Mapendekezo ya CHADEMA juu ya Miswada ya Sheria za Uchaguzi ambayo Kamati ya Bunge inazuia yasisomwe Bungeni

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mapendekezo ya jumla na msimamo wa CHADEMA juu ya miswada ya sheria iliyowasilishwa bungeni 10, Novemba 2023 inayohusu masuala ya uchaguzi na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa

NB; maoni haya ndiyo ambayo kamati ya kudumu ya bunge ya utawala, katiba na sheria inazuia yasisomwe

=====

MAPENDEKEZO YA JUMLA NA MSIMAMO WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA

MAENDELEO (CHADEMA) JUU YA MISWADA YA SHERIA ILIYOWASILISHWA

BUNGENI TAREHE 10, NOVEMBA 2023 INAYOHUSU MASUALA YA UCHAGUZI NA

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

______________________________________



Miswada iliyowasilishwa Bungeni tarehe 10 Novemba, 2023 iondolewe Bungeni kwa sababu miswada hiyo haijajibu matatizo ya msingi ya muundo wa Tume wala Sheria za uchaguzi, hivyo basi, tunapendekeza na tunataka yafanyike mambo yafuatayo;

Serikali iwasilishe muswada Bungeni wa kukwamua mchakato wa Katiba Mpya pamoja na mwelekeo (Road Map) wa kila hatua mpaka ipatikane Katiba Mpya itakayopatikana kwa kuzingatia muafaka wa Kitaifa.

Serikali iwasilishe Bungeni muswada wa kufanya marekebisho ya mpito (minimum Reforms) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) ya mwaka 1977 ili kuwezesha kufanyika uchaguzi huru na haki baada ya kuondoa mapungufu ya kikatiba yaliyopo sasa kwa sababu Sheria zinatungwa kwa mujibu wa Katiba ambayo kwa sasa ina mapungufu mengi ambayo yanaathiri Sheria zinazoenda kutungwa.

Kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa; Serikali iwasilishe Bungeni muswada ambapo pamoja na mambo mengine ya uchaguzi huo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipewe mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa na sio kusimamiwa na Ofisi ya Raise Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa Kanuni ambazo zinatungwa na Waziri wa Nchi anayehusika na TAMISEMI.

Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya siasa (Sheria ⁠ ya Vyama vya Siasa kama ilivyorekebishwa mwaka 2019 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi) uondolewe kwa sababu haitatui changamoto zilizopo sasa na badala yake muswada wa sasa unampa mamlaka zaidi Msajili wa Vyama vya Siasa ambapo Vyama vitabanwa zaidi na Ofisi ya Msajili ambayo haipo huru kwa mujibu wa Katiba. Aidha muswada haujazingatia na umepuuza amri ya Mahakama ya Afrika Mashariki ambapo baadhi ya vifungu iliamriwa kwamba vinakiuka Mkataba wa Afrika ya Mashariki.

Miswada iliyowasilishwa Bungeni tarehe 10 Novemba, 2023 ⁠ iondolewe na kuandikwa upya kwa mujibu wa marekebisho ya mpito ya Katiba ya JMT ya mwaka 1977 yatakayofanyika kama ilivyopendekezwa hapo awali katika aya ya pili.

Pamoja na msimamo huu na maoni ya jumla; mapendekezo yetu yamegawanyika katika sura tatu;

Sura ya Kwanza ni uchambuzi na mapendekezo ya marekebisho ya mpito ya Katiba ya JMT ya mwaka 1977 pamoja na uchambuzi na mapendekezo kuhusu Muswada wa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Sura ya Pili ni uchambuzi na mapendekezo kuhusu Muswada wa Muundo wa Tume ya Uchaguzi.

Sura ya Tatu ni uchambuzi na mapendekezo kuhusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi pamoja Sheria ya Vyama vya Siasa Toleo la mwaka 2019.

SURA YA KWANZA​

HOJA ZA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU NAMNA YA KUBORESHA MFUMO WA UCHAGUZI KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WA MWAKA 2024 NA UCHAGUZI MKUU WA RAIS WABUNGE NA MADIWANI WA MWAKA 2025

_____________________________

Sehemu A: Utangulizi​

Ni miaka 30 na zaidi toka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliporudisha mfumo wa demokrasia ya Vyama vingi vya siasa. Kwa miaka kadhaa kumekuwa na mapendekezo yanayojirudia kila baada ya uchaguzi mkuu na hata uchaguzi wa serikali za mitaa kuhusu haja ya kuufanyia marekebisho mfumo wa uchaguzi nchini. Rai hiyo imetolewa mara kadhaa na vyama vya siasa, asasi za kiraia, mashirika ya kimataifa pamoja waangalizi wa chaguzi mbalimbali nchini.

Hoja kuu kuhusu haja ya kuufanyia marekebisho mfumo wa uchaguzi nchini umejikita katika msingi kwamba ili tuwe na marekebisho yenye tija ya mfumo wa uchaguzi ni muhimu na ni lazima msingi wake uanze kwanza kuifanyia maboresho Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la 2005 ambayo ndio ina hoja za msingi (Primary Contradictions) kuhusu maboresho ya mfumo wa uchaguzi.

Baada ya kuifanyia marekebisho Katiba ya Jamhuri ya Muungano hapo ndipo yafanyike maboresho ya sheria mbalimbali zinazohusu uchaguzi ili kuendana na Katiba iliyoboreshwa.

Sehemu B: Hoja na Maeneo mbalimbali yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977​

Kuna maeneo kadhaa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuboresha mfumo wa uchaguzi kama ifuatavyo;

Hoja Na 1: Haja ya uwepo wa Mgombea Huru Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kuifanyia marekebisho ibara ya 39(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (itafahamika kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano) ili kuondoa ulazima wa Mtu kuwa mwanachama wa Chama cha siasa ndipo awe na sifa za kugombea nafasi ya Urais wa Jumhuri ya Muungano.

Mapendekezo ya Chadema:

Katiba ya Jamhuri ya Muungano iruhusu uwepo wa Mgombea huru kwenye ngazi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama Mgombea wa nafasi ya Urais alikuwa mwanachama wa chama, awe amejitoa uanachama angalau mwaka mmoja kabla ya Tarehe ya Uchaguzi ili akidhi sifa na vigezo vya kuwa Rais

Hoja Na 2: Kuhusu Mgombea wa Urais kutangazwa Mshindi baada ya kupata kura nyingi (Simple Majority) kushinda Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kuna haja ya kufanyia marekebishi Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ili kuondoa sharti la Mgombea wa kiti cha Urais kutangazwa mshindi baada ya kupata kura nyingi (simple majority) na kuweka utaratibu mwingine.

Mapendekezo ya Chadema:

Mgombea atatangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iwapo tu atafikisha angalau 50% ya kura + Kura 1 ya kura halali zilizopigwa wakati wa uchaguzi.

Kukiwa hakuna aliyepata idadi hizo za kura, uchaguzi utarudiwa mara ya pili (re-run) ndani ya miezi miwili.

Wagombea wawili wenye wingi wa kura ndio watahusika kwenye marudio ya uchaguzi.

Hoja Na. 3: Matokeo ya Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kuhojiwa Mahakamani
Kuifanyia marekebisho Ibara ya 41(7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ili kuweka utaratibu wa namna ya kuhoji matokeo ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kwa sasa Ibara hiyo inakataza matokeo ya Urais kuhojiwa Mahakamani.

Mapendekezo ya Chadema:

Mgombea au mpiga kura au wapiga kura, watakuwa na haki ya kuhoji matokeo ya nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mahakama ya Rufani.

Maombi hayo yataletwa ndani ya siku saba (7) tangu kutangazwa kwa matokeo ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Shauri litasikilizwa na Majaji wa Mahakama ya Rufani wasiopungua Saba wakiongozwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuamuliwa ndani ya siku 14 tangu shauri au mashauri kuletwa.

Ikiwa Mahakama ya Rufani itajiridhisha na kutoa uamuzi kufuta matokeo ya Uchaguzi wa nafasi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Uchaguzi mpya utaitishwa ndani ya siku 60 tangu tarehe ya kutolewa kwa hukumu ya Mahakama.

Hoja Na. 4: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua Madaraka
Utaratibu wa sasa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Ibara ya 42 ni kwamba Rais atashika madaraka mapema baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa na si zaidi ya siku saba baada ya kutangazwa.

Mapendekezo ya Chadema:

Rais Mteule na Makamu wa Rais Mteule, watakula kiapo na kupokea madaraka ya kuendesha serikali ndani ya siku 14 tangu kutangazwa kwa matokeo.

Ikiwa kuna shauri Mahakamani la kupinga kuchaguliwa kwao, Rais Mteule na Makamu wa Rais Mteule watakula kiapo na kupokea madaraka ya kuendesha Serikali ndani ya siku 14 iwapo mahakama haitakuwa imetengua matokeo ya Urais.

Bunge litatunga sheria ya makabidhiano ya madaraka ya Urais ili kuweka utaratibu kamili wa makabidhiano ya madaraka kutoka awamu moja kwenda nyingine au kutoka Chama kimoja kwenda Chama kingine cha Siasa.

Hoja Na. 5: Aina za Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Kuna aina kadhaa za Wabunge kwa mujibu wa Ibara ya 66(1)(a) na (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambapo ni kama ifuatavyo; Wabunge wa Majimbo, Wabunge wa Viti Maalum, Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwao, Mwanasheria Mkuu, Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Raise na Spika ikiwa hatachaguliwa miongoni mwa Wabunge. Tunapendekeza Ibara hiyo ifanyiwe marekebisho kwa kuzingatia yafuatayo;

Mapendekezo ya Chadema:

Kuwe na wabunge wawili wa kuchaguliwa kwa kila Jimbo la uchaguzi, moja Mwanaume na Mmoja mwanamke ambao kila mmoja atachaguliwa kwa kura zake kwenye kundi analogombea.

Kuwe na Wabunge watakanao na orodha itakayowasilishwa na Vyama vya Siasa ambao watachaguliwa kwa uwiano wa kura zote za Ubunge ambao Chama Kitapata.

Wabunge watokanao na orodha za Vyama vya Siasa hawatapungua 30% ya wabunge wote bungeni.

Hoja Na 6: Mgombea Binafsi wa nafasi ya Ubunge
Kufanyia marekebisho ya sifa za Mgombea wa Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 67(1)ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ili kuzingatia yafuatayo; Mapendekezo ya Chadema:

Kutakuwa na Mgombea Binafsi kwa nafasi ya Ubunge.

Awe hajawa mwanachama wa chama chochote cha siasa angalau miezi sita kabla ya tarehe ya Uchaguzi.

Akidhi sifa na vigezo vya kuwa Mbunge kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Uchaguzi.

Hoja Na. 7: Kutengua uteuzi wa Wagombea
Kuifanyia marekebisho Ibara ya 67(14) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ili kuondoa tabia ya kuengua kiholela Wagombea wa nafasi ya Ubunge, na kuweka masharti yafuatayo;

Mapendekezo ya Chadema:

Mgombea ataenguliwa iwapo tu amekosa sifa na vigezo kama vilivyoanishwa kwenye Katiba hii.

Mgombea ambae hajatimiza masharti yanayotokana na sheria nyingine, atapewa fursa ya kurekebisha au kukamilisha matakwa ya sheria husika.

Mgombea ambae hataweza kufanya marekebisho au kukidhi matakwa ya sheria husika baada ya kupewa muda wa kutosha basi atakuwa amejiondoa mwenyewe katika mchakato wa uchaguzi.

Hoja Na 8: Muundo wa Tume Huru ya Uchaguzi
Kurekebisha Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuhusu Muundo wa Tume ya uchaguzi;

Mapendekezo ya Chadema:

Kutakuwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi

Kutakuwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi

Kutakuwa na wawakilishi wanne (4) wa Vyama vya Siasa, Mwakilishi mmoja (1) atakaeteuliwa na chama husika kwa kila chama, kutoka kwenye vyama Vinne vyenye wabunge wengi bungeni.

Kutakuwa na wawakilishi wawili kutoka kwenye mashirika ya dini.

Kutakuwa na mwakilishi mmoja(1) kutoka kwenye asasi za kiraia.

Uteuzi wa wajumbe utazingatia pande mbili za Jamuhuri ya Muungano na jinsia.

Hoja Na 9: Kamati ya Usaili na Uteuzi wa Tume ya Uchaguzi
Ibara ya 74(2)(3) na(4) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ifanyiwe marekebisho ili kukidhi yafuatayo;

Mapendekezo ya Chadema:

Kamishna wa Tume ya Maadili ya viongozi Umma wa Jamuhuri ya Muungano.

Kamishna wa Tume ya Maadili ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Mwakilishi mmoja kutoka Tume ya Utumishi wa Umma Jamuhuri ya Muungano.

Mwakilishi mmoja kutoka Tume ya Utumishi wa Umma SMZ

Wawakilishi wawili kutoka Asasi za Kiraia

Wawakilishi wawili kutoka Vyama viwili vyenye wabunge wengi bungeni

Wawakilishi watatu kutoka kwenye Taasisi za dini

Hoja Na. 10: Kufuta Ibara ya 74(3)(d)
Ibara ya 74(3)(d) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano inatoa masharti kuhusu watu ambao hawataweza kuteuliwa Wajumbe wa Tume.

Mapendekezo ya Chadema:

Kufuta kifungu husika ili kuruhusu wajumbe kutoka vyama vya siasa kuwa sehemu ya wajumbe wa Tume ya Uchaguzi.

Aidha Mjumbe anaetokana na Chama cha Siasa atakoma kuwa Mjumbe wa tume ya Uchaguzi ikiwa atapoteza sifa za kuwa Mwanachama au kuhama chama Chake na Chama husika kitataarifiwa ili kupendekeza Jina la Mjumbe Mwingine ili atauliwe kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.

Hoja Na. 11: Kuondoa Mamlaka ya Rais kuondoa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi
Kuifanyia marekebisho Ibara ya 74(5) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano na kuweka masharti yafuatayo;

Mapendekezo ya Chadema:

Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Mjumbe yeyote Mwingine wa Tume ataondolewa iwapo atapoteza sifa zilizowekwa kwenye Katiba hii.

Kwaajili ya kutekeleza hatua hii, ukiacha suala la mhusika kufariki au kujiuzulu, shauri litapelekwa Mahakama Kuu ili kudhibitisha kuwa Mjumbe husika amepoteza Sifa za kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hoja Na 12: Kuiongezea Tume ya Uchaguzi Mamlaka Kusimamia shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Kura za Maoni

Ibara ya 74(6) ya Katiba ya Jamuhuri Ya Muungano ifanyiwe marekebisho ili kuipa Tume jukumu la kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Kura ya maoni ya Katiba.

Mapendekezo ya Chadema:

Tume itakuwa na mamlaka ya kuandikisha wapiga kura na kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kama itavyoanishwa kwenye sheria itakayotungwa na Bunge.

Tume itakuwa na mamlaka ya Kuendesha Kura ya Maoni kama itavyoainishwa kwenye sheria itakayotungwa na Bunge.

Hoja Na. 13: Muundo wa kiutendaji wa Tume ya taifa ya Uchaguzi
Kuifanyia marekebisho Ibara ya 74(7) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ili kuboresha muundo wa kiutendaji wa Tume.

Mapendekezo ya Chadema:

Tume ya Uchaguzi itakuwa chombo huru na itakuwa na mamlaka ya kuajiri Mkurugenzi wa Uchaguzi na watendaji wote wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi angalau mpaka Ngazi ya Kata.

Serikali itatunga Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya utekelezaji wa Mamlaka na kazi za Tume ya Taifa ya uchaguzi

Hoja Na 14: Bunge kutunga sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.
Kuifanyia marekebisho Ibara ya 74(8) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ili kukidhi yafuatayo;

Mapendekezo ya Chadema:

(i) Kuongeza Ibara ndogo mara baada ya Ibara ya 74(8) ili kulipa Bunge la Jamhuri ya Muungano mamlaka ya kutunga sheria kuhusu majukumu na mamlaka ya Tume kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Mamlaka za Miji Midogo.

Hoja Na. 15: Mamlaka ya Tume Kukasimu mamlaka yake
Kufuta mamlaka ya Tume chini ya Ibara ya 74(10) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano kukasimu madaraka yake.

Mapendekezo ya Chadema:

(i) Kufuta kabisa kipengele hiki ili tume ijitosheleze kiutendaji bila kutegemea wala kutumia muundo wa Serikali za Mitaa kusimamia chaguzi.

Hoja Na. 16: Kuondoa Sharti la Uamuzi wa Tume ya Uchaguzi kutohojiwa Mahakamani
Ibara ya 74(12) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ifanyiwe marekebisho kama ifuatavyo;

Mapendekezo ya Chadema:

Tume ya Taifa ya Uchaguzi itaweza kuhojiwa matendo na/au maamuzi yake mahakamani kwa kila hatua ya mzunguko wa Uchaguzi.

Bunge litatunga sheria itakayoweka utaratibu mzuri na wa haraka wa kuwezesha hili kutekelezwa kwa kila hatua ya mzunguko wa uchaguzi.

Hoja Na. 17: Wanaohusika na Uchaguzi kutojuinga na Chama cha Siasa
Ibara ya 74(14) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ifanyiwe marekebisho yafuatayo;

Mapendekezo ya Chadema:

(i) Kuweka upekee (Exception) kwa wajumbe wa Tume ya uchaguzi wanaotokana na Vyama vya Siasa kwa kuzingatia mapendekezo ya awali.

Hoja Na. 18: Wanaohusika na Uchaguzi
Ibara ya 74(15) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano irekebishwe; Mapendekezo ya Chadema:

(i) Wanaohusika na Uchaguzi watakuwa Wajumbe ya Taifa ya Uchaguzi na Watumishi wote wa Tume mpaka ngazi za Kata.

Hoja Na. 19: Mamlaka ya Tume ya Uchaguzi Kuamua Kugawa Mipaka ya majimbo ya Uchaguzi
Ibara ya 75(1) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano irekebishwe;

Mapendekezo ya Chadema:

Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakuwa na Mamalaka Kamili ya Kuamua kama kuna haja ya kugawa majimbo ya uchaguzi.

Hii inaondoa haja ya kuomba kibali kwa Rais ili kuanza mchakato.

Hoja Na. 20: Mamlaka ya Tume ya Uchaguzi Kugawa Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi
Ibara ya 75(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano irekebishwe kukidhi yafuatayo; Mapendekezo ya Chadema:

Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakuwa na mamlaka kamili ya kugawa majimbo ya uchaguzi kwa kuzingatia vigezo vilivyo kwenye Katiba hii na sheria nyingine itakayotungwa na Bunge.

Hii inaondoa mamlaka ya Rais kuwa mwamuzi wa mwisho wa idadi na mipaka ya majimbo.

Hoja Na. 21: Vigezo vya Kugawa Mipaka ya majimbo ya Uchaguzi.
Ibara ya 75(3) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ifanyiwe marekebisho kama ifuatavyo;

Mapendekezo ya Chadema:

Tume ya Taifa ya Uchaguzi itazingatia idadi ya watu kama kigezo kikuu cha kuamua mipaka ya majimbo, mifumo ya mawasiliano na hali ya kijiografia yatazingatiwa kwenye kugawa majimbo ya uchaguzi.

Mwanzo kigezo hiki cha idadi ya watu kilikuwa kimefutwa kwenye Katiba ya 1977.

Hoja Na. 22: Mgawanyo wa Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi Kuhojiwa Mahakamani.
Ibara ya 75(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano irekebishwe ili kukidhi yafuatayo;

Mapendekezo ya Chadema:

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaweza kuhojiwa mahakamani na Raia yeyote mwenye maslahi na uchaguzi Katika Jamhuri ya Muungano.

Bunge litatunga Sheria ili kuweka utaratibu wa namna ya kuhoji namna Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilivyogawa majimbo ya uchaguzi na kwa vyovyote vile mashauri haya yatawasilishwa na kutolewa uamuzi kabla ya muda wa kutoa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali la uchaguzi husika.

Hoja No 23: Mchakato wa Kuchagua Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ibara ya 77 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ifanyiwe marekebisho ili kuboresha mchakato wa kuwachagua Wabunge.

Mapendekezo ya Chadema:

Watachaguliwa Wabunge wawili tu kwa kila jimbo la uchaguzi, mmoja mwanaume na mmoja mwanamke kutokana na kura za ila mmoja kwenye kundi lake.

Kwenye nafasi ambapo mgombea ni mmoja tu, atapigiwa kura ya ndio na Hapana na lazima apate kura za ndio angala 50% + kura 1 ili atangazwe kushinda.

Kila Chama cha siasa kitaruhusiwa kusimamisha wagombea wawili(2) tu kwa kila jimbo la uchaguzi mmoja (1) kwa nafasi wa Mbunge wa jimbo Mwanaume na Mgombea mmoja tu kwa nafasi ya mbunge wa Jimbo mwanamke, na wagombea binafsi watagombea kama itakavyoelekezwa kwenye sheria itakayotungwa na Bunge.

Majina ya Wagombea wote yatawasilishwa kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama itakavyoanishwa kwenye sheria iliyotungwa na Bunge.

Hoja Na. 24: Uchaguzi wa Wabunge wanaotokana na orodha za Vyama
Ibara ya 78 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ifanyiwe marekebisho kukidhi yafuatayo;

Mapendekezo ya Chadema:

Wabunge watokanao na Chama cha siasa watachaguliwa kwa uwiano wa kura za ubunge ambazo Chama kitakazopata kwa wagombea ubunge wake nchi nzima.

Majina ya wabunge kwenye orodha ya chama yatafuata namna yalivyopangwa wakati yanawasilishwa na chama husika (asending order).

Orodha hii, kwa mashauriano na chama husika ndio itatumika kujaza nafasi wazi itakayoacha na mbunge anayetokana na orodha ya chama husika aliyekosa sifa au kifariki.

Hoja Na. 25: Chombo cha kuhoji Uchaguzi wa Rais

Kuweka Ibara mpya ya 117A ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano kama ifuatavyo;

Mapendekezo ya Chadema:

Mahakama ya Rufani ndio itakuwa na mamlaka ya mwanzo ya kusikiliza na kuamua mashauri kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais.

Kwan ajili ya kusikiliza mashauri haya, Mahakama itaongozwa na Jaji Mkuu akiwa Pamoja na Majaji wengine sita(6) wa Mahakama ya Rufani.

Mahakama ya Rufani itajiwekea utaratibu wake wa kupokea, kusikiliza na kuaua mashauri kwa Kanuni zitakazotungwa na Jaji Mkuu.

Bunge linaweza kutunga sheria itakayowezesha utekelezaji wa kazi hii mahususi ya Makahama ya Rufani

Sehemu C: Uchambuzi wa Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Wa Mwaka 2023

Kifungu cha 4 hakijaweka masharti kwamba Kanuni na Miongozo inayotolewa na Tume kuchapwa kwenye Gazeti la Serikali.

Kifungu cha 5 hakijaweza kuondoa changamoto ya uundwaji wa Majimbo ya uchaguzi kwa kutumia kigezo cha uwiano wa idadi ya watu (population quota).

Bado hakuna fursa ya kuhoji maamuzi ya Tume kwenye mgawanyo wa Majimbo Mahakamani hata kama kuna mapungufu au kutokuridhika na mgawanyo uliofanywa na Tume.

Kwa kifungu kilivyo bado tatizo la kuundwa kwa majimbo ya uchaguzi kwa upendeleo au sababu za kisiasa kupendelea Chama kilichopo madaralani halijapata suluhisho (Gerrymandering)

Bado mamlaka ya mwisho ya kuidhinisha mipaka na mgawanyo wa majimbo ya Uchaguzi yameachwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa CCM ambaye anaweza kuwa Mgombea wa nafasi ya Urais.

Kifungu cha 6(1)- Muswada unawarudisha Wakurugenzi ambao ni wateule wa Rais, waliopo chini ya Waziri wa TAMISEMI kuwa wasimamizi wa uchaguzi ambapo Wasimamizi hao wanaweza kupokea maelekezo ya Rais, Waziri wa TAMISEMI na Tume ya Uchaguzi. Hakuna maelezo kwamba ni maelekezo gani yatatamalaki ikiwa maelekezo hayo yanakinzana.

Kifungu cha 6(3) kinafanya kifungu cha 6(2) kutokuwa na maana na kwa hiyo 6(2) ifutwe.

Kifungu cha 6(1) na 6(2) vifutwe ili kuruhusu kifungu cha 6(3) kuwa kifungu mama (main provision) kuhusu uteuzi wa Wasimamizi wa uchaguzi. Tunapendekeza kwamba Time iwe na mamlaka ya kuteua na kichapisha kwenye Gazeti la Serikali Wasimamizi wa uchaguzi bila kulazimisha Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa Wasimamizi wa uchaguzi. Pendekezo hili litaipa Tume mamlaka kamili ya kutoa maelekezo kwa Wasimamizi iliowateua yenyewe.

Kifungu cha 7(3) kiwe kifungu mama na kifungu cha 7(1) na 7(2) vifutwe ili kuwaondoa Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa Maafisa Waandikishaji wa Wapiga Kura.

Kiongezwe kifungu kidogo kitakacholazimu Mratibu wa uchaguzi wa Mkoa kuapa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi na kutoa tamko la kujitoa au kutokuwa Mwanachama wa Chama cha siasa.

Kiongezwe kifungu kidogo kingine kinachoipa Tume kiteua Mratibu wa uchaguzi wa Mkoa kuliko kulazimisha kutumia Makatibu Tawala wa Mikoa.

Kuwe na kifungu kidogo kitakachotoa masharti kwa Tume kuchapisha orodha ya majina na namba zao za simu ya Waratibu wa uchaguzi wa mikoa na vituo vyao vya kazi.

Kifungu cha 10(1) kifutwe ili kuondoa sharti la Mtu aliyewekwa kizuizini na Rais kutokuwa na sifa ya kuandikishwa kuwa mpiga kura. Sheria ya kuweka watu kizuizini ilipendekezwa kufutwa na Tume ya Jaji Nyalali.

- Kifungu cha 10(1)(c) kifutwe, kumzuia Mtu aliyefungwa kifungo cha miezi sita kutoandikishwa sio sahihi; miezi sita ni mifupi sana na kwa hivyo itasababisha watu wengi kukosa kuandikishwa kuwa wapiga kura.

Hata wafungwa Ni raia wa Tanzania na wana haki ya kuandikishwa na kuwa wapiga kura.

Kifungu cha 14(6) wafungwa raia wa Tanzania wanaotumikia vifungo wawe na haki ya kupiga kura na kama kina Sheria inayowazuia ifanyiwe marekebisho kwa kuwa pamoja na kutumikia vifungo bado ni Watanzania na wanayo haki ya kuchagua viongozi.

Kifungu cha 15 kifanyiwe marekebisho ili kuwe na kiapo cha Mtu ambaye majina yake yamebadilika ili kuepuka kuongeza wapiga kura kwa sababu ya mtu kuwa majina tofauti.

Kifungu cha 17(7) kifutwe, kusiwe na kiapo cha kutunza siri kwa Wakala wa uandikishaji. Wakala ameteuliwa na Chama na kwa maana hiyo awe na uhuru wa kutoa mrejesho wa kinachoendelea kwa mamlaka yake ya uteuzi.

Kifungu cha 18(3) kina makosa ya kimantiki hakijaeleza ni taarifa gani Tume inaweza kuzichukua kutoka mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na namna taarifa hizo zitatumika kwenye zoezi la kuandikisha wapiga kura. Kuhamisha taarifa au kuunganisha mifumo ya taarifa (Data migration and data integration) kwenye mifumo miwili tofauti inaweza kunyima watu wengi fursa ya kupiga kura kwakuwa bado watu wengi hawajaingizwa kwenye mfumo wa NIDA.

Kifungu cha 20 kiongezwe kifungu kidogo cha 3 kuweka masharti kwamba Mtu ambaye kadi yake imeharibika alazimike kujaza fomu maalum au kiapo kabla ya kupatiwa kadi mpya na atakiwe kurudisha kadi iliyofutika au kuharibika.

Kifungu cha 13(2)(3) kinamtaka Mtu ambaye ameomba kurekebisha kadi na kukataliwa kukata rufaa Mahakamani. Kuwe na Kanuni au fomu maalum itakayotumika ili iwe rahisi kukata rufaa kwenda Mahakamani na kuepuka urasimu.

Vifungu vya 27(2) na 28(7) kuhusu kulipa dhamana ya fedha kwa kiasi kitakachoamuliwa na Tume kuhusu wale ambao hawataridhika na taarifa kwenye daftari la wapiga Kura kupinga taarifa hizo vifutwe. Itawafanya wananchi kutolalamikia makosa yaliyopo kwenye daftari kwa kuhofia kuingia gharama za kuweka dhamana hiyo. Mchakato wa wananchi kuhakiki daftari na kupinga taarifa ambazo sio sahihi usihusishe kuweka dhamana ya fedha.

Kifungu cha 30(1) kuhusu masharti ya kuweka dhamana ya fedha kabla ya kukata rufaa Mahakama ya Wilaya kuhusu kuongezwa au kufutwa kwenye daftari la Wapiga Kura masharti ya dhamana yafutwe.

Kifungu cha 30(2) kinaelekeza kwamba uamuzi wa Mahakama ya Wilaya kuhusu kufutwa au kuongezwa kwenye daftari la Wapiga ni wa mwisho. Kifungu kiboreshwe kwamba mtu asiporidhika na uamuzi wa Mahakama ya Wilaya anaweza kukata rufaa Mahakama Kuu na asiporidhika anaweza kukata rufaa kwa masuala ya kisheria pekee kwenda Mahakama ya Rufani.

Kiongezwe kifungu kidogo cha 10 kwenye kifungu cha 30 kuonyesha kwamba kutakuwa na fomu maalum zitakazokuwa kwenye Kanuni zitakazotungwa na Jaji Mkuu ya namna ya kukata rufaa.

Kifungu cha 30(4), (5),(6) kirekebishwe ili kuondoa masuala ya kutaifisha dhamana iliyowekwa kabla ya kukata rufaa ambayo tumependekeza ifutwe.

Kifungu cha 35(2)(b) kuhusu kutaifisha dhamana ya Mgombea Urais ambaye amepata chini ya moja ya kumi ya Kura zote kifutwe. Hakuna maana wala sababu ya kuweka sharti kama hilo.

Kifungu cha 37(6) kiandikwe upya kuruhu Mgombea Urais ambaye hajateuliwa na Tume kukata rufaa Mahakama Kuu na Rufaa husika kusikilizwa na kuamuliwa ndani ya 14 toka uamuzi wa kutoteuliwa au kuenguliwa kufanyika.

Kifungu cha 38(2) kiandikwe upya ili Mgombea pekee wa Urais kupata 50% +1 ya kura zote halali ndipo atangazwe kuwa mshindi na kuondoa sharti la kura nyingi pekee.

22.Kifungu cha 45(10) kiandikwe upya ili mshindi wa kiti cha Urais atakiwe kupata 50%+1 ya kura zote halali ndipo atangazwe kuwa amechaguliwa.

Kiongezwe kifungu cha 45(11) ili kama hakuna Mgombea wa kiti cha Urais aliyepata 50%+1 ya kura zote halal, uchaguzi urudiwe kwa Wagombea wawili waliopata kura nyingi zaidi.

Kifungu cha 46 cha marudio ya uchaguzi wa Rais kirekebishwa kiendane na masharti ya kifungu cha 45(10) baada ya marekebisho.

Kifungu cha 51(2) kirekebishwe kuondoa sharti kutaifisha dhamana Mgombea wa Ubunge asipopata moja ya kumi ya Kura zote halali.

Kifungu cha 53(6) kifanyiwe marekebisho ili kufanya yafuatayo;

Mgombea asiyeridhika na uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi kuhusu pingamizi akate rufaa moja kwa moja kwenda Tume ya uchaguzi na sio kupitia kwa Msimamizi wa Uchaguzi ambao wanaamua kuhusu pingamizi Na kupokea rufaa Na kuchelewa kuziwasilisha Tume kwa makusudi. Time ipewe angalau siku 10 kuamua rufaa ili kutopotezea Wagombea muda wa kufanya kampeni.

Sababu za pingamizi zijikite kwenye sifa za kugombea Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 67 ya Katiba pekee, hivyo kifungu cha 51(1) cha muswada kifutwe.

Uamuzi wa Tume kuhusu rufaa uhojiwe Mahakama Kuu na Mahakama baada ya kusikiliza iwe Na uwezo kumrudisha Mgombea kuendelea na kampeni. Utaratibu huu utakuwa sawa Na ule wakati uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapiga Kura.

Kifungu cha 54(2) kiandikwe upya ili kuweka sharti kwa Mgombea pekee wa Ubunge kupata 50%+1 ya Kura zote halali ndipo atangazwe kwamba amechaguliwa.

Kifungu cha 60(1)(e) kinamuondolea sifa Mtu aliyewekwa kizuizini kuteuliwa kugombea udiwani. Kifungu na Sheria ya kuweka watu kizuizini ifutwe.

Kifungu cha 63(2) kinachoweka masharti ya kutaifisha dhamana ikiwa Mgombea Udiwani hatopata moja ya kumi ya Kura zote halali kifutwe.

Kifungu cha 65(7) kirekebishwe ili Mgombea wa nafasi ya udiwani aweze kukata rufaa moja kwa moja kwenda Tume. Baada ya kupokea rufaa Tume iamuru Msimamizi wa Uchaguzi kuwasilisha taarifa au utetezi wake ndani ya siku tatu toka siku ya uamuzi wake na Tume itaamua kuhusu rufaa ndani ya siku 10 toka siku rufaa husika ilipowasilishwa. Kuwe Na nafasi ya Mgombea udiwani kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Tume.

Kifungu cha 66(2) kiandikwe upya ili Mgombea pekee wa udiwani apate 50%+1 ya Kura zote halali ndipo atangazwe kuwa amechaguliwa.

Kifungu cha 77(1) kirekebishwe ili kuondoa maneno “… baada ya kupata ridhaa ya Wagombea…” hii Ina maana kwamba Wakala wa upigaji Kura atateuliwa Na Chama baada ya Chama kupata ridhaa ya Mgombea jambo ambalo sio sahihi.

Vifungu vya 112 na 113 vya Muswada kuhusu Wabunge na Madiwani Maalum vifutwe na kuandikwa ili kuboresha utaratibu wa namna ya kuwapata wawakilishi hao kikatiba.

Kifungu cha 102(c) maneno “… iwapo fomu za matokeo zipo za kutosha….” Yafutwe ili kulazimu Msimamizi wa uchaguzi kumpatia Wakala nakala ya matokeo ya uchaguzi.

Kifungu cha 125 (1)(2)(3)(4)(5)(6) na (7) kuhusu kiapo cha kutunza siri na adhabu zake dhidi kwa Mawakala na Wagombea pamoja na kuwazuia Mawakala kutokuwa na mawasiliano na Chama au Mgombea kitatoa mwanya kwa Wasimamizi wa uchaguzi kufanya jambo lolote kwenye vituo vya kupigia kura na Wakala hatachukua hatua yoyote kwa sababu ya kiapo cha kutunza siri. Kifungu hiki kilitungwa wakati nchi ikiwa ya Chama kimoja na hakina nafasi kwa wakati huu wa demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa.

Kifungu cha 135(1) katazo la kuvaa, kuonesha nembo ya kumuunga mkono Mgombea au Chama lisifanyike ndani ya mita mia moja toka kituo cha kupiga kura. Masharti ya mia tatu kwenye muswada yarekebishwe, kwa sababu maeneo ya mijini vituo vingi vya Wapiga kura vinakaribiana, watu wengi watatiwa hatiani kwa masharti haya.

Kifungu cha 140(1)(2)(3)(4)(5)(6) na (7) kwa upande wa Ubunge na kifungu cha 150(1)(2)(3)(4)(5)(6) na (7) kwa upande wa Udiwani kuhusu masharti ya kuweka dhamana ya fedha Mahakamani kabla ya kusikilizwa shauri la kupinga matokeo ya Ubunge na Udiwani vifutwe. Mashauri ya Uchaguzi ni Mashauri kama yalivyo mashauri mengine ya madai. Hivyo baada ya shauri la uchaguzi kuhitishwa utaratibu wa kudai gharama kwa Mdaawa aliyepewa tuzo ufanyike. Kuweka masharti ya kulipa gharama ni ubaguzi kwa sababu asiyekuwa na fedha za kuweka hataweza kusikilizwa Mahakamani.

Kifungu cha 166 Tume ilazimike kutumia teknolojia na itumie njia nyingine kama kuna changamoto ambazo zitalazimu kufanya hivyo. Maneno “inaweza” yafutwe.

Sehemu D: Hitimisho​

Ili kuondoa changamoto katika mfumo wetu wa uchaguzi nchini kwa ajili ya kuwa na uchaguzi huru utakaozingatia misingi ya haki ni vyema Serikali ikasitisha kuendelea na muswada wa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ili kutoa nafasi ya kuwasilisha kwanza Muswada wa marekebisho ya Katiba ya mwaka 1977 ili kuondoa kasoro zilizopo kikatiba ndipo mengine yafuate kama ilivyoelezwa hapo awali.

SURA YA PILI

MUSWADA WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI WA MWAKA 2023

Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi bado wanateuliwa na Rais kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) na 10 cha Muswada. Muswada umeendelea kumpa mamlaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa hali ya sasa yeye ni Mwenyekiti wa Chama cha

Mapinduzi.

Wajumbe wengine watano wa Tume nao huteuliwa na Rais kama ilivyo kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume kwa mujibu wa kifungu cha 5(1)(2) na 10(1),(2) cha muswada isipokuwa Wajumbe watapitia kwenye Kamati ya Usaili inayoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha Muswada.

Mkurugenzi wa Uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 18(1) cha Muswada anateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ambayo kwa kiasi kikubwa ni Tume ya Rais.

Kamati ya usaili inayoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 9 inaundwa na Wajumbe watano (Jaji Mkuu wa JMT, Jaji Mkuu wa SMZ, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Rais). Wajumbe wote hawa huteuliwa na Rais na kwa maana hiyo ni Kamati ya Usaili ya Wateule wa

Rais. Hakuna ushiriki wa Wajumbe wa Vyama vyenye ushiriki Bungeni, Vyama vya kitaaluma kama TLS, ZLS, hakuna ushiriki wa viongozi wa dini, Mashirika na taasisi zisizo za kiserikali.

Muswada haujaeleza chochote kuhusu haja ya Tume kuwa na Watumishi wake mpaka ngazi ya Mkoa, Jimbo na Kata ili kuondokana na changamoto ya kuwatumia Makatibu Tawala kuwa waratibu wa uchaguzi wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi kwenye Majimbo na Watendaji wa Kata kuwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika ngazi ya Kata. Kifungu cha 21 cha muswada bado kinazungumzia watumishi waliozimwa na Tume kuwa ni waajiriwa wa Tume na hivyo kutakiwa kufuata Kanuni na Miongozo ya Tume jambo ambalo kiuhalisia haijawahi kuwa hivyo kwa sababu wamekuwa wakifuata maelekezo ya aliyewateua na wengine wengi ni makada wa CCM. Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halamashauri ni Wateule wa Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.

Pamoja na Tume kuwa na jukumu la kuchunguza mipaka na kugawa majimbo ya uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 11(1)(c) cha Muswada, bado haiwezi kuwa huru kutekeleza majukumu yake kwa kuwa Tume itatakiwa kupata kibali cha Rais kwa mujibu wa ibara ya 75(1)(2) ya Katiba ya mwaka 1977.

Hakuna kifungu chochote katika Muswada kinachotoa masharti kwa Tume kuhusu haja ya uundwaji wa majimbo ya uchaguzi kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya Watu (population quota).

Muswada hautoi fursa kwa Mtu yeyote kuhoji uamuzi wa Tume baada ya kugawa majimbo, na hii ni kwa sababu ya kikwazo cha Katiba ibara ya 75(6) kinachozuia Mahakama yoyote kuhoji uamuzi wa Tume kuhusu mgawanyo wa mipaka.

Uwepo wa kikwazo kama ilivyoelezwa katika sehemu ya 7 hapo juu, kunapelekea kuwa na tatizo la uundwaji wa Majimbo ya Uchaguzi kwa upendeleo wa Chama, Kiongozi au Mtu fulani (Gerrymandering).

Muswada uongeze katika majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwa ni pamoja na kutunga Kanuni za kusimamia uchaguzi huo kwa kushirikiana na wadau.

Maoni ya jumla kuhusu muswada huu;

Muswada huu uondolewe Bungeni na kwenda kuandikwa upya kama tulivyopendekeza kwenye maoni ya jumla.

SURA YA TATU

MUSWADA WA SHERIA YA GHARAMA ZA UCHAGUZI NA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA

A. Sheria ya Gharama za Uchaguzi


Kifungu cha 4 Muswada kinafanya marekebisho ya kifungu cha 7(3)(b)(c) ambapo kinawaondoa Katibu Tawala na Mtendaji wa Kata mamlaka ya kuidhinisha timu ya kampeni ya Mgombea wa Ubunge na Udiwani na badala yake, timu ya kampeni ya Mgombea Ubunge itaidhinishwa na Msimamizi wa Uchaguzi na Udiwani ataidhinishwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi. Kwa upande wa Mgombea Urais, Msajili wa vyama amebaki na mamlaka ya kuidhinisha timu ya kampeni ya Mgombea Urais. Utaratibu wa kuidhinisha timu ya kampeni ifutwe, hakuna mantiki wala sababu ya msingi kufanya hivyo zaidi kuminya uhuru wa wagombea na timu zao za Kampeni wakati wa uchaguzi.

Kifungu cha 5 cha Muswada kinaandika upya kifungu cha 9(1)(2) ambapo Sheria inaweka masharti kwa Wagombea Urais,, Ubunge na

Udiwani kuwasilisha kwa Tume, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo na Msimamizi Msaidizi wa Kata kiasi cha fedha wanachotegemea kupokea kwa ajili ya uchaguzi, taarifa hiyo iwasilishwe na taarifa za benki na iwasilishwe kabla ya siku ya uteuzi. Kabla ya hapo utaratibu ulitaka taarifa husika kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Chama kwa Mgombea Urais na kwa Katibu wa Wilaya kwa Wagombea Ubunge na Udiwani. Tunapendekeza utaratibu wa zamani urudishwe kwa mapendekezo Serikali inalenga kuwabana Wagombea hasa wa Vyama vya Upinzani.

Kifungu cha 6 kinafanyia marekebisho kifungu cha 13(4) Sheria kuweka masharti kwa taasisi za dini na mashirika yasiyokuwa ya Serikali kuwasilisha taarifa ya fedha walizotumia wakati wa uchaguzi ndani ya siku 90 kwa uchaguzi Mkuu na ndani ya siku 30 kwa uchaguzi mdogo. Masharti haya yalikuwepo isipokuwa Muswada umeongeza masharti ya kuwasilisha taarifa baada ya uchaguzi mdogo.

Kifungu cha 7 cha Muswada kinafanyia marekebisho kifungu cha 18 cha Sheria kwa kuandika upya vifungu vidogo vya 1, 2 na 3 ambapo masharti ni yaleyale isipokuwa yameongezwa masharti kwa Chama kuwailisha taarifa ya matumizi wakati wa uchaguzi mdogo ndani ya siku 60 baada ya uchaguzi na ndani ya siku 180 baada ya uchaguzi mkuu. Aidha Wagombea watatakiwa kuwasilisha taarifa ya matumizi kwa Katibu Mkuu wa Chama ndani ya siku 60 baada ya uchaguzi mkuu na ndani ya siku 30 baada ya uchaguzi mdogo.

Muswada haujafuta au kufanyia kifungu cha 12 cha Sheria ambacho kinazuia kuingiza fedha au vifaa vya kampeni siku 90 kabla ya siku ya uchaguzi. Suala hili linaathiri sana Vyama kwa sababu masharti ya siku 90 kabla ya siku ya uchaguzi Wagombea bado hawajateuliwa na Tume na kuleta changamoto kuingiza vifaa vya uchaguzi.

B. Sheria ya Vyama Vya Siasa

1. Kifungu cha 11 cha muswada kinaongeza vifungu vidogo vya 7, 8 na 9 kwenye kifungu cha 6C cha Sheria; Sheria inafanyiwa marekebisho kwa kukipiga faini ya milioni 20 au kukifuta Chama ambacho Mtu ambaye si raia wa Tanzania atashiriki kwenye mchakato wa kufanya maamuzi kwenye Chama. Muswada haujafafanua maana ya

mchakato wa kufanya maamuzi (decision making process) masharti haya yakiachwa kama yalivyo yanampa Msajili wa Vyama mamlaka ya kutafsiri kama anavyotaka.

Mjumbe wa kikao cha chini aliyeshiriki kuamua jambo fulani, hataruhusiwa kupiga kura kwenye kikao kitakachoketi kusikiliza rufaa. Pendekezo hili limetungwa mahususi kwa Chadema baada ya kuwafukuza wasaliti 19 na Baraza Kuu la Chama kukataa rufaa zao kwa kura, jambo hilo lilifanyika mbele ya Msajili Msaidizi wa Chama. Kifungu hiki kifutwe.

Muswada pia unaelekeza rufaa zote dhidi ya uamuzi wa vikao vya Chama ziwasilishwe kwa Katibu Mkuu.

Kifungu cha 12 cha Muswada kinaweka sharti kwa Chama

kinachoomba usajili wa muda kuwasilisha Katiba na Kanuni zake kwa Msajili. Aidha muswada unaongeza masharti kwamba Chama hakitapewa usajili wa muda kama kinahatarisha usalama wa taifa. Sharti hilo lifutwe kwa sababu tafsiri ya maneno usalama wa Taifa haipo kwenye Sheria na hivyo kutoa nafasi Mtu kukinyima Chama usajili kwa sababu tafsiri yake kwa namna anavyoona na si kwa mujibu wa Sheria.

Kifungu cha 13 cha Muswada kinaongeza kifungu kipya cha 10C, ambacho kinaweka masharti ya nyaraka zinazopaswa kuwa kwenye Masjala ya Chama chenye usajili wa kudumu.

Kifungu cha 14 kinaongeza neno “maandamano” kwenye kifungu cha 11 (2) kuwa yatapaswa kufanywa kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Jeshi la Polisi. Kimsingi masharti haya yanazidi kuwapa mamlaka Jeshi la Polisi kuzuia maandamano ya Vyama vya siasa ambayo ni haki kwa mujibu wa kifungu cha 11(1) cha Sheria.

Kifungu cha 15 kinafanyia marekebisho kifungu cha 11A kinaongeza masharti ya vyama kushirikiana wakati wa uchaguzi mdogo.

Kifungu cha 16 cha Muswada kinafanyia marekebisho kifungu cha 13A kwa kumpa mamlaka ya Msajili kupokea taarifa yoyote ya ukiukwaji wa kifungu chochote cha Sheria ya Vyama.

Kifungu cha 17 kinafanyia marekebisho kifungu cha 16(3)kuhusu masharti ya kupata ruzuku kwa kufuta maneno “uchaguzi wa Serikali ya Mitaa” na kuweka maneno mapya ya uchaguzi mkuu na uchaguzi mdogo. Hii kwa sababu Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utasimamiwa na Sheria moja kwa mapendekezo ya sasa.

Kifungu cha 18 na 19 kinafanyia marekebisho ya kifungu cha 19 na 20 kuweka masharti na kumuongezea mamlaka Msajili kukisimamisha Chama (suspend) isipokuwa atatakiwa kukiandikia na uamuzi wake ni wa mwisho.

Kifungu cha 20 kinafanyia marekebosho kifungu cha 21E(2) ambapo kinatoa adhabu kwa Mwanachama anayeshiriki kufanya shughuli za Chama ambacho kimesimamishwa.

Kifungu cha 21 cha muswada kinaongeza jedwali la 3 kwenye Sheria kuweka sharti kwa kila Chama kuwa program za social inclusion na masuala ya jinsia, kuwajengea uwezo Wanawake na kuwa na dawati maalum la kushughulikia masuala ya Wanawake na social inclusion.

Muswada huu haujagusa kabisa na haujaheshimu amri ya Mahakama ya Afrika Mashariki iliyotolewa kwenye Consolidated Reference No. 3&4 of 2019 Freeman Mbowe and 5 others V. The Attorney General of the United Republic of Tanzania uamuzi ulitolewa tarehe 25 Machi,

2022 ambapo Serikali ya Tanzania kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliamriwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa kwa sababu vifungu vya 4(4), 6A, 6B, 6C, 8C,8D,8E, 11A, 21D na 21 B vya Sheria ya Vyama vilivyofanyiwa marekebisho na vifungu vya 3,5,9,15 na 29 vya The Political Parties (Amendment) Act ya mwaka

2019 kuwa vinakiuka ibara ya 6(d), 7(2) na 8(1)(c) vya mkataba wa Afrika ya Mashariki. Badala ya kufanyia marekebisho sheria husika ili kuheshimu amri ya Mahakama ya Afrika ya Mashariki bado serikali imeongeza masharti mapya yanayokiuka amri hiyo katika baadhi ya vifungu ambavyo Mahakama imeshatoa amri kwamba vinakiuka

Mkataba wa Afrika ya Mashariki.

Maoni ya jumla kuhusu muswada huu;

Kuwe na marekebisho ya Katiba ya sasa kuipa uhuru wa kikatiba ofisi ya Msajili na uamuzi wa Msajili uweze kukatiwa rufaa au mapitio Mahakama Kuu na sio kuacha uamuzi wa Mtu mmoja

utamalaki.

Pamoja na pendekezo la awali, muswada huu uondolewe Bungeni na kuandikwa upya ili kuipa ofisi ya Msajili uhuru na kuondoa mapungufu mengine mengi ikiwa ni pamoja na kutekeleza amri ya Mahakama ya Afrika Mashariki.
 

Attachments

  • MSIMAMO WA CHADEMA - MISWADA.pdf
    272.7 KB · Views: 6
masuala ya uchaguzi na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa

Mjadala huu unatakiwa sasa uendelee katika majukwaa yote ya kijamii, magazeti, vituo vya radio, televisheni na online TV ili hadi tarehe 30 January 2024 bunge la chama kimoja kongwe watapokutana bungeni kupitia ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge waelewe msimamo wa umma mpana ambao upo nje ya mfumo wa bunge wanataka nini
 
Mungu ibariki Chadema

Yani CHADEMA mnapendekeza bunge liwe double the size, mna akili vichwani kweli nyinyi ?????

Eti kila jimbo lipige kura kwa mwanamke na kwa mwanamme. Kwani wanaenda kuchumbiana mle bungeni ????

Basi na kila wizara tuwe na waziri mwanamke na mwanamme!

Every freaking where, tuwe na pair za kijinsia! Na Mwenyekiti wa CHADEMA tupate na mwanamke pia, kum-pair na Mbowe!

Wretchedly poor third world country mnafikiria ku double the legislature?

Most imbecilic proposition in political history of the world
 
Yani CHADEMA mnapendekeza bunge liwe double the size, mna akili vichwani kweli nyinyi ?????

Eti kila jimbo lipige kura kwa mwanamke na kwa mwanamme. Kwani wanaenda kuchumbiana mle bungeni ????

Basi na kila wizara tuwe na waziri mwanamke na mwanamme!

Every freaking where, tuwe na pair za kijinsia! Na Mwenyekiti wa CHADEMA tupate na mwanamke pia, kum-pair na Mbowe!

Wretchedly poor third world coutry mnafikiria ku double the legislature?

Most imbecilic proposition in political history of the world
Wewe ndio wale Chawa wa zamani ! Hivi bado mamaako ni Mwenyekiti wa ccm?
 
Mapendekezo mazuri sana. Sasa tuone hizo 4R ambazo tunajua ni utapeli zitasimama wapi.
Mapendekezo mazuri yepi?

Dirt poor Third World country, masikini wachafu, mnataka bunge la sasa la watu 400 liwe na watu 800!

Halafu you know full well CCM watazoa vast majority of those seats, kwa halali au kwa kuiba au kwa kuua watu kupitia jeshi la Polisi, Usalama na Wakurugenzi wa Halmashauri. CCM siku zote wanakomba the preponderant majority of the seats. Kwa hiyo mnapendekeza kuwaongezea CCM nafasi bungeni ili waongeze kula na kuvimbiwa jasho la wananchi.

Mna nini vichwani, homa ya kimeta ?
 
Ungeweka kwa mtindo wa PDF ingekuwa poa mkuu.
 
Mapendekezo mazuri yepi?

Dirt poor Third World country mnataka bunge la sasa la watu 400 liwe na watu 800!

Halafu you know full well CCM watazoa vast majority of those seats, kwa halali au kwa kuiba au kwa kuua watu. CCM siku zote wanazoa preponderant majority of the seats. Kwa hiyo mnapendekeza kuwaongezea CCM nafasi bungeni ili waongeze kula na kuvimbiwa jasho la wananchi.

Mna nini vichwani
?
Ila MKUU punguza hasira basi daaah😁😁😁
 
Mapendekezo mazuri yepi?

Dirt poor Third World country mnataka bunge la sasa la watu 400 liwe na watu 800!

Halafu you know full well CCM watazoa vast majority of those seats, kwa halali au kwa kuiba au kwa kuua watu. CCM siku zote wanazoa preponderant majority of the seats. Kwa hiyo mnapendekeza kuwaongezea CCM nafasi bungeni ili waongeze kula na kuvimbiwa jasho la wananchi.

Mna nini vichwani
?
Wewe unatoa wapi huo ujinga wako ?
 
Mapendekezo mazuri yepi?

Dirt poor Third World country mnataka bunge la sasa la watu 400 liwe na watu 800!

Halafu you know full well CCM watazoa vast majority of those seats, kwa halali au kwa kuiba au kwa kuua watu. CCM siku zote wanazoa preponderant majority of the seats. Kwa hiyo mnapendekeza kuwaongezea CCM nafasi bungeni ili waongeze kula na kuvimbiwa jasho la wananchi.

Mna nini vichwani
?
Wanaweza kuwa wengi na vikao vya bunge vikapungua muda, ikiwemo na viwango vya malipo. Wenzako wanataka utawala wa majimbo sio lazima wote wakusanyike hapo Dodoma. Mipango ya cdm kisha unataka watumie modality ya ccm?!
 
Mapendekezo ya jumla na msimamo wa CHADEMA juu ya miswada ya sheria iliyowasilishwa bungeni 10, Novemba 2023 inayohusu masuala ya uchaguzi na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa
Chadema inastahili pongezi
Tangu zoezi la kukusanya maoni lianze, maoni ya Chadema ndio the most exhaustive na bango kitita lake ndilo bango kitita kubwa kuliko michango yoyote!.

P
 
Wanaweza kuwa wengi na vikao vya bunge vikapungua muda, ikiwemo na viwango vya malipo.
CHADEMA hawajasema wanataka vikao vya bunge vipunguzwe wala malipo yapunguzwe. Wamesema, kwenye submission yao ya John Mnyika leo, wanataka kila jimbo liwe na wabunge wawili wa kuchaguliwa, mmoja mwanamke mmoja mwanamme.

Kwa hio, kwa mapendekezo ya CHADEMA, bunge hili la sasa la watu 400 linaenda kuwa na watu 800!

Tuwe na Rais wa kike na kiume basi! Na diwani mwanamke na mwanamke. Mana tunatafuta jozi za wawili wawili wa kwenda kuchumbiana kwenye vikao!

Ni mtu gani mwenye akili kichwani, wa chama cha upinzani cha nchi ya dunia ya tatu, ya watu masikini wa kutupwa, wachafu wenye njaa, wanaoshindia mihogo na maji machafu ya mitoni, biashara za masinia ya ndizi vichwani, boda boda na mama ntilie, anaependekeza kuongeza gharama za kutajirisha viongozi ???
 
Back
Top Bottom