Kitanzi chamng’ang’ania aliyeua walinzi wawili wa Kimasai

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, limebariki adhabu ya kifo aliyopewa mmoja wa mafundi waliokuwa wanajenga kituo cha kuuza mafuta Jijini Dodoma, Menroof Haule aliyewaua walinzi wawili wa kimasai.

Hukumu ya kubariki adhabu hiyo imetolewa Februari 20, 2024 na majaji Augustine Mwarija, Rehema Kerefu na Mustafa Ismail, ambao wamesema kuwa kesi ya upande wa Jamhuri ilikuwa imethibitishwa pasipo kuacha mashaka.

Hivyo majaji hao wamezitupa sababu 12 alizokuwa ameziwasilisha mbele ya Mahakama ya Rufani akijaribu kujinasua na adhabu ya kifo aliyokuwa amehukumiwa Aprili 11, 2022 na Jaji Adam Mambiwa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma.

Maelezo yake mwenyewe ya kukiri kosa akisimulia hatua kwa hatua namna alivyowaua walinzi hao kwa kuwaponda vichwa kwa kutumia sululu, ndio yalimmaliza ambapo majaji wamesema ushahidi dhidi yake ulikuwa mzito.

Walinzi hao wawili, Paulo Nduluma na Aloyce Patsango, waliuawa Agosti 4,2015 na maiti zao ziligunduliwa saa 11:00 alfajiri na mama lishe, Bilha Yaho ambaye ana kawaida ya kuwauzia chakula mafundi waliokuwa wanajenga kituo hicho.

Kama ulivyo utaratibu wake, siku hiyo alifika eneo la ujenzi na kuanza kuwaita walinzi hao bila mafanikio, ambapo aliamua kuingia ndani kuchota maji ili kusafisha vyombo, ndipo alipoona damu ukutani na baadaye miili ya walinzi hao.

Baada ya kuona hivyo, aliwapigia simu mafundi wengine ambao nao walimjulisha msimamizi wa ujenzi huo na taarifa zikafikishwa Polisi, ambao walifika eneo la tukio na kuanza uchunguzi na baadaye kumkamata Haule Agosti 9,2015.

Mashahidi sita wa Jamhuri wakiwemo askari wawili waliochunguza mauaji hayo, walisema katika uchunguzi wao walibaini kasha (container), lililokuwa linahifadhi mifuko ya saruji likiwa limevunjwa na mifuko 60 ilikuwa imeibwa.

Kulingana na ushahidi huo, Haule alipokamatwa na Polisi, alikiri kufanya mauaji hayo na kuiba mifuko hiyo 60, ambapo maelezo yake ya onyo yaliandikwa na baadaye akapelekwa kwa mlinzi wa amani na kuandika maelezo ya ungamo.

Maelezo ya ungamo

Sehemu ya maelezo yake ya onyo aliyoyaandika Polisi, muuaji huyo anaeleza “Ilipofika tarehe 4.8.2015 nikaingia kazini asubuhi nikafanya kazi nikamaliza saa 11 jioni na kuacha Sululu ndani ya shimo lenye futi tano,”

Anaendelea kueleza “Majira ya saa 2:00 usiku nikiwa tayari nimekwishapitia pale shimoni na kuchukua sululu tayari kwa kuwavizia walinzi wa kimasai na kuwaua kabisa, walikaa wakiwa wanaongea kwa muda hadi saa 6:00 usiku”

“Ndipo nikawaona wametawanyika na kila mmoja ameelekea kulala. Mmoja akapanda kwa juu na mwingine akalala kwa chini. Nikakaa kidogo kuwasubiria usingizi uwapitie kwanza kwa muda wa nusu saa hivi.”

“Ndipo nikaona muda ule unatosha nikavua viatu vyangu na kuviacha nje kwenye banda la mama lishe nikarudi nikaruka ukuta nikatembea kwa kuambaa ambaa na ukuta huku nikinyata hadi sehemu ya juu ya jengo nikamkuta Mmasai amelala,”

“Nikiwa nimeshikilia sululu mkononi ambayo ilikuwa imekatika upande mmoja, nikampiga na sululu kichwani mara mbili kwa kutumia upande ule uliokatika nikahakikisha hatikisiki kabisa. Nikashuka kumtafuta mmasai mwingine.”

“Nikamkuta na yeye amelala nikampiga kichwani mara tatu kwa kutumia ile sululu na kumpasua kichwa naye hakuamka wala kutikisika. Ndipo nikapata wazo la kwenda kuvunja kontena (kasha) ili nichukue cement (saruji).

Sehemu ya maelezo yake aliyoyaandika kwa mlinzi wa amani ambaye ni Hakimu, alieleza “Kuanzia saa 2 usiku nilianza kuwavizia kujua wanalala wapi. Nilipoona wamelala usiku huo, niliamua kuwafuata na kuwapiga na kitu kizito kichwani”

“Nikawaona wote wamekufa baada ya kuwagonga, walikuwa wawili. Nilipojua wamekufa nilichukua nyundo nikafungua kontena nikachukua mifuko ya cement (saruji) jumla mifuko 60…”, ameeleza muuaji huyo katika maelezo yake ya ungamo.

Alivyojitetea ili kujinasua lakini wapi

Katika utetezi wake, muuaji huyo anayesubiri kunyongwa kama Rais ataweka saini yake, alikiri kuwa mmoja wa mafundi katika eneo la ujenzi na anawafahamu marehemu, walikuwa ni marafiki wakubwa na hawakuwahi kugombana.

Akaeleza kuwa mchana wa Agosti 3,2015, alikwenda katika eneo la ujenzi na kukaa na marehemu (walinzi) kwa amani kabisa na Agosti 4,2015 ndipo akajulishwa kuwa na shahidi wa kwanza (mama lishe) kuwa wameuawa.

Pia akakiri kuwa Agosti 9, 2015 alikamatwa akihusishwa na mauaji hayo na akadai kuwa aliteswa alipokamatwa lakini hata hivyo akakiri kuandika maelezo hayo ya onyo na ya ungamo, ambayo tayari yalikuwa yamepokelewa kama kielelezo.

Pamoja na utetezi huo, Jaji alimtia hatiani kwa kuzingatia mazingira ya tukio na maelezo yake mwenyewe ya kukiri kufanya mauaji hayo, ambayo Jaji alisema yalieleza kila kitu namna alivyoua hivyo akamuhukumu adhabu ya kifo.

Hakuridhika na adhabu hiyo ya Jaji Dk Adam Mambi ndipo akakata rufaa Mahakama ya Rufani ambayo hata hivyo ilibariki maamuzi ya Mahakama Kuu iliyomuhukumu kunyongwa hadi kufa, wakisema rufaa yake haina mashiko.

Source - Mwananchi
 
Fundi mjinga sana huyo! Mifuko 60 ya saruji ndiyo imsababishe aue watu wawili!!

Sema tu kwabupande wangu sijaridhishwa na mwenendo wa mshtaka. Binafsi nilitamani kuona wapepelezi wa hiyo kesi wanafikia hatua ya kuwafahamu wahusika waliouziwa hiyo saruji ya wizi ili wathibitishe kama ni kweli waliuziwa na mtuhumiwa baada ya kukiri kosa!

Na pia waoneshe usafiri (kama upo) uliotumika kubebea hiyo saruji. Yaani kiufupi walitakiwa kutuambia mtuhumiwa aliipeleka wapi hiyo saruji baada ya kufanya hayo mauaji, na pia kulivunja hilo kontena.

Huu ushahidi ulikuwa ni muhimu sana.
Maana isije ikawa polisi wamemlazimisha kukiri kosa baada ya kumtesa mtuhumiwa, kama ilivyo kawaida yao ya kutumia nguvu kubwa kuliko akili! huku wahusika halisi wakiwa wakipotelea kusiko julikana.
 
Halaf anakuja kaa miaka 30 jela..kazeeka anaachiwa kwa msamaha wa raisi..hiv hawa maraisi inabid siku1 wawe wanaulizwa..why huwa hawa sign..maana ni kaz yao hyo na hawaifanyi
 
Hiyo kazi ya kusaini kunyongwa watu hadi kufa wangenipa mimi, jamaa anakula ugali tu vijana wa watu wameshaoza kaburini haipo fair kabisa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Halaf anakuja kaa miaka 30 jela..kazeeka anaachiwa kwa msamaha wa raisi..hiv hawa maraisi inabid siku1 wawe wanaulizwa..why huwa hawa sign..maana ni kaz yao hyo na hawaifanyi
Hivi ilishawahi kutokea mfungwa aliyehukumiwa kunyongwa akaachiwa kwa msamaha wa rais?
 
Nimesoma maelezo ya ungamo ninaona kabisaa kuna matundu yanayomtoa mtuhumiwa hatiani.
Yaani baada ya kuua ndo akapata wazo la kwenda kuvunja na kuiba saruji?
Maelezo ya ushahidi wa polisi ni katika kudadavua upelelezi ulivyofanyika, je mashahidi wengine kutoka eneo husika walisemaje kuhusu yeye kudiriki kuua?

Ninaona kabisa upo uwezekano muuaji akawa ameshika mpini mahala na polisi wamemuokoa kwa style yao ya kumbabatiza yeyote kwenye kumi na nane zao akiri kosa kama walivyofanya kina Kingai kwa ile kesi ya Mbowe
 
Nikawaona wote wamekufa baada ya kuwagonga, walikuwa wawili. Nilipojua wamekufa nilichukua nyundo nikafungua kontena nikachukua mifuko ya cement (saruji) jumla mifuko 60…”, ameeleza muuaji huyo katika maelezo yake ya ungamo.
 
Fundi mjinga sana huyo! Mifuko 60 ya saruji ndiyo imsababishe aue watu wawili!!

Sema tu kwabupande wangu sijaridhishwa na mwenendo wa mshtaka. Binafsi nilitamani kuona wapepelezi wa hiyo kesi wanafikia hatua ya kuwafahamu wahusika waliouziwa hiyo saruji ya wizi ili wathibitishe kama ni kweli waliuziwa na mtuhumiwa baada ya kukiri kosa!

Na pia waoneshe usafiri (kama upo) uliotumika kubebea hiyo saruji. Yaani kiufupi walitakiwa kutuambia mtuhumiwa aliipeleka wapi hiyo saruji baada ya kufanya hayo mauaji, na pia kulivunja hilo kontena.

Huu ushahidi ulikuwa ni muhimu sana.
Maana isije ikawa polisi wamemlazimisha kukiri kosa baada ya kumtesa mtuhumiwa, kama ilivyo kawaida yao ya kutumia nguvu kubwa kuliko akili! huku wahusika halisi wakiwa wakipotelea kusiko julikana.
Ulilosema haswa ndilo lilipaswa hata judge wa mahakama kuu kulizingatia kabla ya kutoa hukumu kwa mshtakiwa. Mara nyingi watuhumiwa hulazimishwa kutoa maelezo ya kukiri kwenye "Onyo" na "Ungamo" ili mradi kufupisha uchunguzi na kuikimbiza case mahakamani ili DCI warelax. Wanasema aliyekamatwa na ngozi ndiye mla nyama.....
 
Mifuko 60 ya saruji imesababisha mauti ya nafsi mbili na maisha jela ya nafsi moja.

Hii ni fedheha kwa Serikali ya CCM (tena katika awamu) iliyojitanabaisha kuleta maisha bora kwa kila mwananchi.

Shame on them.
 
Halaf anakuja kaa miaka 30 jela..kazeeka anaachiwa kwa msamaha wa raisi..hiv hawa maraisi inabid siku1 wawe wanaulizwa..why huwa hawa sign..maana ni kaz yao hyo na hawaifanyi
Baadae ya miaka 30 wakiachiwa huwa wanateseka sana sana
 
Na pia waoneshe usafiri (kama upo) uliotumika kubebea hiyo saruji. Yaani kiufupi walitakiwa kutuambia mtuhumiwa aliipeleka wapi hiyo saruji baada ya kufanya hayo mauaji, na pia kulivunja hilo kontena.
Waandishi wa habari Tanzania hawapo makini, inatakiwa wajiongeze wanapo ripoti taarifa za Mahakamani au Polisi:

Maelezo katika hukumu hapa chini yamenukuliwa na kutafsiriwa kwa kiswahili, fasiri isiyo kamili ya lugha ya kisheria (ambayo ni English) yamejibu swali lako zuri kama msomaji makini wa JF :

Askari polisi Nambari F.3630 D/SGT Zephania (PW6) na Mpelelezi Na. E.9788
Fabian (PW7) alieleza kwamba, tarehe 4 Agosti, 2015, walipewa kazi hiyo kuchunguza tukio la mauaji katika eneo la ujenzi. Walikwenda kwenye tukio siku hiyo hiyo na kukuta damu na container llililohifadhi simenti likiwa limevunjwa na
walifahamishwa kuhusu tukio la wizi. Ilikuwa ni ushuhuda zaidi wa PW6 kwamba walimkamata dereva na gari ambalo lilikuwa limetumika kubeba mifuko sitini ya saruji iliyoibiwa kutoka kwenye container ya ujenzi. Alisema dereva aliwapeleka kwa Mustapha Salum Rajab (PW5), mnunuzi wa simenti zilizoibiwa
ambaye aliwaambia kuwa alinunua simenti hiyo kutoka kwa mrufani.

Baadaye, mrufani alikamatwa tarehe 9 Agosti, 2015 na
alipohojiwa, alikiri kuwaua watu waliofariki kwa kwa kutumia sululu na kisha kuiba mifuko sitini ya saruji. PW7 alithibitisha kuwa alimhoji mrufani na kurekodi onyo lake kauli. Katika taarifa hiyo, mrufani alikiri kuwa
alifanya kosa na kuwapeleka mahali ambapo alificha sululu,
....

Ukurasa wa 4

No. F.3630 D/SGT Zephania (PW6) and No. E.9788 Detective
Fabian (PW7) testified that, on 4th August, 2015, they were assigned to investigate the murder incident at the construction site. They went to the scene on the same day and found blood and the broken container and were informed about the theft incident. It was further testimony of PW6
that they arrested the driver and the motor vehicle which was used to carry the stolen sixty bags of cement from the construction site. The said
driver took them to Mustapha Salum Rajab (PW5), the buyer of the stolen cement who told them that he bought the same from the appellant.
Subsequently, the appellant was arrested on 9th August, 2015 and
upon interrogation, he confessed to have killed the deceased persons by using the pick axe and thereafter, stole the sixty bags of cement. PW7 testified that he interviewed the appellant and recorded his cautioned
statement. In the said statement, the appellant confessed to have
committed the offence and led them to a place where he hid the pick axe, he used to kill the deceased persons. The appellant's cautioned statement
and the pick axe were admitted in evidence as exhibits P2 and P5
respectively.
Thereafter, on 10th August, 2015, the appellant was taken to Rachel Magoti (PW4), the Justice of Peace and the Resident Magistrate who was .....

Page 4

Soma hukumu kamili :
Source : Menroof January Haule vs Republic (Criminal Appeal No. 121 of 2022) [2024] TZCA 69 (20 February 2024)

Menroof January Haule vs Republic (Criminal Appeal No. 121 of 2022) [2024] TZCA 69 (20 February 2024)​

Back
Top Bottom