lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,168
- 33,420
Jamani ni mimi peke yangu ndio naona hivyo?
Mikutano ya Lissu tofauti na mikutano ya Magufuli. Watu kwenye mikutano ya Lissu huenda kumpokea mgombea huyo kwa sherehe, shangwa, nderemo na fifijo.
Hakuna wasanii wengi na sijui wana wimbo mmoja tu,"Tundu Lisu wapeleke, mchakamchaka. Tundu Lisu wapeleke kikamada" wimbo huu mmoja tu watu wanaurudi hatari, wanapagawa hatari, wanasisimuka hatari, wanaserebuka hatari.
Sijui wimbo huo umerekodiwa au kuna mtu huwa anauimba lakini Furaha iliyopo huko CCM na wasanii wa nchi nzima na wa nje ya nchi hakuna. Watu wa CCM hata wakifurahi ni kama wanawafurahia wasanii tu, hata hao ni wanawashangaa tu.
Nasikia kuna sehemu umeme ulikatika, ilikuwa jioni sana, makutano wakaamua kumsindikiza Lissu hadi mahala salama, hebu fikiria umati ule unaingia Mjini wakimsindikiza mgombea wao, ni upendo ulioje.
Nasikia sehemu fulani watu walikua wakicheza Reggae, wimbo maarufu wa Bob Marley, One Love. waliucheza wimbo huu pamoja na Lissu, ni furaha iliyoje?
Kuna ujumbe mkubwa sana kwenye mikutano ya Lissu. Lissu katengwa na kila huduma anazostahili kama kuoneshwa na TV au Redio au Magazeti ya Taifa, lakini anafarijiwa na wanyonge wenzie, tena furaha halisi itokayo ndani ya nyumba vya mioyo ya wapigakura wake.
Furaha, upendo na hamasa waliyonayo watu wa Lissu sio ya kulazimisha, ni furaha halisi.
Nakumbuka ni hawahawa walimchangia alipopigwa,walimsalia apone, walisoma al badir ili watesi wake wapate adhabu ya Mungu, waliwachangia Viongozi wa Chadema walipowekwa ndani, walimchangia damu, walijitokeza kwa wingi kwenda Uwanja wa ndege kumpokea bila kujali vitisho vya Polisi na sasa wanaojitokeza kwa wingi kwenye mikutano yake ambayo imegekua kuwa Shule ya Uraia.
Ni upendo, furaha na elimu.
Chagua Rais Lissu, chagua mbunge Chadema, chagua diwani Chadema.
Wagombea wa CCM wote huwa wanaunga mkono hoja ambazo leo ndio mwiba mchungu kwa Watanzania, na safari hii wanaenda kuunga mkono hoja ya kuondoa ukomo wa Rais kukaa madarakani.
Fikiria mateso ya miaka hi mitano, itakuaje kama Rais akibaki bila kikomo.