Kuwe na muwakilishi wa BAKITA kwenye vituo vya Redio

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Hakuna maana yoyote ya kijinadi kama taifa la Kiswahili kama kwenye vyombo vyetu vya habari vinakuwa na makosa mengi kwenye matamshi ya Kiswahili.

Au la basi mmoja wa Watangazaji anayekidhi vigezo apate ithibati ya Baraza. Walau kwa vile vituo vya rediuo vyenye Wasikilizaji wengi.

Kazi yake kubwa itakuwa ni kusahihisha kila pale ambapo Mtangazaji atakosea kutamka neno au maneno ya Kiswahili kwa ufasaha. Hata ikiwezekana marekebisho yafanyike papo hapo baada ya Mtangazaji kukosea.

Fikiria tu Mgeni kafika Tanzania na amejifunza Kiswahili fasaha huko kwao, anasikiliza Redio anakutana na Watangazaji wanaobanga Kiswahili, anasema zarura badala ya dharura, Mkoa wa Ilinga badala ya Iringa n.k.

Kutokana na Watangazaji tulio nao mpaka wa leo sijui uwanja ni wa Riti au Liti, Ruangwa au Luangwa n.k. yaani kila Mtangazaji anatamka kivyake.

Tunawaweka njiapanda wanaotarajia kujifunza zaidi kupia kusikilza Redio.
 
Back
Top Bottom