Search results

  1. May Day

    Simba mnatolewa kwenye mstari na Ushabiki wa kijinga

    Kumezuka mtindo wa baadhi ya Mashabiki kujiona kwamba wao ndio Mashabiki wenye haki au bora au kindakindaki sana kuliko Mashabiki wengine. Kila jambo wao wanataka kuliongelea hata kama hawana chochote wanachofahamu kuhusina nalo. Ni ushabiki gani huu wa kushindwa kukubali timu kupoteza au...
  2. May Day

    Kuwe na muwakilishi wa BAKITA kwenye vituo vya Redio

    Hakuna maana yoyote ya kijinadi kama taifa la Kiswahili kama kwenye vyombo vyetu vya habari vinakuwa na makosa mengi kwenye matamshi ya Kiswahili. Au la basi mmoja wa Watangazaji anayekidhi vigezo apate ithibati ya Baraza. Walau kwa vile vituo vya rediuo vyenye Wasikilizaji wengi. Kazi yake...
  3. May Day

    Mashabiki Limbukeni na Wajuaji

    Siku chache zilizopitanilingia matatani baada ya kumtandia ngumi "mlevi" mmoja aliyekuwa anatukana hovyo matusi ya nguoni Wachezaji kwenye Luninga huku akijua fika kuwa hawamsikii bali anatusumbua tu sisi tuliopo pale kufuatilia mechi. Utashangaa Mtu anavyomkosoa Kocha mpaka unajiuliza hivi...
  4. May Day

    Fafanuzi za Oni sigala

    Mara kadhaa nimemsikia Mtaalamu wa Lugha Bw Oni Sigala akitoa ufafanuzi au maana ya maneno mbalimbali ya Kiswahili baada ya kuulizwa na Mtangazaji. Mimi sio Mtalamu wa lugha hii ila ni mfuatiliaji na mpenzi wa lugha na napenda kujifunza kila wakati. Hivi karibuni nimemsikia Mtaalamu huyu...
  5. May Day

    TFF hakikisheni ahadi ya pesa kwa Timu iambatane na wajibu

    Binaadamu ukimuahidi au akitarajia jambo anaweza asijali sana usalama wa wengine na wakati mwingine hata usalama wake mwenyewe. Teja anapohitaji pesa au chochote ulichonacho haoni shida kukuchoma kisu au bisbisi ya ubavu...kwake kwa wakati huo chenye thamani ni elfu mbili uliyonayo na sio uhai...
  6. May Day

    Wachezaji walipwe vizuri sambamba na elimu ya kifedha

    Nimekutana na hii hoja kuwa baadhi ya Wachezaji Wastaafu wanalalamika kuwa hawakuwa wanalipwa vizuri ndio maana maisha sasa yanawawia magumu. Bila kujiingiza kwenye sakata hili la Fei Toto na wala sina tatizo na Mtu kupigania haki yake ya kulipwa vizuri na ikiwezekana alipwe vizuri kwa kadri...
  7. May Day

    Baadhi ya maneno ya matusi ambayo jamii hutumia kwa kujua au bila kujua

    Kumekuwa na mtindo kwenye Jamii kugeuza maneno yenye mlengo wa ki matusi kuwa kama sentensi au misemo rasmi na halali kuitumia kwenye maongezi ya kawaida. Na kwa isivyo bahati kwa utitiri huu wa vyombo vya habari imekuwa ni rahisi sana kueneza misemo au mneno yenye ukakasi au matusi hata kama...
  8. May Day

    Kibu Dennis asaidiwe kisaikolojia

    Kuna ule usemi maarufu ya kwamba "Ukitaka kazi ya jeshi basi lazima ugangamale". Hivyo kwa mchezaji yeyote wa timu ndogo anapopambana na kuonesha makali ili afanikiwe kuwashawishi timu kubwa kumpa kazi, basi ajiandae pia kwa maisha ya upande wa pili wa shilingi, ambako kuna maisha ya presha...
  9. May Day

    Hili la Muharami Viongozi waSimba mpo sahihi

    Naona baadhi ya Watu ni kama wanalazimishwa kusikiliza au kuimbishwa mapambio yanayohanikiza kwamba Simba haikufanya sahihi kujiweka mbali na hili suala lililomkuta Bw Muharami. Na hata ukiwauliza ni kwa upande upi haswa wao wanaona Simba imekosea hawana hoja ya msingi zaidi ya kung'ang'ania tu...
  10. May Day

    Mkuu wa mkoa kuwaamuru Jamii moja kuondoka mkoani haijakaa sawa

    Leo asubuhi kwenye taarifa nimesikia ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Talak amewapa siku mbili Wafugaji walioingia mkoani hapo kuondoka. Kwa upande wangu sioni kama hii imekaa sawa, anachopaswa kujiuliza Kiongozi huyu ambaye ni Muwakilishi wa Raisi wa nchi hapo Mkoani kwake ni "waende wapi...
  11. May Day

    Hivi ilikuwaje Pepe Kale akaimba ule wimbo wa "Yanga Africa?".

    Anayejua hebu atujulishe kama je Pepe kale alifuatwa na Wadau akapewa dili?. Viongozi/kiongozi mmoja alimpa dili akamlipa?. au ni mapenzi yake binafsi kwa timu ya Yanga?
  12. May Day

    Salama pekee ya Mtu Mweusi kujikomboa ni kwa Siasa ya Ujamaa na kujitegemea

    Nimekaa na kuwaza sana kuhusu nafasi ya Mtu Mweusi kwenye ulimwengu huu wa kibabe na ni kwa hakika wala siioni nafasi yetu zaidi ya kuonekana tu kuwa tunafaa kubaki kama Jamii ya kuwatumikia hao Wakubwa. Mifumo yetu yote ya Elimu imeasisiwa kwao na Wengine huko nasi kubaki kama wapokeaji...
  13. May Day

    Napendekeza utaratibu wa points kwenye soka urekebishwe

    Ili kuvutia ufungaji wa magoli mengi kwenye soka na kuongeza burudani, basi FIFA waanzishe utaratibu pale ambapo timu moja itafanikiwa kufunga zaidi ya magoli matatu bila basi waongezewe pointi moja zaidi. Kwamba iwapo timu itafunga bao tatu bila Mpinzani kufunga goli basi badala ya point tatu...
  14. May Day

    Kuwepo utaratibu kuwalinda watoto viwanjani wakati wa mechi

    Mara kadhaa nimeshuhudia watoto wadogo walioambatana na wazazi au walezi wao uwanjani wakiwa katikati ya watu huku akiwa amezungukwa na ile midude wanayopuliza almaarufu kama vuvuzela. Nilikuwa sijui kero ya haya madude mpaka wakati fulani Bwana mmoja alikuja nalo mahali nilipokuwa nafuatilia...
  15. May Day

    Tuwekeze kwenye Teknolojia kutafuta suluhu ya Maji

    Tengeneza picha umeamka siku moja na kujikuta kati kati ya jangwa saa sita mchana jua lipo utosini, ukizunguka pande zote huoni Mmea wala Mbu zaidi ya miale (mirage) inayotokana na kuakisiwa kwa jua juu ya uso wa Dunia. Hicho ndio kifo, na iwapo ghafla mbele yako itafumuka chemu chemu ya maji...
  16. May Day

    Chonde chonde Viongozi Simba msimtwishe Mgunda zigo zito, mtamuumiza

    Kutokana na kuwa Simba wanaendelea kupata matokeo mazuri kumekuwa na kelele kila kona kutoka kwa Mashabiki wakitaka Mgunda apewe timu kamili kama Kocha Mkuu. Na Viongozi wa Simba ni kama vile wamekaa wakisubiri kama vile wanasikilizia. Nadhani hili litawagharimu Simba, huu mchezo wa...
  17. May Day

    Kuendelea kwa haya matukio. Kanisa Mjitathmini.

    Kiukweli inatamausha sana kusikia haya matukio ya mara kwa mara yakijirudia ya unyanyaswaji Watoto na Watu ambao ilitarajiwa kuaminiwa na Jamii. Hainiingii akilini ni kwa vipi Taasisi yenye Wasomi kushindwa kuweka mifumo ya kudhibitiana wao kwa wao...hivi mnashindwa vipi kutambua Mwenendo wa...
  18. May Day

    Sio kila fursa ni fursa, tuwe makini kuchuja jamani

    Leo asubuhi kupitia redioni nimesikia wakisoma moja ya Gazeti lenye kichwa cha habari kinachosema, vifuu, machicha, ungawa mbao n.k vinahitajika huko kwa wenzetu. Sidhani kama hii ni fursa sahihi, kwa nini tusifikirie kwenye kuuza bidhaa tayari? hivi kweli bidhaa za nishati zinaweza kukosa soko...
  19. May Day

    Shule ziwe na "madarasa kando" kwa ajili ya Wanafunzi Wabunifu

    Dunia inaenda kasi sana na hakuna wa kumsubiri mwingine eti ndio tuende sawa. Ni dhahiri kuwa Mataifa yaliyoshika hatamu za dunia hii wao wamewekeza sana kwenye sayansi na teknolojia, gunduzi mbalimbali zinazofanywa na Wananchi wao ndio zinazogeuzwa bidhaa na wengine tuliobaki tunakuwa Wateja...
  20. May Day

    Mashabiki wa Tanzania ni wakosa subira wakubwa.

    Kwanza niweke rekodi sawa. Tanzania hakuna Wapenzi wengi wa Mpira wa Miguu kama wanavyoamini wengi wetu, bali kuna Mashabiki wengi wa Simba na wa Yanga. Kwa isivyo bahati mashabiki wetu hawa wanachowazidi Mashabiki wa sehemu nyingine Duniani ni namna hata wanavyoshabikia hizi timu zao. Leo hii...
Back
Top Bottom