Waziri Dkt. Ndumbaro: Haikuwa Kazi Rahisi Kushinda Kuandaa AFCON 2027

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema haikuwa kazi rahisi kwa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kushinda zabuni ya kuandaa Fainali za Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027).

Dkt. Ndumbaro amesema hayo Septemba 29, 2023 jijini Dar es Salaam alipokuwa kwenye mkutano na waandishi wa Habari kuhusu nchi hizo za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuandaa mashindano hayo makubwa barani Afrika.

“Haikuwa kazi ndogo, ilikuwa kazi ngumu sana, tuliweka mikakati ya pamoja ya kutosha kuhakikisha zabuni yetu ambayo sasa ni EA Pamoja AFCON 2027 inashinda. Mipango yetu ilikuwa na nguvu na msukumo wa Marais wetu watatu; Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Dkt. William Samoye Ruto na Mhe. Jenerali Yoweri Kaguta Museveni utayari na mchango wao kwenye mashindano haya kwetu ulikuwa mtaji wa kwanza” amesema Dkt. Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro amesema Wizara itatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kujenga viwanja vipya viwili na kusisitiza maandalizi mengine yafanyike haraka na kwa wakati ili Watanzania wanufaike.

Vigezo ambavyo vimetumika kushinda zabubi hiyo ni pamoja na Serikali zote tatu ziwe na dhamana ya Dola za Marekani Milioni 30 kwa kila nchi ambapo jumla yake ni Dola za Marekani Milioni 90, viwanja sita vya mashindano na kila nchi inapaswa kuwa na angalau viwanja viwili ambapo kwa Tanzania upo Uwanja wa Benjamin Mkapa umekidhi sifa na unaendelea kufanyiwa ukarabati wa awamu ya kwanza, Uwanja wa Aman Zanzibar, huu unaendelea na maboresho huku Uwanja mpya wa Arusha unatarajiwa kujengwa na kukamilika kabla ya mashindano ya AFCON 2027.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw. Wallace Karia amesema anawashukuru mawaziri wote wa michezo, Dkt. Damasi Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania, Mhe. Ababu Namwamba, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Kenya na Mhe. Peter Ogwang, Waziri wa Nchi Elimu na Michezo, Uganda kwa kazi kubwa waliyoifanya kufanikisha ushindi huo nan chi hizo kupewa dhamana ya kuwa mwenyeji wa AFCON 2027.

WhatsApp Image 2023-09-29 at 20.40.04(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-29 at 20.40.04.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-29 at 20.40.03(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-29 at 20.40.03.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-29 at 20.40.01.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-29 at 20.40.00.jpeg
 
Kumbe sio yanga. Kuna uzi wa wana yanga kujinasibu wao ndo wameleta mtashindano.
 
Ana mbwembwe huyu

Kuna siku nlipishana naye mahali

Kimo chake kilikuwa chini ya mabega

Yangu

Ova
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema haikuwa kazi rahisi kwa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kushinda zabuni ya kuandaa Fainali za Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027).

Dkt. Ndumbaro amesema hayo Septemba 29, 2023 jijini Dar es Salaam alipokuwa kwenye mkutano na waandishi wa Habari kuhusu nchi hizo za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuandaa mashindano hayo makubwa barani Afrika.

“Haikuwa kazi ndogo, ilikuwa kazi ngumu sana, tuliweka mikakati ya pamoja ya kutosha kuhakikisha zabuni yetu ambayo sasa ni EA Pamoja AFCON 2027 inashinda. Mipango yetu ilikuwa na nguvu na msukumo wa Marais wetu watatu; Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Dkt. William Samoye Ruto na Mhe. Jenerali Yoweri Kaguta Museveni utayari na mchango wao kwenye mashindano haya kwetu ulikuwa mtaji wa kwanza” amesema Dkt. Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro amesema Wizara itatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kujenga viwanja vipya viwili na kusisitiza maandalizi mengine yafanyike haraka na kwa wakati ili Watanzania wanufaike.

Vigezo ambavyo vimetumika kushinda zabubi hiyo ni pamoja na Serikali zote tatu ziwe na dhamana ya Dola za Marekani Milioni 30 kwa kila nchi ambapo jumla yake ni Dola za Marekani Milioni 90, viwanja sita vya mashindano na kila nchi inapaswa kuwa na angalau viwanja viwili ambapo kwa Tanzania upo Uwanja wa Benjamin Mkapa umekidhi sifa na unaendelea kufanyiwa ukarabati wa awamu ya kwanza, Uwanja wa Aman Zanzibar, huu unaendelea na maboresho huku Uwanja mpya wa Arusha unatarajiwa kujengwa na kukamilika kabla ya mashindano ya AFCON 2027.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw. Wallace Karia amesema anawashukuru mawaziri wote wa michezo, Dkt. Damasi Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania, Mhe. Ababu Namwamba, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Kenya na Mhe. Peter Ogwang, Waziri wa Nchi Elimu na Michezo, Uganda kwa kazi kubwa waliyoifanya kufanikisha ushindi huo nan chi hizo kupewa dhamana ya kuwa mwenyeji wa AFCON 2027.

View attachment 2766597View attachment 2766598View attachment 2766599View attachment 2766600View attachment 2766601View attachment 2766602
Mtu hata mwezi haujakaa kwenye hicho kiti tayari unajifanya unajua ugumu wa huu mchakato.
 
Ana mbwembwe huyu

Kuna siku nlipishana naye mahali

Kimo chake kilikuwa chini ya mabega

Yangu

Ova
Kawaida kwa watu wafupi hata huku kwetu Moro wako hivyo hivyo. Wengi hupenda mabibi wenye miili mikubwa na matako makubwa, magari makubwa na stori za Mambo makubwa.j
 
Back
Top Bottom