Waziri Dkt. Ndumbaro Aagiza Mikoa Kujiandaa Vyema Mashindano Samia Taifa CUP

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
WAZIRI DKT. NDUMBARO AIAGIZA MIKOA KUJIANDAA VYEMA MASHINDANO YA SAMIA TAIFA CUP

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameiagiza Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kujiandaa vyema kwa ajili ya mashindano ya Samia Taifa Cup ambayo yatafanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Mhe. Ndumbaro ametoa maagizo hayo Septemba 21, 2023 Zanzibar wakati akikabidhi vifaa vya michezo kwa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo ambayo yatahusisha michezo mbalimbali.

"Mwaka huu mashindano yatajumuisha pia Zanzibar na kutakua na Mashindano ya Muziki wa Kizazi Kipya. Lengo la mashindano haya ni kuendelea kuenzi Muungano wetu na kuhakikisha jamii inajishughulisha na michezo, Sanaa na Utamaduni kwakua ni Sekta ambazo zinaibua vipaji na kutoa fursa ya ajira" amesema Mhe. Ndumbaro.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita amesema vifaa hivyo vitagawiwa katika mikoa yote ya Zanzibar na mashindano yataanzia katika ngazi ya Shehia mpaka Mkoa ili kupata wawakilishi wazuri Kitaifa.

Miongoni mwa vifaa alivyokabidhi Mhe. Ndumbaro ni pamoja na mipira ya michezo ya mpira wa Miguu, Kikapu na Wavu ambayo kila mchezo mipira 18 huku akiwakaribisha wadau kuiunga mkono jambo hilo katika michezo mingine.

F6ipoYVXoAElLVT.jpg

F6ipp8UXUAAO98C.jpg
F6ipripWcAAO6wa.jpg
F6ips9mXQAAIYYU.jpg
 
Huyu ni mjanja sana. Ukitaka kuwasahaulisha Watanzania, wekeza kwenye michezo na burudani hasa mpira wa miguu.

Tunaendelea kushauri pia, ule mpango wa kuboresha viwanja vya mpira wa miguu muufanyie kazi na ikiwezekana mfanye utaratibu kila mkoa uwe na timu ya ligi kuu, hakika mtatukamata sana Watanzania, hatutawasumbua kuhoji mambo yenu mnayopuyanga.

Na ikikaribia kampeni, fanyeni mpango mzilipe Simba na Yanga wazunguke nchi nzima wacheze mechi za kirafiki kila mkoa, hapo lazima tutawapa kura.
 
Na wasanii waimba amapiano singeli watazunguka nchi nzima
Na wabongo walivyomazz lazima watajitokeza

Ova
 
Hayo mashindano ndiyo mbadala wa mashindano ya TAIFA CUP yaliyoanza enzi za Mwalimu?
Kama ni hayo nadhani yangeitwa NYERERE CUP kwa heshima ya Mwalimu!
 
Samua cup ni mpango wa CCM kuanza kampeni mapema maana walishajua mama muuza hauziki. Sasa wanatafuta angalau huruma za wapumbavu wasiojua maana ya utu wao.
 
Back
Top Bottom