Salama pekee ya Mtu Mweusi kujikomboa ni kwa Siasa ya Ujamaa na kujitegemea

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Nimekaa na kuwaza sana kuhusu nafasi ya Mtu Mweusi kwenye ulimwengu huu wa kibabe na ni kwa hakika wala siioni nafasi yetu zaidi ya kuonekana tu kuwa tunafaa kubaki kama Jamii ya kuwatumikia hao Wakubwa.

Mifumo yetu yote ya Elimu imeasisiwa kwao na Wengine huko nasi kubaki kama wapokeaji. Mzungu ndiye wa kutuambia uking'atwa na Mbu unapata Malaria, au atuambie kuhusu Isack Newton, Easten, Archimedes n.k.

Ila linapokuja suala la Mweusi tutaambiwa kuhusu Kinjekitile Ngwale aliyekuwa anaziamuru risasi kuwa maji, au Mkwawa aliyeuwawa na Wajerumani.

Hivi kweli tunaamini kila wanachoongea hao walioendelea huko mbele ya macho yetu ndicho hicho wanachoongea hata wakiwa peke yao? la hasha.

Weusi tumekuwa Watu wa kulia lia tu kwa kila jambo na kuomba kuonewa huruma. Hivi kwa mazingira hayo wewe una nafasi gani mbele ya Watu unaowalilia wakupe fidia ya kutunza Misitu na ukae pembeni usubiri wakuonee huruma wakupe?.

Akili zetu zote zipo kwenye pesa pesa pesa ambazo hata hatuna asili nazo. Na hapo Viongozi wetu tunajua kitakachoendelea wakipata hayo mapesa, ni kugawana wao na familia zao kwanza kisha kidogo zinazobaki ndio zitajengea Zahanati zisizo hata na Wahudumu..

Hivi unadhani hata hao Watoto wa Viongozi wanosomeshwa kwenye Mashule ya Mamilioni ya pesa watakuja kuisaidia Nchi baadae?. la hasha, sanasana ni kutumia hizo elimu kutafuta madaraka na malipo mazuri.

Tupo karne ya 21 Watu weusi bado tumalimbukeni wakubwa wa pesa kuliko maendeleo yetu wenyewe au ya mazingira tunayoishi. Angalia hata Weusi wenzetu wanaoishi huko huko, wakipata hayo mabilioni wala hawana cha kufanyia zaidi ya kununua Magari, Majumba, Vidani vya thamani kubwa mpaka hizo pesa zitakapoisha.

Tunahitaji maisha tofauti kabisa kama kweli tunatamani kuona tuna nafasi sawa kwenye ulimwengu huu. tunahitaji kuishi na kubaki kama Waafrika zaidi, tunahitaji kusahau kuhusu pesa, tunahitaji kuachana na bidhaa zote zisizo na maana wala ulazima kwa maisha yetu, tuandae na kutumia tunavyovimudu au tunavyoandaa wenyewe.

Tunahitaji kuchagua muelekeo mmoja, tufuge na kulima kwelikweli ,tulime mpaka Dunia ifike mahali ione tunaihitaji Africa ili tusife njaa.

Tukae chini tujiulize tunahitaji hizo Simu za nini, Televisheni na cheni za dhahabu za kazi gani?. Hatuhitaji Matajiri hawa wanaotutengenezea Ice cream na soda na vinywaji vya kusisimua mwili(energy drinks). Africa kusiwe na Tajiri ambao ndio chanzo kikubwa cha Mgawanyiko na kubaguana wenyewe kwa wenyewe, kusiwe na Masikini, asilimia 98 ya Mahitaji tuandae Wenyewe, tusichonacho basi tuachane nacho mpaka pale tutakapoweza kuwa nacho.

Kusanya Vijana wote wa Tanzania wanaoshabikia Ubepari dhidi ya Ujamaa uone hata kama wana hoja ya msingi. Hawana hoja yoyote ya msingi zaidi ya kutamani tu kumiliki mali na pesa dhidi ya Wenzao, kila mmoja anatamani kumuona mwenzake ni dhalili dhidi yake, ajisikie ufahari anapoendesha Range Rover ya milioni mia tatu kati kati ya kundi la Watu wasio na uhakika wa mlo wa siku. Tunatumia Elimu wanazotuaminisha wao kisha tunapeana madaraja ya kuitana Injinia, Mhasibu, Dokta. Lawyer n.k na kujitenga na wengine kwa Kigezo cha usomi hivyo tunajipa stahili ya kulipana vizuri, kula vizuri, kulala pazuri n.k, kana kwamba wengine wote wanaobaki wao ni Mbuzi tu.

Wanachokitamani Vijana wetu wa leo na kutukana Siasa za Ujamaa na Kujitegemea na ndicho kinachoendelea Ulimwenguni kote huko. kila kukicha Matajiri wanatupatia Mabilioni ya pesa bila kuwafanyia chochote...hivi unafikiri ni lini watakuwa tayari kuishi bila kuombwa ombwa pesa? haitotokea mpaka kiama, hivyo tutabaki dhalili daima kwa sababu hatuko tayari kuishi bila choclate na coca cola zao.

Wanaoshangilia haya ni wale tu wanaofaidika nayo, ambao ni asilimia ndogo tu ukilinganisha na wengi wanaomia na wala hawana nafasi ya kusema au kushauri. Watu wanawaibia wenzao kwa kuwa tu wamejipa dhamana, Mtu anajiona sawa kujenga Ghorofa la milioni mia tatu kati kati ya Masikini aliowaibia na kujiona ana akili kuliko wao ndio maana yupo hapo. alafu utegemee Mtu huyo achukie Ubepari dhidi ya Ujamaa?.

Tuishi kama Wakulima, Wafugaji, Wahunzi n.k. Wakulima watapata Nyama kutoka kwa Wafugaji na Wafugaji watapata Mchele na Unga kutoka kwa Wakulima. Watu watembee, watumie Wanyama kazi kulima, kusafiri na kubeba mizigo mpaka pale akili zitakapoona haja ya kuwa na mashine za kuwasaidia. Ipo haja tuishi kana kwamba hakuna wa kutusaidia huko kwingine.

Natamani itokee Pigo moja na kuangamiza asilimia 99 ya Vijana wa nchi hii, wabaki Wazee Wachache na Watoto wote wasiozidi miaka mitano wabaki, alafu Mungu amrudishe Mwalimu akiwa na miaka kumi na saba tu ili tuanze upya kwa Siasa ya Ujamaa na kujitegemea. Nina uhakika baada ya miaka hamsini baadae tutakuwa na Nchi moja imara sana na inayoheshimika.
 
Nilikaa na kuwaza sana kuhusu nafasi ya Mtu Mweusi kwenye ulimwengu huu wa kibabe na ni hakika siioni nafasi yetu zaidi ya kuonekana kuwa tunafaa tu kubaki kama wa kuwatumikia Wakubwa.

Mifumo yetu yote ya Elimu imeasisiwa kwao na Wengine huko nasi kubaki kama wapokeaji. Mzungu ndiye wa kutuambia uking'atwa na Mbu unapata Malaria, au atuambie kuhusu Isack Newton, Easten, Archimedes n.k.

Ila linapokuja swala la Mweusi tutaambiwa kuhusu Kinjekitile Ngwale aliyekuwa anaziamuru risasi kuwa maji, au Mkwawa aliyeuwawa na Wajerumani.

Hivi kweli tunaamini kila wanachoongea hao walioendelea huko mbele ya macho yetu ndicho wanachoongea hata wakiwa peke yao? la hasha.

Weusi tumekuwa Watu wa kulia lia tu kwa kila jambo na kuomba kuonewa huruma. Hivi kwa mazingira hayo wewe una nafasi gani mbele ya Watu unaowalilia wakupe fidia ya kutunza Misitu na ukae pembeni usubiri wakuonee huruma wakupe.

Akili zetu zote zipo kwenye pesa pesa pesa ambazo hata hatuna asili nazo. Na hapo Viongozi wetu tunajua kitakachoendelea wakipata hayo mapesa.

Tupo karne ya 21 Watu weusi bado ni tumalimbukeni wakubwa wa pesa kuliko maendeleo yetu wenyewe au ya mazingira tunayoishi. Angalia hata Weusi wenzetu wanaoishi huko huko, wakipata hayo mabilioni wala hawana cha kufanyia zaidi ya kununua Magari, Majumba, Vidani vya thamani kubwa mpaka hizo pesa zitakapoisha.

Tunahitaji maisha tofauti kabisa kama kweli tunatamani kuona tuna nafasi sawa kwenye ulimwengu huu. tunahitaji kuishi na kubaki kama Waafrika zaidi, tunahitaji kusahau kuhusu pesa, tunahitaji kuachana na bidhaa zote zisizo na maana wala ulazima kwa maisha yetu, tuandae n kutumia tunavyoandaa wenyewe.

Tunahitaji kuchagua muelekeo mmoja, tufuge na tuwe Wakulima kwelikweli tulime kweli walau Dunia ifike mahali ione umuhimu wa kuwa na Africa ili wasife njaa.

Tukae chini tujiulize tunahitaji hizo Simu za nini, Televisheni na cheni za dhahabu za kazi gani?. Hatuhitaji Matajiri wa kututengenezea Ice cream na soda na vinywaji vya kusisimua mwili(energy drinks). Africa kusiwe na Tajiri ambao ndio chanzo kikubwa cha Mgawanyo na kubaguana wenyewe kwa wenyewe, kusiwe na Masikini, asilimia 98 ya Mahitaji tuandae Wenyewe tusichonacho basi tuachane nacho mapaka pale tutakapoweza kuwa nacho.

Kusanya Vijana wote wa Tanzania wanaoshabikia Ubepari dhidi ya Ujamaa uone hata kama wana hija ya msingi, hawana hoja yoyote zaidi ya kutamani tu kumiliki mali na pesa dhidi ya Wenzao, kila mmoja anatamani kumuona mwenzake dhalili. Tunatumia Elimu wanazotuaminisha wao kisha tunapeana madaraja ya kuitana Injinia, Mhasibu, Dokta na kujitenga na wengine kwa Kigezo cha usomi hivyo anastahili kula vizuri, kulala pazuri kana kwamba wanaobaki wao ni Mbuzi tu.

Wanachokitamani Vijana wetu wa leo na kutukana Siasa za Kijamaa ndicho kinachoendelea Ulimwenguni huko. kila kukicha Matajiri wanatupatia Mabilioni...hivi unafikiri ni lini watakuwa tayari kutokuombwa pesa? haitotokea mpaka kiama, tutabaki dhalili daima kwa sababu hatuko tayari kuishi bila choclate.

Wanaoshangilia haya ni wale tu wanaofaidika nayo, ambao ni asilimia ndogo tu ukilinganisha na wanaomia na wala hawana nafasi ya kusema au kushauri. Watu wawaibia wenzao kwa kuwa tu wamejipa dhamana, Mtu anajiona sawa kujenga Ghorofa la milioni mia tatu kati kati ya Masikini aliowaibia na kujiona ana akili kuliko wao ndio maana yupo hapo. alafu utegemee Mtu huyo achukie Ubepari dhidi ya Ujamaa?.

Tuishi Wakulima, Wafugaji, Wahunzi n.k, Wakulima watapata Nyama kutoka kutoka Mfugaji na Mfugaji atapata Mchele na Unga kutoka kwa Mfugaji. Watu watembee, watumie Wanyama kazi mpaka pale akili zitakapoona haja ya kuwa na mashine za kuwasaidia.

Natamani itokee Pigo moja na kuangamiza asilimia 99 ya Vijana, wabaki Wazee Wachache na Watoto wote wasiozidi miaka mitano wabaki, alafu Mungu amrudishe Mwalimu akiwa na miaka kumi na saba hivi ili tuanze upya kwa Siasa ya Ujamaa na kujitegemea. Nina uhakika mika hamsini baadae tutakuwa na Nchi.

Ww utakuwa ni mzee lazima ndio maana unahusudu ujamaa. Ujamaa ulitufanya tuvae viraka, sasa sijui ni ujamaa gani unaoongelea boss.
 
Ujamaa ulio wafanya watanganyika kuvaa kaniki uku bidhaa Kama sukari,sabuni,unga kuwa bidhaa adimu naza anasa hapana kwa kweli.

Hivi Watanzania ule mkanda ambao Mwl,l.Nyerere alisema watu wafunge kwa miezi 18 mliifungua lini?
 
Tofauti ya kiongozi wa kijamaa na mfalme ni kwamba kiongozi wa kijamaa anasema yeye si mfalme lakini dikteta/dhalimu kuliko mfalme,mungu mtu na mtakatifu
 
Ww utakuwa ni mzee lazima ndio maana unahusudu ujamaa. Ujamaa ulitufanya tuvae viraka, sasa sijui ni ujamaa gani unaoongelea boss.
Ndio huo huo, tuvae viraka mpaka tujue kazi ya Pamba na ngozi na kujishonea nguo zetu wenyewe.
 
Ujamaa ulio wafanya watanganyika kuvaa kaniki uku bidhaa Kama sukari,sabuni,unga kuwa bidhaa adimu naza anasa hapana kwa kweli.

Hivi Watanzania ule mkanda ambao Mwl,l.Nyerere alisema watu wafunge kwa miezi 18 mliifungua lini?
Ndio exactly ninachomaanisha mana kinachoendelea sasa hivi ni kuomba omba tu kama wasiojiweza.

Mkifuga Vizuri na Kulima Vizuri mnahitaji nini zaidi hata kama Mzungu hatokuletea Coca cola na Colgate?.
 
Nimekaa na kuwaza sana kuhusu nafasi ya Mtu Mweusi kwenye ulimwengu huu wa kibabe na ni kwa hakika wala siioni nafasi yetu zaidi ya kuonekana tu kuwa tunafaa kubaki kama Jamii ya kuwatumikia hao Wakubwa.

Mifumo yetu yote ya Elimu imeasisiwa kwao na Wengine huko nasi kubaki kama wapokeaji. Mzungu ndiye wa kutuambia uking'atwa na Mbu unapata Malaria, au atuambie kuhusu Isack Newton, Easten, Archimedes n.k.

Ila linapokuja suala la Mweusi tutaambiwa kuhusu Kinjekitile Ngwale aliyekuwa anaziamuru risasi kuwa maji, au Mkwawa aliyeuwawa na Wajerumani.

Hivi kweli tunaamini kila wanachoongea hao walioendelea huko mbele ya macho yetu ndicho hicho wanachoongea hata wakiwa peke yao? la hasha.

Weusi tumekuwa Watu wa kulia lia tu kwa kila jambo na kuomba kuonewa huruma. Hivi kwa mazingira hayo wewe una nafasi gani mbele ya Watu unaowalilia wakupe fidia ya kutunza Misitu na ukae pembeni usubiri wakuonee huruma wakupe?.

Akili zetu zote zipo kwenye pesa pesa pesa ambazo hata hatuna asili nazo. Na hapo Viongozi wetu tunajua kitakachoendelea wakipata hayo mapesa, ni kugawana wao na familia zao kwanza kisha kidogo zinazobaki ndio zitajengea Zahanati zisizo hata na Wahudumu..

Hivi unadhani hata hao Watoto wa Viongozi wanosomeshwa kwenye Mashule ya Mamilioni ya pesa watakuja kuisaidia Nchi baadae?. la hasha, sanasana ni kutumia hizo elimu kutafuta madaraka na malipo mazuri.

Tupo karne ya 21 Watu weusi bado ni tumalimbukeni wakubwa wa pesa kuliko maendeleo yetu wenyewe au ya mazingira tunayoishi. Angalia hata Weusi wenzetu wanaoishi huko huko, wakipata hayo mabilioni wala hawana cha kufanyia zaidi ya kununua Magari, Majumba, Vidani vya thamani kubwa mpaka hizo pesa zitakapoisha.

Tunahitaji maisha tofauti kabisa kama kweli tunatamani kuona tuna nafasi sawa kwenye ulimwengu huu. tunahitaji kuishi na kubaki kama Waafrika zaidi, tunahitaji kusahau kuhusu pesa, tunahitaji kuachana na bidhaa zote zisizo na maana wala ulazima kwa maisha yetu, tuandae na kutumia tunavyovimudu au tunavyoandaa wenyewe.

Tunahitaji kuchagua muelekeo mmoja, tufuge na kulima kwelikweli ,tulime mpaka Dunia ifike mahali ione tunaihitaji Africa ili tusife njaa.

Tukae chini tujiulize tunahitaji hizo Simu za nini, Televisheni na cheni za dhahabu za kazi gani?. Hatuhitaji Matajiri wa wanaotutengenezea Ice cream na soda na vinywaji vya kusisimua mwili(energy drinks). Africa kusiwe na Tajiri ambao ndio chanzo kikubwa cha Mgawanyiko na kubaguana wenyewe kwa wenyewe, kusiwe na Masikini, asilimia 98 ya Mahitaji tuandae Wenyewe, tusichonacho basi tuachane nacho mapaka pale tutakapoweza kuwa nacho.

Kusanya Vijana wote wa Tanzania wanaoshabikia Ubepari dhidi ya Ujamaa uone hata kama wana hoja ya msingi. Hawana hoja yoyote ya msingi zaidi ya kutamani tu kumiliki mali na pesa dhidi ya Wenzao, kila mmoja anatamani kumuona mwenzake ni dhalili dhidi yake, ajisikie ufahari anapoendesha Range Rover ya milioni mia tatu kati kati ya kundi la Watu wasio na uhakika wa mlo wa siku. Tunatumia Elimu wanazotuaminisha wao kisha tunapeana madaraja ya kuitana Injinia, Mhasibu, Dokta. Lawyer n.k na kujitenga na wengine kwa Kigezo cha usomi hivyo tunajipa stahili ya kulipwa vizuri, kula vizuri, kulala pazuri n.k, kana kwamba wengine wote wanaobaki wao ni Mbuzi tu.

Wanachokitamani Vijana wetu wa leo na kutukana Siasa za Ujamaa na Kujitegemea na ndicho kinachoendelea Ulimwenguni kote huko. kila kukicha Matajiri wanatupatia Mabilioni ya pesa bila kuwafanyia chochote...hivi unafikiri ni lini watakuwa tayari kuishi bila kuombwa ombwa pesa? haitotokea mpaka kiama, hivyo tutabaki dhalili daima kwa sababu hatuko tayari kuishi bila choclate na coca cola zao.

Wanaoshangilia haya ni wale tu wanaofaidika nayo, ambao ni asilimia ndogo tu ukilinganisha na wengi wanaomia na wala hawana nafasi ya kusema au kushauri. Watu wanawaibia wenzao kwa kuwa tu wamejipa dhamana, Mtu anajiona sawa kujenga Ghorofa la milioni mia tatu kati kati ya Masikini aliowaibia na kujiona ana akili kuliko wao ndio maana yupo hapo. alafu utegemee Mtu huyo achukie Ubepari dhidi ya Ujamaa?.

Tuishi kama Wakulima, Wafugaji, Wahunzi n.k. Wakulima watapata Nyama kutoka Wafugaji na Wafugaji watapata Mchele na Unga kutoka kwa Wakulima. Watu watembee, watumie Wanyama kazi kulima, kusafiri na kubeba mizigo mpaka pale akili zitakapoona haja ya kuwa na mashine za kuwasaidia. Ipo haja tuishi kana kwamba hakuna wa kutusaidia huko kwingine.

Natamani itokee Pigo moja na kuangamiza asilimia 99 ya Vijana wa nchi hii, wabaki Wazee Wachache na Watoto wote wasiozidi miaka mitano wabaki, alafu Mungu amrudishe Mwalimu akiwa na miaka kumi na saba tu ili tuanze upya kwa Siasa ya Ujamaa na kujitegemea. Nina uhakika baada ya miaka hamsini baadae tutakuwa na Nchi.
Kuna utandu na uchawi uliopandikizwa vichwani mwa walio wengi, huo ndio utakaofanya hoja yako kupingwa na wengi sana.
Wameaminishwa UJAMAA HAUWEZEKANI, nao wamemeza imani hiyo kikamilifu na wako radhi kuiitoa popote, tena wakijivunia Fikra zao hasi juu ya Ujamaa.

Nakazia: Nje ya Ujamaa, kamwe haitatokea siku ambayo MTU mweusi atabeba hadhi sawa na white races kiustawi wa aina yoyote.
Nje ya Ujamaa sisi ni Watumwa wa Kudumu milele na milele.
 
Ndio huo huo, tuvae viraka mpaka tujue kazi ya Pamba na ngozi na kujishonea nguo zetu wenyewe.
Hongera Mkuu, Fikra zako ni Kuu sana, hakikisha zinabebwa na watoto wako.
IPO Siku Tutaimba Wimbo mmoja, haijalishi itachukua karne ngapi.
 
Ujamaa ni utopolo mmoja hiv
Ukitaka kujua ujamaa ni upuuzi na ni kivuli cha udikteta tazama russia na north korea

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
Sidhani kama ujamaa wote unatekelezwa kwa aina moja.

Kama Russia na Korea walifeli sio lazima tuwatumie kama mfano.

Na hilo haliondoi msingi mkuu wa ujamaa.
 
Kuna utandu na uchawi uliopandikizwa vichwani mwa walio wengi, huo ndio utakaofanya hoja yako kupingwa na wengi sana.
Wameaminishwa UJAMAA HAUWEZEKANI, nao wamemeza imani hiyo kikamilifu na wako radhi kuiitoa popote, tena wakijivunia Fikra zao hasi juu ya Ujamaa.

Nakazia: Nje ya Ujamaa, kamwe haitatokea siku ambayo MTU mweusi atabeba hadhi sawa na white races kiustawi wa aina yoyote.
Nje ya Ujamaa sisi ni Watumwa wa Kudumu milele na milele.
Tuna Vijana wa ajabu sana Nchi hii Mkuu.

Mtu ukimwambia akwambie ubaya wa Ujamaa wala hatoi hoja za msingi zaidi ya kutukana na kutoa mifano ya walioshindwa.
 
Nimekaa na kuwaza sana kuhusu nafasi ya Mtu Mweusi kwenye ulimwengu huu wa kibabe na ni kwa hakika wala siioni nafasi yetu zaidi ya kuonekana tu kuwa tunafaa kubaki kama Jamii ya kuwatumikia hao Wakubwa.

Mifumo yetu yote ya Elimu imeasisiwa kwao na Wengine huko nasi kubaki kama wapokeaji. Mzungu ndiye wa kutuambia uking'atwa na Mbu unapata Malaria, au atuambie kuhusu Isack Newton, Easten, Archimedes n.k.

Ila linapokuja suala la Mweusi tutaambiwa kuhusu Kinjekitile Ngwale aliyekuwa anaziamuru risasi kuwa maji, au Mkwawa aliyeuwawa na Wajerumani.

Hivi kweli tunaamini kila wanachoongea hao walioendelea huko mbele ya macho yetu ndicho hicho wanachoongea hata wakiwa peke yao? la hasha.

Weusi tumekuwa Watu wa kulia lia tu kwa kila jambo na kuomba kuonewa huruma. Hivi kwa mazingira hayo wewe una nafasi gani mbele ya Watu unaowalilia wakupe fidia ya kutunza Misitu na ukae pembeni usubiri wakuonee huruma wakupe?.

Akili zetu zote zipo kwenye pesa pesa pesa ambazo hata hatuna asili nazo. Na hapo Viongozi wetu tunajua kitakachoendelea wakipata hayo mapesa, ni kugawana wao na familia zao kwanza kisha kidogo zinazobaki ndio zitajengea Zahanati zisizo hata na Wahudumu..

Hivi unadhani hata hao Watoto wa Viongozi wanosomeshwa kwenye Mashule ya Mamilioni ya pesa watakuja kuisaidia Nchi baadae?. la hasha, sanasana ni kutumia hizo elimu kutafuta madaraka na malipo mazuri.

Tupo karne ya 21 Watu weusi bado ni tumalimbukeni wakubwa wa pesa kuliko maendeleo yetu wenyewe au ya mazingira tunayoishi. Angalia hata Weusi wenzetu wanaoishi huko huko, wakipata hayo mabilioni wala hawana cha kufanyia zaidi ya kununua Magari, Majumba, Vidani vya thamani kubwa mpaka hizo pesa zitakapoisha.

Tunahitaji maisha tofauti kabisa kama kweli tunatamani kuona tuna nafasi sawa kwenye ulimwengu huu. tunahitaji kuishi na kubaki kama Waafrika zaidi, tunahitaji kusahau kuhusu pesa, tunahitaji kuachana na bidhaa zote zisizo na maana wala ulazima kwa maisha yetu, tuandae na kutumia tunavyovimudu au tunavyoandaa wenyewe.

Tunahitaji kuchagua muelekeo mmoja, tufuge na kulima kwelikweli ,tulime mpaka Dunia ifike mahali ione tunaihitaji Africa ili tusife njaa.

Tukae chini tujiulize tunahitaji hizo Simu za nini, Televisheni na cheni za dhahabu za kazi gani?. Hatuhitaji Matajiri wa wanaotutengenezea Ice cream na soda na vinywaji vya kusisimua mwili(energy drinks). Africa kusiwe na Tajiri ambao ndio chanzo kikubwa cha Mgawanyiko na kubaguana wenyewe kwa wenyewe, kusiwe na Masikini, asilimia 98 ya Mahitaji tuandae Wenyewe, tusichonacho basi tuachane nacho mapaka pale tutakapoweza kuwa nacho.

Kusanya Vijana wote wa Tanzania wanaoshabikia Ubepari dhidi ya Ujamaa uone hata kama wana hoja ya msingi. Hawana hoja yoyote ya msingi zaidi ya kutamani tu kumiliki mali na pesa dhidi ya Wenzao, kila mmoja anatamani kumuona mwenzake ni dhalili dhidi yake, ajisikie ufahari anapoendesha Range Rover ya milioni mia tatu kati kati ya kundi la Watu wasio na uhakika wa mlo wa siku. Tunatumia Elimu wanazotuaminisha wao kisha tunapeana madaraja ya kuitana Injinia, Mhasibu, Dokta. Lawyer n.k na kujitenga na wengine kwa Kigezo cha usomi hivyo tunajipa stahili ya kulipwa vizuri, kula vizuri, kulala pazuri n.k, kana kwamba wengine wote wanaobaki wao ni Mbuzi tu.

Wanachokitamani Vijana wetu wa leo na kutukana Siasa za Ujamaa na Kujitegemea na ndicho kinachoendelea Ulimwenguni kote huko. kila kukicha Matajiri wanatupatia Mabilioni ya pesa bila kuwafanyia chochote...hivi unafikiri ni lini watakuwa tayari kuishi bila kuombwa ombwa pesa? haitotokea mpaka kiama, hivyo tutabaki dhalili daima kwa sababu hatuko tayari kuishi bila choclate na coca cola zao.

Wanaoshangilia haya ni wale tu wanaofaidika nayo, ambao ni asilimia ndogo tu ukilinganisha na wengi wanaomia na wala hawana nafasi ya kusema au kushauri. Watu wanawaibia wenzao kwa kuwa tu wamejipa dhamana, Mtu anajiona sawa kujenga Ghorofa la milioni mia tatu kati kati ya Masikini aliowaibia na kujiona ana akili kuliko wao ndio maana yupo hapo. alafu utegemee Mtu huyo achukie Ubepari dhidi ya Ujamaa?.

Tuishi kama Wakulima, Wafugaji, Wahunzi n.k. Wakulima watapata Nyama kutoka Wafugaji na Wafugaji watapata Mchele na Unga kutoka kwa Wakulima. Watu watembee, watumie Wanyama kazi kulima, kusafiri na kubeba mizigo mpaka pale akili zitakapoona haja ya kuwa na mashine za kuwasaidia. Ipo haja tuishi kana kwamba hakuna wa kutusaidia huko kwingine.

Natamani itokee Pigo moja na kuangamiza asilimia 99 ya Vijana wa nchi hii, wabaki Wazee Wachache na Watoto wote wasiozidi miaka mitano wabaki, alafu Mungu amrudishe Mwalimu akiwa na miaka kumi na saba tu ili tuanze upya kwa Siasa ya Ujamaa na kujitegemea. Nina uhakika baada ya miaka hamsini baadae tutakuwa na Nchi.

Asante sana kwa kuendelea kutukumbusha juu ya itikadi hii ya ujamaa na kujitegemea.

Kila mmoja wetu anatakiwa kutambua kuwa ujamaa sio kuwa maskini na wala ubepari (ubeberu) sio kuwa tajiri.

Ujamaa ni ushirikiano na wenzako katika kazi kwa manufaa ya wote. Na pia; kujitegemea ni kutumia juhudi zetu pamoja na rasilimali zetu zote tulizonazo ili kujiletea maendeleo endelevu.

Ubepari unategemea udhaifu wa upande mmoja katika pande mbili zinazohusiana; udhaifu huo ni mwanya laini wa yule anayesikilizwa kuweza kujenga matakwa yake, kuupoteza upande dhaifu na kisha kuumeza upande huo katika nyanja zote. Mwisho, Serikali/dola hulinda masilahi ya kibeberu kwa gharama yoyote.​
 
Back
Top Bottom