Fafanuzi za Oni sigala

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Mara kadhaa nimemsikia Mtaalamu wa Lugha Bw Oni Sigala akitoa ufafanuzi au maana ya maneno mbalimbali ya Kiswahili baada ya kuulizwa na Mtangazaji.

Mimi sio Mtalamu wa lugha hii ila ni mfuatiliaji na mpenzi wa lugha na napenda kujifunza kila wakati.

Hivi karibuni nimemsikia Mtaalamu huyu akitoa maelezo au ufafanuzi wa msemo "kuachwa solemba".

Kuna jambo sijaridhishwa nalo kabisa hapa.

Nijuavyo mimi msemo huu "kuachwa solemba" imetokana na wimbo maarufu wa kitambo, ambapo Mtunzi au Muimbaji anamlalamikia Mwanamke anayemtaja kwa jina la Solemba baada ya Solemba kutotimiza ahadi ya kukutana siku husika.

Kwenye wimbo huu kuna mstari unasema "nilikupenda kimapenzi Solemba wee ila dharau uliweka mbele Solemba"

Nilitarajia walau kwa maneno machache na muda mdogo uliopewa basi walau Mtaalamu angeuleza uma chimbuko la neno hilo Solemba. Kwa mfano nijuavyo mimi msemo huu ulitokana na wimbo huu...na ingawa Mtunzi alitumia Solemba kama jina la Muhusika ila baaadae Jamii walikuja kubadilisha kutoka jina la Muhusika kwenye wimbo hadi kumaanisha tukio lile la kutotimiza ahadi ya kukutana.

Labda ungenisahihisha kama taarifa niliyonayo mimi ni sahihi au la, je labda neno Solemba lilishakuwepo kabla ya Mtunzi au neno lilitokana na huo wimbo, na pia je, msemo huu ulisharasimishwa na baraza la Kiswahili au bado ni neno tu la mtaani?.

Badala yake Mtaalamu Oni anatoa maelezo hafifu sana na tena amenisikitisha zaidi anavyoonesha ya kuwa hana hata uhakika wa wimbo huo kwa kusema "anadhani ni wimbo wa zamani" sasa kwa nini uliharakisha kujibu badala ya kwanza kutafuta uhakika na kutoa kwa uma maelezo yaliyotimia?

Ni vema pale ambapo Mtaalamu unapata fursa ya kufafanua jambo basi uamini ya kuwa kuna hadhira kubwa mbele yako wanakusikilia, tukiwa na matarajia makubwa ya kujifunza kwa yale tusiyoyajua au kusahihishwa kutoka kile ambacho tumekuwa tukikiamini kabla, tuione tofauti ya Mtangazaji na Mtaalamu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom