CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
469
1,000
1599043679748.png

Jiji la Dar es Salaam ambayo ni ngome Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo linatarajiwa kusimama kwa siku tatu kupisha uzinduzi wa kihistoria wa mgombea Urais wa Chama hicho.

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Lissu atazindua Rasmi kampeni zake kuelekea Ikulu ya Magogoni na Chamwino kwa siku tatu mfululizo katika Jiji la DSM.

Viongozi wakuu wa chama hicho watashiriki uzinduzi huo wa kampeni wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe Katibu Mkuu John Mnyika na Wajumbe wote wa Kamati Kuu.

Taarifa kutoka ndani ya Chadema zinasema siku ya kwanza ya Uzinduzi itakuwa Ijumaa tarehe 28/8/20 katika viwanja vya Mbagala Zakiem; Siku ya Pili ya Uzinduzi itakuwa Jumamosi tarehe 29/8/20 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe na siku ya Tatu ya Uzinduzi itakuwa Jumapili tarehe 30/8/20 katika viwanja vya Tabata Segerea.

Tayari viongozi wa Kanda ya Pwani pamoja na mikoa ya kichama ya Ilala, Kinondoni na Temeke umeshaanza maandalizi makubwa ambapo inatarajiwa mikutano hiyo kuwa na umati mkubwa wa watu huku ikiongozwa kwa maandamano makubwa kabla na baada ya mikutano.

Itakuwa ni Mara ya kwanza kwa chama Cha siasa kuzindua kampeni kwa siku 3 mfululizo katika Jiji la Dar.

-----------------------------------------
Chadema kuzindua kampeni Kikanda

Baada ya mikutano mitatu ya uzinduzi katika Jiji la Dar es Salaam (Kanda ya Pwani), na Kanda ya Kaskazini (Arusha, Manyara, Tanga na Kilimanjaro), Kanda ya Viktoria (Mwanza, Geita na Kagera), Kanda ya Serengeti (Mara, Shinyanga na Simiyu), Kanda ya Magharibi (Tabora, Katavi na Kigoma), ratiba ya mikutano ya uzinduzi, ikiwemo siku ya leo Ijumaa, itaendelea kama ifuatavyo;

vii. Septemba 4, 2020, Uwanja wa Uhuru, jijini Dodoma, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

viii. Septemba 5, 2020, Uwanja wa Rwandanzovwe, jijini Mbeya, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

ix. Septemba 6, 2020, Uwanja wa Sabasaba, mjini Mtwara, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

x. Septemba 7, 2020, Uwanja wa Gombani, Chakechake, Pemba, kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana. Uwanja wa Maisara, Unguja, kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 12.00 jioni.

Tunatanguliza shukrani zetu, tukikuahidi ushirikiano na kutarajia hivyo kutoka kwako na chombo chako pia kwa ujumla katika kuimarisha demokrasia nchini kwetu ikiwa nguzo muhimu ya maendeleo ya Watanzania wote.

Kupitia taarifa hii, chombo chako kinakaribishwa na kualikwa rasmi kwenye Mkutano wa Uzinduzi a Kampeni za Mgombea Urais wa Chadema, Mhe. Tundu Lissu akiwa na Mgombea Mwenza, Mhe. Salum Mwalim Juma Mwalim, utakaofanyika Uwanja wa Uhuru Shule ya Msingi, jijini Dodoma.

Pamoja na salaam za Chama.

Wako katika ujenzi wa Taifa letu.

Tumaini Makene.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano.

=====


Bado siku 10 kuanzia leo 17 October 2020.
Ratiba ya Kampeni ya Mgombea uraisi (CHADEMA) Mh Tundu Lissu- hatua ya lala salama!

17/10/2020
1-Manyoni
2- Bahi
3- Kongwa
4- Dodoma mjini.

18/10/2020
1- Hanang
2- Mbulu
3- Karatu

19/10/2020
1-Simanjiro
2- Monduli
3- Longido
4- Arumeru
5- Hai
6- Moshi mjini

20/10/2020
1- Mwanga
2- Lushoto

21/10/2020
1-Korongwe
2- Muheza
3- Tanga Town

22/10/2020
1-Wete
2- Chakechake
3- Mkoa Magh
4- Pemba

23/10/2020
1- Lindi
2- Nachingwea
3- Newala
4- Nanyumbu

24/5/2020
1- Tunduru
2- Nyasa
3- Songea town

25/10/2020
1- Chemba
2- Singida
3- IKUNGI

26/10/2020
1- Same
2- Handeni
3- Pangani

27/10/2020
1- Dar es Salaam.

28/10/2020
Unachukua unaweka Tundu Lissu-!✌️✌️
Kisanduku cha mwisho kabisa chini!
# Ni YEYE-
# One Love!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom