Waziri Dkt. Ndumbaro: Mikutano ya Kimataifa Inayofanyika Nchini ni Fursa Kukuza Kiswahili

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942

WAZIRI DKT. NDUMBARO: MIKUTANO YA KIMATAIFA INAYOFANYIKA NCHINI NI FURSA YA KUTANGAZA KISWAHILI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema mikutano ya Kimataifa inayofanyika hapa nchini ni fursa ya kutangaza lugha adhimu ya Kiswahili ambayo ni mojawapo ya Lugha Rasmi ya Kikazi ya Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Jumuiya kadhaa za Kikanda Barani Afrika.

Mhe. Ndumbaro amesema hayo Oktoba 7, 2023 jijini Arusha katika kikao cha Maandalizi ya Mkutano wa 77 wa Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 20 hadi Novemba 9, 2023 jijini Arusha.

Mhe. Ndumbaro ameongeza kuwa, Tanzania ina Wataalamu katika tafsiri na ukalimani hivyo wana uwezo wa kutoa huduma ya ukalimani katika Mikutano hiyo.

Kikao hicho kimeongozwa na Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana, Waziri wa Katiba na Sheria na kuhudhuriwa na Mhe. Haroun Suleimani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 

Attachments

  • F71iD3eXsAAnWWu.jpg
    F71iD3eXsAAnWWu.jpg
    116.3 KB · Views: 1
  • F71iEnuWwAAj54O.jpg
    F71iEnuWwAAj54O.jpg
    207 KB · Views: 1
Back
Top Bottom