Teko Modise

JF-Expert Member
May 20, 2017
1,914
6,033
Kuna tetesi kuwa Tundu Lissu amekamatwa na Polisi asubuhi hii akiwa hotelini huko Karatu.

Taarifa zaidi kukujia hapahapa jukwaani.

UPDATE:
Waliokamatwa Karatu hadi sasa ni
  1. Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu
  2. Walinzi wote wa Tundu Lissu
  3. Katibu wa BAWACHA Catherine Ruge
  4. Mzee Hashim, Mwenyekiti Wa Baraza La Wazee CHADEMA Taifa
  5. Suzan Kiwanga na
  6. Mwandishi wa Jambo TV (Oscar).

Polisi wanaendelea kuwatafuta wengine walio ambatana na Tundu Lissu Wilayani Karatu

20230910_114116.jpg


====

Leo Septemba 10, 2023 Majira ya saa nne asubuhi Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu lilifika Hotel ya Ngorongoro iliyopo Karatu na kuizingira, Polisi hao wakiwa na mitutu ya bunduki pamoja na mabomu. Jeshi hilo liliwaeleza wahudumu wa hotel hiyo kuwa wanataka kujua chumba alicholala Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara Mhe. Tundu Lissu wakaelezwa na kwenda kwenye chumba hicho.

Baada ya purukushani ya Jeshi la Polisi na walinzi wa Mhe. Lissu, Jeshi hilo lilingia kwa nguvu katika chumba alichofikia Mhe. Lissu na kuondoka nae bila kueleza wanaenda nae wapi.

Baadae wengine waliokamatwa na Jeshi hilo ni Mhe. Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Catherine Ruge Katibu Bawacha Taifa, Mhe. Twaha Mwaipaya, walinzi wa Mhe. Lissu pamoja na watu wengine.

Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea Karatu.

Samwel Welwel

===

Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu wameamuru kufungwa kwa ofisi ya Chadema wilaya ya Karatu na kuwakamata watu wengine wakiwemo viongozi wa Chadema wa wilaya hiyo.

1. Joseph Mtui
2. John Malle
3. Fabiola Niima
4. Daniel Mnyampanda
5. Eliya Kibola, Katibu wa Chadema wilaya ya Karatu
6. Valerian Qurama
7. Samwel Welwel, Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Karatu
 
Kwenye nchi za watu weusi inataka moyo wa chuma kutetea raia wake ambao kimsingi hata hawaelewi haki zao na faida ya mwanaharakati kama tundu lissu, freeman Aikaeli, John pambalu, twaha mwaipaya na wengine wengi.. Itafika wakati mapinduzi yafanywe na wachache tu tukitegemea watanzania waandamane kudai haki hapo hatutaweza

Kifuatacho ni Chama kuandaa mbinu kabambe za kukabiliana na ccm pasipo nguvu ya umma maana umma wenyewe hawana meno ndio maana serikali inajitafunia nchi inavyotaka.. Tundu lissu inabidi ajuwe kuwa hao anaowatetea ndohaohao wakishapewa ardhi ya ngorongoro watamshukuru Samia Kwa kuwaacha waendelee kuishi ndani ya hifadhi kuliko lissu aliepambana kuwatetea
 
Back
Top Bottom