Search results

  1. Yoda

    Kisukari ni tatizo kubwa zaidi kwa Waarabu na watu wa visiwani!

    Katika nchi 15 zenye asilimia kubwa zaidi ya wagonjwa wa kisukari duniani nchi 5 ambazo ni Kuwait, Misri, Qatar, Saudi Arabia na Sudan ni za kiarabu. Nchi moja ya Pakistan ina ustaarabu unaokaribiana na Waarabu nchi nyingine 10 zilizobaki katika listi hiyo ni visiwa vidogo vidogo. Inasemekana...
  2. Yoda

    Profesa Janabi kama Dr. Fauci wa Marekani

    Dr. Anthony Fauci alikuwa ni Mkurugenzi wa taasisi ya kitaifa ya Marekani ya magonjwa ya mzio na kuambukiza(NIAID) kwa takribani miaka 20 na jina kubwa katika masuala ya Afya Marekani kama alivyo Janabi hapa Tanzania. Wakati wa mlipuko wa COVID anakumbukwa zaidi kwa jinsi alivyokuwa akitoa...
  3. Yoda

    Utafiti wa Mwananchi ni matokeo ya ombwe la utafiti halisi wa maoni ya wananchi

    Kabla ya utawala wa awamu ya tano kuingia madarakani kulikuwa na taasisi binafsi za utafiti zilizokuwa zinafanya utafiti wa masula ya kijamii kwa raia na kutoa matoke ya hapa na pale. Waliokuwa wanafuatilia watazikumbuka Twaweza, IPSOS, Afrobarometer na REDET. Japo matokeo ya utafiti wa taasisi...
  4. Yoda

    Tunaweza kuwa na Muungano wa Serikali mbili na nusu pia, sio lazima kufikiria ni moja, mbili au tatu tu

    Kila mara kunapozuka mjadala kuhusu muungano wetu mara zote watu hubishania kati ya serikali mbili au tatu, kuna kundi dogo pia ambalo huwazia na kuibua hoja za serikali moja kabisa. Je tunaweza kujiongeza kufikiria nje ya mawazo haya? Mfano uwepo wa serikali mbili na nusu. Katika mfumo huu...
  5. Yoda

    Waziri Jerry Silaa, kwanini hushughuliki na maafisa ardhi? Jifunze kutoka Libya ya Gaddafi pia

    Katika muendelezo wa kile waziri wa ardhi Jerry Silaa anachokiita kliniki ya ardhi na kutatatua changamoto za ardhi ameendelea kupuuza kabisa documents/nyaraka halali za serikali na mahakama za wale wanaodaiwa kuwa ni wavamazi au wanunuzi matapeli waliojimilikisha ardhi za watu wengine. Yani mtu...
  6. Yoda

    Budapest Memorandum: Ulaghai wa kihistoria Warusi waliowafanyia Marekani, Uingereza na Ukraine

    Mwaka 1991 wakati USSR inavunjika mataifa kadhaa yaliyokuwa yanaunda umoja huo yalikuwa yanamiliki silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu. Ukraine lilikuwa ni taifa mojawapo lililokuwa likimiliki mzigo mkubwa wa silaha za nyuklia na nyinginezo nzito, ilikuwa taifa la tatu duniani kwa...
  7. Yoda

    Kigwangala, kumsifia Rais sio uzalendo wa kwanza, nchi yetu ni Jamuhuri sio Ufalme

    Maneno ya Mbunge Kigwangala kwamba kumsifia Rais ni uzalendo wa kwanza ni maneno ya kusikitisha yanayatuonyesha ni watu wa ajabu jinsi gani wanaotungoza wakati mwingine. Huyu ni mtu aliyekuwa waziri kamili na kutaka pia kuwa Rais wa taifa hili lakini hata huelewei kwamba nchi yake ni Jamuhuri na...
  8. Yoda

    Bunge la Marekani laidhinisha kitita cha $ billion 60 kwa Ukraine

    Baada ya mkwamo wa muda mrefu uliochangiwa na baadhi ya wabunge wa Marekani wenye mahaba na Putin hatimaye bunge la Marekani limepitisha kifurushi kipya cha $billion 60 kwa vita vya Ukraine. Msaada huu mpya kwa Ukraine unajiri baada ya mwaka mmoja na nusu tangu bunge lililokuwa likiongozwa na...
  9. Yoda

    Mpina ataka viongozi wa wizara, mashirika, mikoa na wilaya kupatikana kwa usahili!

    Akichangia bungeni leo mbunge machachari wa CCM anasema umefika wakati sasa viongozi kama mawaziri, wakurugenzi, makatibu wakuu,wakuu wa mikoa na wilaya wapatikane kwa kuomba nafasi hizo na kufanyiwa usahili. Anasema mfumo wa sasa hauna uwazi kwani Rai hawezi kusoma CV za watu wote wanofaa...
  10. Yoda

    Namna ya shambulizi la Israel huko Isfahan-Iran inathibitisha Israel wamedhamiria na wanawaalika Iran kwa vita kamili.

    Tukio la Jana la Israel kushambulia kwa ndege nchini Iran kujibu shambulizi la drones la Iran lililotangulia ni la kiwango cha juu kuashiria vita kamili . Hili Shambulizi lilipangwa kwa mkakati kama vile jeshi lililoko vitani serious na sio kama michezo ya kidali poo anayojaribu kufanya Iran...
  11. Yoda

    Jinsi Iran ilivyojipata chini ya utawala wa Ki-Ayatollah

    Kabla ya Iran kutawaliwa katika mfumo wake wa sasa wa Ki- Ayatollah ilikuwa ikitawaliwa kwa mfumo aina fulani karibia na Ufalme hivi ambao watawala wake walikuwa wakiitwa Shah. Mashah wawili wa mwisho, baba na mtoto wake walitokana na mapinduzi ya ufalme halisi wa muda mrefu wa Qajar mwaka 1925...
  12. Yoda

    Watanzania ndiyo raia waungawana zaidi Africa Mashariki?

    Huwa kuna kauli zinasemwa au zinaandikwa kwamba "...arudi kwao Rwanda au Burundi", "huyo atakuwa Mtusi", "Watanzania hatuko hivyo" n.k Kwa nini inadhaniwa watu wa Rwanda na Burundi kuwa wana roho mbaya sana kuliko Watanzania? Nini kinatufanya au kinaashira tuamini kwamba sisi ni watu...
  13. Yoda

    Lusinde, hoja yako nzuri ya kuzingatia matokeo ya sensa isiwe kwa miradi tu, bali hadi kugawa majimbo

    Akichangia katika bunge la JMT Mbunge wa Mtera Lusinde ameitaka serikali izingatie matokeo ya sensa katika ugawanywaji wa huduma za kijamii kama shule, hospitali na barabara, anasema huduma hizo lazima ziwe na uwiano na idadi ya watu katika eneo husika. Ameshangaa kuna maeneo yenye watu wengi...
  14. Yoda

    Samaki, nyama, kuku na maharage kuliwa kama mboga ni dalilli ya umaskini?

    Kwenye hoteli kubwa zote, na nyingi za kati menu ya chakula kikuu huwa ni samaki, kuku, nyama ya ng'ombe, mbuzi kitimoto na nyinginezo halafu ndio unachagua utakula na nini ikiwa ni ugali, wali, viazi n.k Kwenye hizi hoteli bei ya chakula inapimwa kwa samaki, kuku na nyama kisha (wanga) ambao...
  15. Yoda

    Kwanini Mashariki ya Kati ni eneo korofi lisilopata utulivu watu wanaishi ngumi mkononi?

    Eneo la Mashariki ya kati ni kama eneo lenye laana fulani hivi ya vurugu. Tangu nimeanza kupata akili za kufuatilia habari sijawahi kusikiliza taarifa ya habari katika redio au TV bila kusikia kuna watu Mashariki ya wakati wamezinguana. Yani huwa hakuna kutulia, ukiachilia mbali mgogoro wa...
  16. Yoda

    Uwezekano wa Vita Vikuu vya Tatu (WW III) vya Dunia ni mdogo sana

    Pamoja na purukushani zinazoendelea sehemu mbalimbali za dunia za kuchokozana, kuvamiana na kubutuana siku za hivi karibuni uwezekano wa kutokea vita vikuu vya tatu vya dunia bado ni mdogo sana. Kwanza tukumbuke katika vita vya kwanza na vya pili vya dunia ambavyo chanzo chake kilikuwa ni ulaya...
  17. Yoda

    Iran kazabuliwa kofi la uso yeye karudisha kwa kumsukuma tu Israel

    Kinachoitwa shambulizi la Iran kwa Israel jana ni kelele kubwa tu za majidai na usumbufu ambazo hazikuleta chochote cha maana. Unashambulia nchi iliyo umbali wa KM 2300 kwa kutuma drones ambazo zinakatiza anga za nchi nyingine kadhaa kwa masaa na karibia zote kuishia kutunguliwa au kuanguka...
  18. Yoda

    Sherehe ya kumbukumbu ya kifo cha Sokoine ilikuwa ya kiserikali au familia?

    Serikali ina bajeti iloyotengwa ya kufanya sherehe za kumbukumbu za vifo kwa viongozi wa taifa waliofariki ? Ni viongozi gani waliofariki ambao wanakidhi vigezo vya kufanyiwa kumbukumbu za kiserikali kwa bajeti ya serikali? Wizara gani inasimamia ufanyikaji wa hizo kumbukumbu?
  19. Yoda

    Tusiendekeze nyadhifa(titles) za kifamilia katika siasa na uongozi wa umma

    Kuitana "mama yangu", "baba yangu", "mdogo wangu", "kaka yangu", "dada yangu", "shangazi yangu", "shemeji yangu" na vyeo vingine kama hivyo katika shughuli za siasa na umma ni utamaduni mpya uliovuka mipaka, kushika kasi na sasa unaanza kukomaa. Zamani vyeo vya kifamilia ambavyo nilikuwa...
  20. Yoda

    Kuhemea, Kujumua na Kuingiliwa ni misamiati sahihi ya Kiswahili?

    Wataalamu wa Kiswahili, haya ni maneno au misamiati sahihi ya lugha ya Kiswahili? " Kujumua" kwa maana ya kununua vitu kwa jumla. Huu msamiati unatumika sana Iringa, Njombe na Mbeya. "Kuingiliwa" kwa maana ya kupunjwa pesa unayostahili au kulipa pesa zaidi ya unavyostahili. Huu msamiati...
Back
Top Bottom