa kwa wahanga wa ukatili wa kingono ikiwemo ndoa za utotoni na kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wahanga

13. Kufanyia uchunguzi na kuwachukulia hatua wanaoshtakiwa kwa ndoa za utotoni na ukatili wa kingono

14. Kuchukulia hatua kuhusu watu wote wanaohusika na upimaji wa mimba wa lazima na wanaowabagua wasichana kuhusu hali yao ya mimba, ndoa na masuala mengine

15. Kutoa huduma maalum kwa wasichana wanaopata ujauzito na walioingia kwenye ndoa kuendelea na elimu katika shule watakazopenda na kuwaruhusu machaguzi

Kamati pia imeipa Tanzania kuchukua hatua hizo ndani ya siku 180 tangu kutoka kwa hukumu hiyo na kuhakikisha Tanzania inawasilisha taarifa ya utekelezaji wa hukumu hii katika Kamati.

Ushindi huu ni muhimu sana kwa ajili ya wasichana wa Tanzania na tunaamini serikali ya Tanzania itazingatia na kutekeleza yaliyoamriwa kwenye hukumu hii ili haki za wasichana ziweze kusimamiwa ipasavyo
 
Mpo sahihi kwa future ya watoto wa kike na hongereni, ila kwa hawa wasichana wa leo akipata mimba yeye mwenyewe hakubali kurudi shule
 
Kwa hiyo wanafunzi wasiwe wanapima mimba shuleni?
Hizi shule zitakuwa shule au vituo vya wazazi!!!
Tuachane na kufuatilia wanaonyandua wanafunzi hata wanaowapa mimba tuachane nao.
 
"Yaani Mtu akapate mimba halafu arudishwe shuleni? Yaani tuwasomeshe wazazi? Hili kamwe halitawezekana kipindi Cha utawara wangu"

Maneno ya Kiongozi mmoja toka bara la Giza.
 
Back
Top Bottom