Mashabiki Limbukeni na Wajuaji

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Siku chache zilizopitanilingia matatani baada ya kumtandia ngumi "mlevi" mmoja aliyekuwa anatukana hovyo matusi ya nguoni Wachezaji kwenye Luninga huku akijua fika kuwa hawamsikii bali anatusumbua tu sisi tuliopo pale kufuatilia mechi.

Utashangaa Mtu anavyomkosoa Kocha mpaka unajiuliza hivi huyu ndiye mwenye mawazo sahihi kuliko Kocha aliyepo pale? Yaani yeye ndiye Arsene Wenger au Furguson au Morinyo?

Hivi wakati huyo Kocha anaomba kazi wewe ulikuwa wapi? Si ungeomba na wewe kai upewe?.

Huyo Kocha kapeleka wasifu wake ndio maana yupo hapo, yupo kazini na analipwa kwa hiyo kazi sasa ni vipi tena nyie ndio mnataka kumuelekeza aifanye vipi kazi yake?.

Ujuzi aliojinadi nao ndio anaopaswa kuutekeleza pale ili aendelee kuwa kazini, sasa huo ushauri wenu nyie ni wa nini, kwani atakugawia mshahara wake? au siku akifukuzwa kazi atakuita ukamtetee?.

Huyo Kocha hatokaa hapo milele hivyo kama ninyi mnajua cha kufanya subirini akifukuzwa au akiondoka nanyi muombe kazi mkaweke huo utaalmu wenu, ambapo kila mkimpanga Mchezaji akikosea basi unamtoa unamuingiza mwingine, naye akikosea unamtoa na kumuingiza mwingine. Nadhani pia mtapendekeza na sheria ya substitution ibadilishwe kuwe na Wachezaji mia wanaosubiri nje, na vikombe mtazoa kwa kila shindano.

Mjinga siku zote hufikiri kila jambo ni rahisi tu, na vichwa vyenu vitupu hivyo ukipewa viatu vya Kocha wakati wa mechi anayohitaji ushinda ili ajira yake ibaki hivi ni wangapi mtaviweza?

Utamsikia Mtu analalamika kwa nini hujamuingiza huyu au yule, Watu vichwa vimeshaathiriwa na betting sasa kazi imekuwa ni kubashiri tu kila kitu...kwamba akiingia fulani atacheza vizuri, au akiingia fulan ndio atafunga magoli.

Tuache ushabiki Maandazi na tuheshimu kazi za Wengine.
 
Umeandika Vizuri sana

BINAFSI MIJITU INAYONIBOA ZAIDI NI WATETEZI WA MOSES PHIRI

Tangu Enzi za Zolan Mark
Hata Robertinho.
Hawa ni Professional Coaches wote wanamuweka Benchi.

(Jiulize kwanini MAKOCHA wote wawili wakuweke Benchi).

Phiri ni Mshambuliaji WA pili
(Second straiker)
Au false No 9
Uwe na mshambuliaji kamili kama Baleke HALAFU uende na Phiri hili halikubaliki na HAIWEZEKANI.

UDHAIFU WAKE.
1. Anapoteza sana Mipira.
2. Hawezi ku Link up team kutoka chini.
3. Hafai kuwa hata Target man.
4. Anakuwa Off position ya No 10.
5.Mfupi WA kimo na Hana low center of gravity Compare to Saido, KIBU Miquissone na mzamiru.

6.Anaanguka kupita kiasi na ni mwepesi.

7. Huwa anapoteana kwenye michezo mikubwa eg wakati WA Mgunda alicheza Simba na Yanga Ya 1-1 wafungaji Azizi ki na Okrah. Hakuonekana hata kwa Dakika 1

8. Majeraha ya mara kwa mara.

NB.
NILIWAAMBIA mchezaji mzuri Huwa HAUMII (si injury prone otherwise Afanyiwe Upasuaji utakao muweka Nje kwa muda mrefu?)
Phiri anasingizia majeraha tu

UIMARA.
1.Analijua sana Goli
2. Kasi.
3. Uwezo WA kutumia Miguu yote.

JUZI kaingia Dk 89
Anapata kigugumizi na Kutaka kuichomesha Simba mbele ya Alahly.

Phiri si MCHEZAJI MZURI.
Kama Ningukuwa kwenye kamati ya UFUNDI ama usajili, Moja ya Wachezaji wa Kupunguzwa ni Moses phiri.

NIKIONA mtu anamtetea Phiri
najua huyo mtu hamna kitu na hajuhi Mpira.

Pathetic
 
Bado anatufaa atatuvusha ni majeruhi tu ndio yanamsumbua tumvumilie

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
 
Unless unafatilia soka la Bonga tu unaweza kuandika post kama hii.
Wewe taja Nchi, acha siasa hapa. Kazi ya shabiki ni kupiga kelele sasa wewe unataka wafanyeje. Ndio maana nimeuliza wapi mashabiki hawapayuki, kule Uingereza na Italy hadi wanaandamana, nyie mnazungumzia kupayuka tu.
 
Back
Top Bottom