May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,162
- 8,820
Kumezuka mtindo wa baadhi ya Mashabiki kujiona kwamba wao ndio Mashabiki wenye haki au bora au kindakindaki sana kuliko Mashabiki wengine.
Kila jambo wao wanataka kuliongelea hata kama hawana chochote wanachofahamu kuhusina nalo.
Ni ushabiki gani huu wa kushindwa kukubali timu kupoteza au kutoka suluhu?, hivi hizo timu nyingine kwani hazijiandai kushindana, kwani hao Makocha wengine hawafundishi hizo timu zao kwamba basi wakikutana na Timu yako tu basi wanapaswa kupoteza?
Ni sawa huenda kufungwa na Mtani kunanyong'onyeza lakini ndio iwe nongwa? Hawa Namungo si ndio waliwasumbua hata Yanga na nusura tu watoke suluhu, na si waliwapiga Azam 3 na ubora wao wote, sasa Simba kupata droo vipi iwe nongwa?.
Ingekuwa ni Timu inayopaswa kushinda tu wakati wote kuna haja gani basi ya kuwa na ligi?.
Nadhani udhaifu mkubwa kabisa kuliko wote ni hii ya kuonekana kukosa umoja pindi tu timu inapopoteza, kuliko hata kupoteza kwenyewe ndani ya uwanja.
Hiki ni kipindi cha Simba kuwa makini sana maana ndio kipindi ambacho Mamluki wanapenyeza ajenda zao na ikiwezekana kuitoa kabisaTimu kwenye Reli.
Furaha ya Simba ni Yanga kupoteza, na furaha ya Yanga ni Simba kupoteza, na tusisahau kwamba si kupoteza uwanjani tu, bali pia hata ikiwezekana kuipoteza timu.
Chondechonde Wana Simba, kuna Watu wapo kazini wanachochea kuni kwa bidii, hawalali, tusiwe kama Mazuzu mnachonganishwa nanyi mnavurugana kweli.