USHAURI: Kwako Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu

Myfriend

Member
Aug 14, 2023
59
85
Salaam Mhe. Tundu lissu, Natumaini unaendelea vema. Mhe. Tundu lissu nikiri kwamba mimi ni miongoni mwa watanzania ninayekupenda na kukufatilia sana.

Naamin kabisa katika siasa za Tanzania wewe ndiye mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kwa sasa. Ushawishi wako unajengwa na misimamo yako na uelewa mkubwa ulionao katika maswala ya sheria na kimataifa. Eneo hili unalitendea haki kwelikweli. Ukweli usiopingika wewe ni mbishi sana na unaamin unachokisimamia, upo tayari kukifia na kukifanya kwa Gharama yoyote unahulka kama za Magufuri ila tofauti yenu ni kwamba wewe ulkuwa na uelewa wa mambo ya sheria na uko tayari kukosolewa, Hayati Magufuli alikuwa amenyooka, anadhubutu kufanya anachoamini na hakutaka ushauri na kukosolewa.

Mhe.Tundu lissu, naamini kupitia chama chako kama itawependeza utapitishwa kugombea tena nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

leo kupitia jukwaa hili naomba nikushauri mambo 3 tu, ninayoyaona kwako na ninayoamin watanzania wengi watayapenda, Inawezekana nisiwe sahihi sana lakin kwa mtazamo wangu kama utaamua kuyafanya, itakuongezea ushawishi maradufu.

1. UTATUZI WA MATATIZO YA JAMII.
Watanzania wanapenda kutatuliwa matatizo katika jamii, hawataki kujua aliyeyaleta au kuwasababishia.

Magufuli aliliweza hili, alkuwa tayari kuikana CCM ili tu kuwaonesha kuwa yeye yupo kutatua matatizo ya jamii,Viongozi waliokosea hakusita kuwasema, kuwapa onyo na kalipio kali au kuwatumbua,hii ni njia iliyompa umaarufu sana hasa kwa watu maskini. Watanzania wala hawajali kama matatizo yote haya yameletwa na CCM lkn wanahtaji mtu atakaeweza kuwasemea tena kwa ukali bila hofu,anaeonya na anaeonesha utatuzi.

Kwa sasa huna uwezo wa kimamlaka kutatua matatizo ya jamii,lakini unaweza kusababisha utatuzi na jamii ikaona wewe ndiye uliyeleta suluhu,katika ziara za kisiasa utakazofanya sasa jikite sana katika kueleza matatizo yaliyopo katika jamii, waseme watendaji wazembe, wanaojitahidi wape stahiki yao,lakini pia wambie wananchi wewe ukishika mamlaka utafanya lipi au utatatuaje hayo matatizo waliyonayo.

2. USITUMIE MUDA MWINGI KUMLAUMU MAGUFULI, HILI WATANZANIA WANALIJUA VIZURI KWA SASA.
Naomba niweke wazi tu katika hili. Kama nilvoeleza licha ya mapungufu mengi aliyokuwa nayo magufuri lakini mpaka sasa wananchi wa kawaida na hata baadhi ya watanzania wanamkumbuka magufuli hasa katika hatua zake nyingi za haraka alizokuwa anachukua kutatua changamoto za kiutendaji serikalini, kwa sasa hakuna kiongozi mwenye udhubutu huo,Raisi anaagiza lakin maagizo yake hayazingatiwi na watendaji.

Mfano tu Rais ameagiza mara nyingi kutocheleweshwa malipo ya makandarasi hasa wazawa ambayo hulimbikizwa na mwisho wa siku wanaanza kucharge interest za kuchelewehewa malipo lakini ukweli ni kwamba wakandarasi wa ndani na wazabuni sasa ni zaidi ya miezi takribani 10 hawajalipwa, ukitoa miradi ya TARURA labda na TANROAD na hazina wanajua hili na hakuna anaewajibika.

Watanzania wengi wanajua hukutendewa haki,ulionewa na halkuwa jambo jema kabisa kushambuliwa lakin kwa sasa wanawaza sana matatizo waliyonayo,wanataka kiongozi anayesema na wasaidizi kutii na kufanya,wanamkumbuka magufuri ndo mana wanamuona makonda kama anaweza kuvaa viatu vyake.

Watanzania wamechoka na siasa za uchawa, hawapendi kiongozi anayesema tu bila utekelezwaji, wewe ndie unaeweza kusema na kutenda, unaweza kusimamia ulichosema na kikatendeka,kwa sasa jikite katika kuwakusanya watanzania kwa pamoja bila kuajli itikadi zao na bila kujali walimpenda nani.

Hakika nakwambia Tundu Lissu, Watanzania wanakuamini usiwaangushe kuna kitu unawanyima.

3. USIKAE KIMYA SANA HASA WATANZANIA WANAPOKUMBWA NA JAMBO KATIKA JAMII.
Inawezekana kuna ile hali ya kusema ngoja wote tuongee lugha moja,lkn watanzania ni wasahaulifu sana, ikitokea tatzo walilonalo limeisha wanajisahaulisha. Mfano kwa sasa kunatatizo kubwa la kukatika kwa umeme na mgao wa maji baadhi ya maeneo.

Hakuna kiongozi yoyote wa serikali aliyeingilia kutatua hili swala, hata kauli za Viongozi wa kuu wa serikali zinaonesha zimekaa kisiasa na utani tu.mimi naamini nyakati kama hizi hustahili kuwa kimya, na hii itawafanya Viongozi waamke lkn watanzania wataona wewe ndo umewapa msaada. kiongozi uskate tamaa kuaddress matatizo lakini kila wakati ukiaddress jitahidi sana kuonesha mbadala wa kutatua.

Mhe.Tundu Lissu pamoja na wote mtakao wania nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkumbuke tu kwamba watanzania wengi ni maskini,mifumo ya uwajibikaji ni mibovu, elimu inayotolewa haijitoshelezi kuwezesha vijana kujiajiri lkn mifumo ya kusidia vijana kujiajiri ni mibovu pia, mifumo ya kufanya biashara si rafiki sana, Viongozi wengi wa juu serikalini ni mafisadi kwa kiwango kikubwa.

Mhe.Tundu lissu, umasikini ni mbaya sana,ni kama laana. Tafadhali ukiwa Raisi jitahidi kuinua kaya maskini, na vijana ikibidi kwa kutenga budget ya kuwalipa kila mwezi kiwango kizuri kitakachowainua kiuchumi, najua pia serikali ya CCM inafanya Hivyo lkn kinachofanyika ni uhuni na urasimu mkubwa sana, pesa zinatafunwa na haziwafikii walengwa no body cares in the system.

Mhe.Tundu lissu, naamin utakuwa Rais ajae. Najua unajua mengi sana katika jamii ya watanzania lkn naamn andiko langu litakusaidia walau kama si kufanya yote lkn utapata nafasi ya kutafakari upya.

Pamoja na ombi lako , lakini huwezi kutatua matatizo bila kuwataja waliyoyaleta na kuwatolea mfano , kwa mfano huwezi kuzungumzia Demokrasia ya Tanzania bila kumtaja Dikteta Magufuli , enzi za huyu mtu ndio viroba vilivyojaa maiti viliokotwa Baharini kila Wiki , baada ya yeye kuondoka na viroba vimepotea .

Huwezi kutatua changamoto kwa kuficha Ukweli
 
Salaam mhe.Tundu lisu,Natumaini unaendelea vema.
Mhe,Tundu lisu nikiri kwamba mimi ni miongoni mwa watanzania ninayekupenda na kukufatilia sana,Naamin kabisa katika siasa za Tanzania wewe ndiye mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kwa sasa. Ushawishi wako unajengwa na misimamo yako na uelewa mkubwa ulionao katika maswala ya sheria na kimataifa,Eneo hili unalitendea haki kwelikweli. Ukweli usiopingika wewe ni mbishi sana na unaamin unachokisimamia,upo tayari kukifia na kukifanya kwa Gharama yoyote unahulka kama za Magufuri ila tofauti yenu ni kwamba wewe ulkuwa na uelewa wa mambo ya sheria na uko tayari kukosolewa,Hayati Magufuri alikuwa amenyooka,anadhubutu kufanya anachoamini na hakutaka ushauri na kukosolewa.

Mhe.Tundu lisu,naamin kupitia chama chako kama itawependeza utapitishwa kugombea tena nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

leo kupitia jukwaa hili naomba nikushauri mambo 3 tu, ninayoyaona kwako na ninayoamin watanzania wengi watayapenda, Inawezekana nisiwe sahihi sana lakin kwa mtazamo wangu kama utaamua kuyafanya,itakuongezea ushawishi maradufu.

1.UTATUZI WA MATATIZO YA JAMII.
Watanzania wanapenda kutatuliwa matatizo katika jamii,hawataki kujua aliyeyaleta au kuwasababishia.Magufuri aliliweza hili,alkuwa tayari kuikana CCM ili tu kuwaonesha kuwa yeye yupo kutatua matatizo ya jamii,Viongozi waliokosea hakusita kuwasema,kuwapa onyo na kalipio kali au kuwatumbua,hii ni njia iliyompa umaarufu sana hasa kwa watu maskini. Watanzania wala hawajali kama matatizo yote haya yameletwa na CCM lkn wanahtaji mtu atakaeweza kuwasemea tena kwa ukali bila hofu,anaeonya na anaeonesha utatuzi.

Kwa sasa huna uwezo wa kimamlaka kutatua matatizo ya jamii,lakini unaweza kusababisha utatuzi na jamii ikaona wewe ndiye uliyeleta suluhu,katika ziara za kisiasa utakazofanya sasa jikite sana katika kueleza matatizo yaliyopo katika jamii, waseme watendaji wazembe,wanaojitahidi wape stahiki yao,lakini pia wambie wananchi wewe ukishika mamlaka utafanya lipi au utatatuaje hayo matatizo waliyonayo.

2. USITUMIE MDA MWINGI KUMLAUMU MAGUFURI,HILI WATANZANIA WANALIJUA VIZURI KWA SASA.
Naomba niweke wazi tu katika hili.Kama nilvoeleza licha ya mapungufu mengi aliyokuwa nayo magufuri lakini mpaka sasa wananchi wa kawaida na hata baadhi ya watanzania wanamkumbuka magufuri hasa katika hatua zake nyingi za haraka alizokuwa anachukua kutatua changamoto za kiutendaji serikalini,kwa sasa hakuna kiongozi mwenye udhubutu huo,Raisi anaagiza lakin maagizo yake hayazingatiwi na watendaji.Mfano tu Raisi ameagiza mara nyingi kutocheleweshwa malipo ya makandarasi hasa wazawa ambayo hulimbikizwa na mwisho wa siku wanaanza kucharge interest za kuchelewehewa malipo.lakini ukweli ni kwamba wakandarasi wa ndani na wazabuni sasa ni zaidi ya miezi takribani 10 hawajalipwa,ukitoa miradi ya Tarura labda na Tanroad na hazina wanajua hili na hakuna anaewajibika.

Watanzania wengi wanajua hukutendewa haki,ulionewa na halkuwa jambo jema kabisa kushambuliwa lakin kwa sasa wanawaza sana matatizo waliyonayo,wanataka kiongozi anayesema na wasaidizi kutii na kufanya,wanamkumbuka magufuri ndo mana wanamuona makonda kama anaweza kuvaa viatu vyake.

Watanzania wamechoka na siasa za uchawa,hawapendi kiongozi anayesema tu bila utekelezwaji,wewe ndie unaeweza kusema na kutenda,unaweza kusimamia ulichosema na kikatendeka,kwa sasa jikite katika kuwakusanya watanzania kwa pamoja bila kuajli itikadi zao na bila kujali walimpenda nani.

Hakika nakwambia Tundu Lisu,Watanzania wanakuamini usiwaangushe kuna kitu unawanyima.

3.USIKAE KIMYA SANA HASA WATANZANIA WANAPOKUMBWA NA JAMBO KATIKA JAMII.
Inawezekana kuna ile hali ya kusema ngoja wote tuongee lugha moja,lkn watanzania ni wasahaulifu sana,ikitokea tatzo walilonalo limeisha wanajisahaulisha. Mfano kwa sasa kunatatizo kubwa la kukatika kwa umeme na mgao wa maji baadhi ya maeneo.Hakuna kiongozi yoyote wa serikali aliyeingilia kutatua hili swala,hata kauli za Viongozi wa kuu wa serikali zinaonesha zimekaa kisiasa na utani tu.mimi naamini nyakati kama hizi hustahili kuwa kimya,na hii itawafanya Viongozi waamke lkn watanzania wataona wewe ndo umewapa msaada. kiongozi uskate tamaa kuaddress matatizo lakini kila wakati ukiaddress jitahidi sana kuonesha mbadala wa kutatua.

Mhe.Tundu Lisu pamoja na wote mtakao wania nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,mkumbuke tu kwamba watanzania wengi ni maskini,mifumo ya uwajibikaji ni mibovu,elimu inayotolewa haijitoshelezi kuwezesha vijana kujiajiri lkn mifumo ya kusidia vijana kujiajiri ni mibovu pia,mifumo ya kufanya biashara si rafiki sana,Viongozi wengi wa juu serikalini ni mafisadi kwa kiwango kikubwa.

Mhe.Tundu lisu,umasikini ni mbaya sana,ni kama laana.Tafadhali ukiwa Raisi jitahidi kuinua kaya maskini,na vijana ikibidi kwa kutenga budget ya kuwalipa kila mwezi kiwango kizuri kitakachowainua kiuchumi,najua pia serikali ya CCM inafanya Hivyo lkn kinachofanyika ni uhuni na urasimu mkubwa sana,pesa zinatafunwa na haziwafikii walengwa no body cares in the system.

Mhe.Tundu lisu,naamin utakuwa Rais ajae,Najua unajua mengi sana katika jamii ya watanzania lkn naamn andiko langu litakusaidia walau kama si kufanya yote lkn utapata nafasi ya kutafakari upya.
Tanzanian Moise Katumbi 🐒
 
Pamoja na ombi lako , lakini huwezi kutatua matatizo bila kuwataja waliyoyaleta na kuwatolea mfano , kwa mfano huwezi kuzungumzia Demokrasia ya Tanzania bila kumtaja Dikteta Magufuli , enzi za huyu mtu ndio viroba vilivyojaa maiti viliokotwa Baharini kila Wiki , baada ya yeye kuondoka na viroba vimepotea .

Huwezi kutatua changamoto kwa kuficha Ukweli
Mtoa mada yupo sahihi , the guy magufuli is no more , so we need to keep head up .

Lissu ajikite kuonesha njia bora za sisi kusonga mbele kirahisi maana tatizo la Watz ni mindset
 
Watanzania tulimpoteza Rais.

Mungu atuletee mwingine aina ya Magu ila tu asiminye upinzani.
 
Pamoja na ombi lako , lakini huwezi kutatua matatizo bila kuwataja waliyoyaleta na kuwatolea mfano , kwa mfano huwezi kuzungumzia Demokrasia ya Tanzania bila kumtaja Dikteta Magufuli , enzi za huyu mtu ndio viroba vilivyojaa maiti viliokotwa Baharini kila Wiki , baada ya yeye kuondoka na viroba vimepotea .

Huwezi kutatua changamoto kwa kuficha Ukweli
Ni sahihi kabisa mkuu, ktk hili lazima haki kwa waliotendewa uovu itaftwe,lkn yeye hayupo sasa na hiyo inaweza kuwa ni part ya maovu yake,lkn ground kwa wananchi wa kawaida tunaoamin ndo wapiga kura wengi wanamtazamo tofaut kwake.kumsema tu haitasaidia sana na nikuonekana inatafutwa sympathy,waliotenda uovu wengne bado wapo je tutaendelea kumsema tu yeye?
 
Pamoja na ombi lako , lakini huwezi kutatua matatizo bila kuwataja waliyoyaleta na kuwatolea mfano , kwa mfano huwezi kuzungumzia Demokrasia ya Tanzania bila kumtaja Dikteta Magufuli , enzi za huyu mtu ndio viroba vilivyojaa maiti viliokotwa Baharini kila Wiki , baada ya yeye kuondoka na viroba vimepotea .

Huwezi kutatua changamoto kwa kuficha Ukweli
Mkuu mtoa mada yupo sahihi.

Ni kweli hayati magufuli alikuwa dikteta lakini mh. Tundu lissu ajikite kuonyesha ni jinsi gani ya kutatua hizo changamoto zinazo watatiza watanzania wa hali ya chini.

Mfano, kama hiyo vdeo hapo ya magufuli.
 
Huna akili wewe! Mtoa mada amejenga hoja mjarabu
 
Mkuu mtoa mada yupo sahihi.

Ni kweli hayati magufuli alikuwa dikteta lakini mh. Tundu lissu ajikite kuonyesha ni jinsi gani ya kutatua hizo changamoto zinazo watatiza watanzania wa hali ya chini.

Mfano, kama hiyo vdeo hapo ya magufuli.
Kumbuka Magufuli alikuwa anashirikiana na akina Makonda , Bashiru Ally , Polepole , Kipilimba , Sirro , Kingai na wengine wengi ambao wako hai , Waliyoyafanya ni lazima yakemewe kwa kuwataja hadharani ili pasitokee tena uchafu ule , ni lazima watajwe hadharani ili Wananchi waliopotelewa na ndugu zao waelewe Wahusika halisi wa huu uharamia .

Shetani hapaswi kuhurumiwa na ndio maana anatajwa miaka yote
 
Salaam Mhe. Tundu lissu, Natumaini unaendelea vema. Mhe. Tundu lissu nikiri kwamba mimi ni miongoni mwa watanzania ninayekupenda na kukufatilia sana.

Naamin kabisa katika siasa za Tanzania wewe ndiye mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kwa sasa. Ushawishi wako unajengwa na misimamo yako na uelewa mkubwa ulionao katika maswala ya sheria na kimataifa. Eneo hili unalitendea haki kwelikweli. Ukweli usiopingika wewe ni mbishi sana na unaamin unachokisimamia, upo tayari kukifia na kukifanya kwa Gharama yoyote unahulka kama za Magufuri ila tofauti yenu ni kwamba wewe ulkuwa na uelewa wa mambo ya sheria na uko tayari kukosolewa, Hayati Magufuli alikuwa amenyooka, anadhubutu kufanya anachoamini na hakutaka ushauri na kukosolewa.

Mhe.Tundu lissu, naamini kupitia chama chako kama itawependeza utapitishwa kugombea tena nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

leo kupitia jukwaa hili naomba nikushauri mambo 3 tu, ninayoyaona kwako na ninayoamin watanzania wengi watayapenda, Inawezekana nisiwe sahihi sana lakin kwa mtazamo wangu kama utaamua kuyafanya, itakuongezea ushawishi maradufu.

1. UTATUZI WA MATATIZO YA JAMII.
Watanzania wanapenda kutatuliwa matatizo katika jamii, hawataki kujua aliyeyaleta au kuwasababishia.

Magufuli aliliweza hili, alkuwa tayari kuikana CCM ili tu kuwaonesha kuwa yeye yupo kutatua matatizo ya jamii,Viongozi waliokosea hakusita kuwasema, kuwapa onyo na kalipio kali au kuwatumbua,hii ni njia iliyompa umaarufu sana hasa kwa watu maskini. Watanzania wala hawajali kama matatizo yote haya yameletwa na CCM lkn wanahtaji mtu atakaeweza kuwasemea tena kwa ukali bila hofu,anaeonya na anaeonesha utatuzi.

Kwa sasa huna uwezo wa kimamlaka kutatua matatizo ya jamii,lakini unaweza kusababisha utatuzi na jamii ikaona wewe ndiye uliyeleta suluhu,katika ziara za kisiasa utakazofanya sasa jikite sana katika kueleza matatizo yaliyopo katika jamii, waseme watendaji wazembe, wanaojitahidi wape stahiki yao,lakini pia wambie wananchi wewe ukishika mamlaka utafanya lipi au utatatuaje hayo matatizo waliyonayo.

2. USITUMIE MUDA MWINGI KUMLAUMU MAGUFULI, HILI WATANZANIA WANALIJUA VIZURI KWA SASA.
Naomba niweke wazi tu katika hili. Kama nilvoeleza licha ya mapungufu mengi aliyokuwa nayo magufuri lakini mpaka sasa wananchi wa kawaida na hata baadhi ya watanzania wanamkumbuka magufuli hasa katika hatua zake nyingi za haraka alizokuwa anachukua kutatua changamoto za kiutendaji serikalini, kwa sasa hakuna kiongozi mwenye udhubutu huo,Raisi anaagiza lakin maagizo yake hayazingatiwi na watendaji.

Mfano tu Rais ameagiza mara nyingi kutocheleweshwa malipo ya makandarasi hasa wazawa ambayo hulimbikizwa na mwisho wa siku wanaanza kucharge interest za kuchelewehewa malipo lakini ukweli ni kwamba wakandarasi wa ndani na wazabuni sasa ni zaidi ya miezi takribani 10 hawajalipwa, ukitoa miradi ya TARURA labda na TANROAD na hazina wanajua hili na hakuna anaewajibika.

Watanzania wengi wanajua hukutendewa haki,ulionewa na halkuwa jambo jema kabisa kushambuliwa lakin kwa sasa wanawaza sana matatizo waliyonayo,wanataka kiongozi anayesema na wasaidizi kutii na kufanya,wanamkumbuka magufuri ndo mana wanamuona makonda kama anaweza kuvaa viatu vyake.

Watanzania wamechoka na siasa za uchawa, hawapendi kiongozi anayesema tu bila utekelezwaji, wewe ndie unaeweza kusema na kutenda, unaweza kusimamia ulichosema na kikatendeka,kwa sasa jikite katika kuwakusanya watanzania kwa pamoja bila kuajli itikadi zao na bila kujali walimpenda nani.

Hakika nakwambia Tundu Lissu, Watanzania wanakuamini usiwaangushe kuna kitu unawanyima.

3. USIKAE KIMYA SANA HASA WATANZANIA WANAPOKUMBWA NA JAMBO KATIKA JAMII.
Inawezekana kuna ile hali ya kusema ngoja wote tuongee lugha moja,lkn watanzania ni wasahaulifu sana, ikitokea tatzo walilonalo limeisha wanajisahaulisha. Mfano kwa sasa kunatatizo kubwa la kukatika kwa umeme na mgao wa maji baadhi ya maeneo.

Hakuna kiongozi yoyote wa serikali aliyeingilia kutatua hili swala, hata kauli za Viongozi wa kuu wa serikali zinaonesha zimekaa kisiasa na utani tu.mimi naamini nyakati kama hizi hustahili kuwa kimya, na hii itawafanya Viongozi waamke lkn watanzania wataona wewe ndo umewapa msaada. kiongozi uskate tamaa kuaddress matatizo lakini kila wakati ukiaddress jitahidi sana kuonesha mbadala wa kutatua.

Mhe.Tundu Lissu pamoja na wote mtakao wania nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkumbuke tu kwamba watanzania wengi ni maskini,mifumo ya uwajibikaji ni mibovu, elimu inayotolewa haijitoshelezi kuwezesha vijana kujiajiri lkn mifumo ya kusidia vijana kujiajiri ni mibovu pia, mifumo ya kufanya biashara si rafiki sana, Viongozi wengi wa juu serikalini ni mafisadi kwa kiwango kikubwa.

Mhe.Tundu lissu, umasikini ni mbaya sana,ni kama laana. Tafadhali ukiwa Raisi jitahidi kuinua kaya maskini, na vijana ikibidi kwa kutenga budget ya kuwalipa kila mwezi kiwango kizuri kitakachowainua kiuchumi, najua pia serikali ya CCM inafanya Hivyo lkn kinachofanyika ni uhuni na urasimu mkubwa sana, pesa zinatafunwa na haziwafikii walengwa no body cares in the system.

Mhe.Tundu lissu, naamin utakuwa Rais ajae. Najua unajua mengi sana katika jamii ya watanzania lkn naamn andiko langu litakusaidia walau kama si kufanya yote lkn utapata nafasi ya kutafakari upya.

View attachment 2864655
Una akili sana wewe jamaa!!! Hata Mimi nampenda sana Lissu ila kasoro ndo hizo ulizosema.

Labda niongeze jambo Moja tu,
Lissu ana msimamo usioyumba lakini yumo ndani ya chama Cha mtu ambaye ni king'ang'anizi sana. Mbowe hataki kufunikwa na Wala kukisolewa. Mbowe siyo mwaminifu na mtu wa deal mno. Ni rahisi sana Lissu kuuzwa!!

Ikimpendeza Mungu basi AMTWAE MBOWE ili Taifa lipone na Lissu aongoze nchi
 
Pamoja na ombi lako , lakini huwezi kutatua matatizo bila kuwataja waliyoyaleta na kuwatolea mfano , kwa mfano huwezi kuzungumzia Demokrasia ya Tanzania bila kumtaja Dikteta Magufuli , enzi za huyu mtu ndio viroba vilivyojaa maiti viliokotwa Baharini kila Wiki , baada ya yeye kuondoka na viroba vimepotea .

Huwezi kutatua changamoto kwa kuficha Ukweli
Huu ujinga ndio unaowapoteza. Sasa endeleeni kukomaa na visasi vyenu muone kama mtatoboa. Sijui kwanini Wachaga mna roho kama Hamas
 
Una akili sana wewe jamaa!!! Hata Mimi nampenda sana Lissu ila kasoro ndo hizo ulizosema.

Labda niongeze jambo Moja tu,
Lissu ana msimamo usioyumba lakini yumo ndani ya chama Cha mtu ambaye ni king'ang'anizi sana. Mbowe hataki kufunikwa na Wala kukisolewa. Mbowe siyo mwaminifu na mtu wa deal mno. Ni rahisi sana Lissu kuuzwa!!

Ikimpendeza Mungu basi AMTWAE MBOWE ili Taifa lipone na Lissu aongoze nchi
Mmeulizwa humu kwamba tajeni hizo dili za Mbowe wekeni na ushahidi lakini mnabwabwaja tu , Wajinga wakubwa nyie !
 
Kumbuka Magufuli alikuwa anashirikiana na akina Makonda , Bashiru Ally , Polepole , Kipilimba , Sirro , Kingai na wengine wengi ambao wako hai , Waliyoyafanya ni lazima yakemewe kwa kuwataja hadharani ili pasitokee tena uchafu ule , ni lazima watajwe hadharani ili Wananchi waliopotelewa na ndugu zao waelewe Wahusika halisi wa huu uharamia .

Shetani hapaswi kuhurumiwa na ndio maana anatajwa miaka yote
Sawa malaika umeeleweka
 
Una akili sana wewe jamaa!!! Hata Mimi nampenda sana Lissu ila kasoro ndo hizo ulizosema.

Labda niongeze jambo Moja tu,
Lissu ana msimamo usioyumba lakini yumo ndani ya chama Cha mtu ambaye ni king'ang'anizi sana. Mbowe hataki kufunikwa na Wala kukisolewa. Mbowe siyo mwaminifu na mtu wa deal mno. Ni rahisi sana Lissu kuuzwa!!

Ikimpendeza Mungu basi AMTWAE MBOWE ili Taifa lipone na Lissu aongoze nchi
Hivi ni kwanini watu wengi wanamuhusisha mh mbowe Kama msaliti pale chadema?

Hili jambo si baadhi ya watu wanalitengeneza mkuu kuleta mpasuo ndani ya chama ili waanze kumuhisi yeye ayupo pamoja nao na ni msaliti?

Nimeona wengi wakimhusisha mbowe na upande wa pili wa CCM.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom