Nategemea Lissu atashinda, ila Sina uhakika Kama atatangazwa. Vyovyote itakavyokua Lissu ataingia kwenye kumbukumbu Kama mgombea Urais alieshinda kwa mbinde. Lissu anagombea wakati Vyombo vya habari vinatishwa visitangaze habari zake hasa za kampeni, Lissu anafanyiwa kila aina ya hujuma.


Lissu hana hata bango moja barabarani lakini Bado anapata watu wengi kumsikiliza. Magazeti ambayo yangekua yanaripoti habari zake yalifungiwa mapema, kimkakati. Mfano Tanzania Daima.

Habari za Lissu huwezi kuzipata kwa undani kwenye TV na radio lakini watu wanajazana kwenye mikutano yake. Kitu Cha ajabu mgombea wa CCM, TBC wanarusha mambo yake tokea asubuhi lakini Lisu hapati fursa kama hiyo, lakini watu wanajaa kwenye mikutano yake.

Hata hivyo kubwa kuliko ni kwamba Lissu wa CHADEMA ndio mgombea Urais wa Tanzania ambae habari zake zinatawala sana kwenye mitandao ya kijamii. Hii yote inaonesha kuwa Lissu anakubalika zaidi na Vijana wasomi, wasomi na watu wenye ufahamu wa Juu wa TEHAMA na wenye kipato cha kati na kuendelea.

Pia Lissu habari zake zinatamba sana mitandaoni kwa sababu vyombo vingine vya kawaida vimepigwa biti. Hata hivyo mitandao ya kijamii ndio njia za mawasiliano na kupashana habari za kizazi kipya na tayari imekwisha ifunika Vyombo vya habari vya zamani.

Hitimisho: Tundu Lissu katawala media na kama magazeti Redio na tv zingekua huru kuripoti habari za Lissu Kuna mgombea asingesikika.

Magazeti yangeuza Sana habari za Lissu.
 
#Ni yeye , Tundu A Lissu ndio anauzika hapa Tanzania kwenye Chaguzi za mwaka huuu 2020 kuliko habari yoyote ile.
Farhia Middle, Leo ameanza na Habari pendwa ya Tundu Lissu,

Uzi tayari.
Ni yeye tu
IMG_20200915_201610.jpeg
 
Kabla ya huyu mwamba kurejea toka ulaya watu wengi walikuwa wamekata tamaa kabisa na walishafanya maamuzi kwamba huu mwaka hawatapiga kura.

Ila baada ya Lissu kurudi tu na kutangaza kwamba atapambana na jiwe watu wameonyesha imani kubwa kwake na sasa wameamua kwenda kupiga kura kwa wingi ili kuiondoa ccm madarakani.

Lissu ndio habari ya mjini kwa sasa. Ni Yeye2020
 
Kabla ya huyu mwamba kurejea toka ulaya watu wengi walikuwa wamekata tamaa kabisa na walishafanya maamuzi kwamba huu mwaka hawatapiga kura. Ila baada ya Lissu kurudi tu na kutangaza kwamba atapambana na jiwe watu wameonyesha imani kubwa kwake na sasa wameamua kwenda kupiga kura kwa wingi ili kuiondoa ccm madarakani.

Lissu ndio habari ya mjini kwa sasa. Ni Yeye2020
Unavyosema ni kweli ndg watu wengi nimewasikia wakisema Sasa watapiga kura.
 
Back
Top Bottom