Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, limebariki adhabu ya kifo aliyopewa mmoja wa mafundi waliokuwa wanajenga kituo cha kuuza mafuta Jijini Dodoma, Menroof Haule aliyewaua walinzi wawili wa kimasai.
Hukumu ya kubariki adhabu hiyo imetolewa Februari 20, 2024 na majaji Augustine Mwarija...