WAZIRI DKT. NDUMBARO: UWANJA WA CCM MAJIMAJI KUFANYIWA UKARABATI
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekabidhi mashine mbili za kukatia nyasi katika uwanja wa mpira wa miguu wa CCM Majimaji kwa uongozi wa chama hicho Mkoa wa Ruvuma...
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro ametembelea na kukagua eneo la Olmoth ambalo litajengwa uwanja mpya wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kuchukua watazamaji Elfu thelathini utakaotumika katika michuano ya AFCON 2027.
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekagua eneo hilo Desemba 15...
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Wizara anayoiongoza itaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa Kituo Cha Michezo katika Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya mkoani Mwanza kama ilivyopanga.
Dkt. Ndumbaro amesema hayo Novemba 6, 2023 Bungeni Jijini Dodoma...
WAZIRI DKT. NDUMBARO: TAMASHA LA KABILA LA WAMATENGO KUFANYIKA KILA MWAKA
Tamasha la Utamaduni wa kabila la Wamatengo Mkoani Ruvuma litafanyika kila mwaka ili kutangaza utamaduni wa kabila hilo na Mkoa wa Ruvuma ndani na nje ya Tanzania.
Hayo yameelezwa Oktoba 30, 2023 na Waziri wa Utamaduni...
WAZIRI DKT. NDUMBARO ATETA NA UONGOZI WA FIFA NA CAF
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA ) katika Ukanda wa CECAFA, Andrea Silva na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu...
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameilekeza Bodi ya Filamu nchini ishirikiane na Sekta binafsi katika kuhakikisha filamu za Tanzania zinakua bora zaidi na zinapata soko la uhakika.
Dkt. Ndumbaro ametoa agizo hilo Oktoba 12, 2023 alipofanya ziara katika Bodi hiyo...
WAZIRI DKT. NDUMBARO AIPONGEZA COSOTA NA KUTOA MAAGIZO
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameiagiza Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) iandae taarifa kuhusu mgogoro wa Hakimiliki kwa kazi ya ubunifu wa michoro ya Tingatinga pamoja na kufuatilia Mtunzi na Mmiliki...
WAZIRI DKT. NDUMBARO AAGIZA KUMBI ZOTE ZA STAREHE ZISAJILIWE KABLA YA NOVEMBA 30
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewaagiza Maafisa Utamaduni kote nchini kuhakikisha kuwa wanasajili Kumbi zote za starehe na kuhakikisha kumbi hizo zinakidhi vigezo vyote kwa mujibu...
Ukarabati wa Awamu ya Kwanza unaoendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam umefikia asilimia 95 na asilimia tano zilizobaki zinatarajiwa kukamilika ndani ya siku tano kuanzia leo.
Akikagua ukarabati huo leo Oktoba 9, 2023, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas...
WAZIRI DKT. NDUMBARO: MIKUTANO YA KIMATAIFA INAYOFANYIKA NCHINI NI FURSA YA KUTANGAZA KISWAHILI
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema mikutano ya Kimataifa inayofanyika hapa nchini ni fursa ya kutangaza lugha adhimu ya Kiswahili ambayo ni mojawapo ya Lugha Rasmi...
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema haikuwa kazi rahisi kwa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kushinda zabuni ya kuandaa Fainali za Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027).
Dkt. Ndumbaro amesema hayo Septemba 29, 2023 jijini Dar es Salaam...
WAZIRI DKT. NDUMBARO ATETA NA WAZIRI WA MICHEZO MISRI
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Vijana na Michezo wa nchini Misri Mhe. Ashraf Sobh Septemba 25, 2023 Jijini Cairo.
Viongozi hao wamekubaliana kushirikiana baina ya...
WAZIRI DKT. NDUMBARO - TANZANIA NA IRELAND KUSHIRIKIANA KATIKA SOKA LA WANAWAKE NA UCHORAJI
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na Balozi wa Ireland hapa nchini Mhe. Mary O' Neill na kukukubaliana kushirikiana katika Sekta ya michezo hususan soka la...
WAZIRI DKT. NDUMBARO AIAGIZA MIKOA KUJIANDAA VYEMA MASHINDANO YA SAMIA TAIFA CUP
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameiagiza Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kujiandaa vyema kwa ajili ya mashindano ya Samia Taifa Cup ambayo yatafanyika mwishoni mwa mwaka huu...
WAZIRI DKT. NDUMBARO ASISITIZA WADAU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUENDELEZA MICHEZO NCHINI
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Septemba 20, 2023 Jijini Dar es Salaam amekutana na viongozi wa timu ya Simba ambapo wamejadili masuala mbalimbali yakiwemo maendeleo ya michezo...
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo na Mbunge wa JImbo la Songea Mjini, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameambatana na Komredi Alhaji Mwinyi Msolomi, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Songea kutoa msaada wa mifuko 50 ya Saruji ili kuwezesha ujenzi wa Ofisi ya Tawi la Mahenge Kata ya Songea...
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Avetisyan Septamba 14, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Katika Mazungumzo yao viongozi hao wamekubaliana kushirikiana katika Sekta ya Utamaduni na Michezo...
WAZIRI DKT. NDUMBARO - BASATA VIBES KUTIKISA MIKOA YOTE NCHINI
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lihakikishe kuwa Mradi wa Baraza hilo ujulikanao kama BASATA Vibes unawafikia Wasanii mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar ili azma ya Serikali ya...
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amemuagiza Mkandarasi wa Ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa Beijing Construction Engineering Group (BCEG) kufanya kazi hiyo, kwa saa 24 na siku zote za wiki ili kazi hiyo ikamilike kabla ya Oktoba 15, 2023.
Dkt. Ndumbaro ametoa...
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amezindua Bodi ya Hakimiliki Tanzania (COSOSTA) na Bodi ya Bodi ya Filamu Tanzania na kuwataka Wajumbe wa Bodi hizo kuhakikisha sekta ya Sanaa inatoa ajira za kutosha na wananchi wanafaidi matunda ya kazi zao.
Waziri Dkt. Ndumbaro...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.