Baadhi ya maneno ya matusi ambayo jamii hutumia kwa kujua au bila kujua

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Kumekuwa na mtindo kwenye Jamii kugeuza maneno yenye mlengo wa ki matusi kuwa kama sentensi au misemo rasmi na halali kuitumia kwenye maongezi ya kawaida.

Na kwa isivyo bahati kwa utitiri huu wa vyombo vya habari imekuwa ni rahisi sana kueneza misemo au mneno yenye ukakasi au matusi hata kama hakuna ulazima wa kuyatumia.

BAADHI YA MANENO HAYO:-
1)"Pale kulipoungua shoka mpini ukabakia"...sidhani kama kunahitajika maelezo marefu kuelezea sentesi hii maana inajieleza vyema. ni muhimu kwa mtumiaji wa msemo huu kujiuliza ni nini maana ya msemo huu? ni wapi huko kulikoungua shoka mpini ukabaki?.

NIMETUMIA MCHORO KUFAFANUA MSEMO WA "KULIKOUNGUA SHOKA MPINI UKABAKI".

Shoka 01.png

Shoka na Mpini wake.

Shoka 02.png

Mpini baada ya kupoteza shoka.

Picha ya Mpini baada ya kupoteza shoka lake, ambako Jamii wanatafsiri kama baada ya kukita hapo shoka likaungua na kuteketea, hivyo hilo kovu ndiko kulikoungulia hilo shoka na 'Mtema Kuni' kabaki na mpini wake.

2)Msemo mwingine ni ule wa "Sauti ya kumtoa Nyoka pangoni"...jiulize ni Nyoka gani anayetolewa Pangoni kwa sauti nyororo? msemo huu hulenga zaidi kwa sauti ya Mwanamke na mwenye pango lenye Nyoka ni Mwanaume.

3)Neno kama "Kudadadeki"....hili ni neno mbadala wa lile tusi maarufu la Mama, hivyo sioni kwa nini Mtu ulazimeke kulitumia kama huna nia ya kutukana.

4)Kuna misemo kama "kuingia choo cha kike" na sasa hivi kuna huu wa "atalowa au amelowa" n.k.
 
View attachment 2456579
Shoka na Mpini wake.

View attachment 2456577

Kwenye shoka hapo umechemka.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom