Waziri Dkt. Ndumbaro Azindua Bodi Mbili, Azipa Jukumu la Kuongeza Mapato

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amezindua Bodi ya Hakimiliki Tanzania (COSOSTA) na Bodi ya Bodi ya Filamu Tanzania na kuwataka Wajumbe wa Bodi hizo kuhakikisha sekta ya Sanaa inatoa ajira za kutosha na wananchi wanafaidi matunda ya kazi zao.

Waziri Dkt. Ndumbaro amesema hayo Septemba 12, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa bodi za taasisi hizo zinajishughulisha na sekta ya Sanaa nchini na kuongeza kuwa wajumbe wa bodi hizo ni wawakilishi wa Serikali katika taasisi hizo.

“Wizara hii ina dhamana kubwa na watekelezaji wa kazi zake ni taasisi zinazosimamiwa na Bodi, kazi yenu ni kuhakikisha taasisi mnazozisimamia zinakua kiuchumi ili kukuza Pato la Taifa na uchumi wa wadau wa sekta yetu ya Sanaa ambayo imekua kwa asilimia 19 ”amesisitiza Waziri Dkt. Ndumbaro.

Awali akimkaribisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro kuzindua Bodi hizo, Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma amewahimiza wajumbe wa bodi hizo kutekeleza wajibu wao ili kuleta uhalisia na utofauti wa utendaji wa kazi wa taasisi hizo kabla ya uteuzi na baada ya kuingia madarakani.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Saidi Yakubu amesisitiza kuwa sekta ya Sanaa nchini imekuwa na Tanzania ni ya pili Afrika ambapo inazalisha filamu 2000 kwa mwaka sawa na wastani filamu sita kwa siku.

Ameongeza kuwa Sekta hiyo imefanikiwa kuzalisha wingi wa filamu na kuwahimiza wajumbe hao kushirikiana na taasisi wanazoziongoza ili kujikita kuzalisha kazi bora ambazo zitakuwa chanzo adhimu cha mapato kwa wasanii na taifa kwa ujumla.

Aidha, Bw. Yakubu amezitaka Bodi hizo kuhakikisha Taasisi zinaongeza ukusanyaji wa mapato kutoka nje ya nchi kupitia kazi za Sanaa ambazo zinazooneshwa katika nje ya mipaka ya Tanzania na kuongeza ushirikiano na Taasisi zenye majukumu yanayofanana nayo.

Wakizungumza kuhusu uzinduzi wa Bodi hizo, Mwenyekiti wa Bodi ya Hakimiliki Tanzania (COSOSTA) Bw. Victor Tesha na Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Dkt. Mona Mwakalinga wamesema watahakikisha linakuwepo jukwaa ndani la kuonesha na kusambaza kazi za Sanaa ndani na nje ya nchi kama ilivyo majukwaa mengine na kusisitiza watasimia kuongeza ubora katika filamu za Tanzania ili zipate soko kubwa zaidi duniani.
IMG-20230912-WA0046.jpg
IMG-20230912-WA0049.jpg
IMG-20230912-WA0050.jpg
IMG-20230912-WA0054.jpg
IMG-20230912-WA0053.jpg
IMG-20230912-WA0045.jpg
IMG-20230912-WA0051.jpg
 
Betting inatengeneza 'pesa ya kutosha'.
Ngumbaru atunge kanuni ya KULAZIMISHA kampuni za betting kutumia 1% ya mapato yao kusaidia yatima, wajane, walemavu, wasiojiweza na wazee.
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amezindua Bodi ya Hakimiliki Tanzania (COSOSTA) na Bodi ya Bodi ya Filamu Tanzania na kuwataka Wajumbe wa Bodi hizo kuhakikisha sekta ya Sanaa inatoa ajira za kutosha na wananchi wanafaidi matunda ya kazi zao...
Hivi bodi ya sanaa ni msanii?
 
Na Eleuteri Mangi WUSM, Dar es salaam

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amezindua Bodi ya Hakimiliki Tanzania (COSOSTA) na Bodi ya Bodi ya Filamu Tanzania na kuwataka Wajumbe wa Bodi hizo kuhakikisha sekta ya Sanaa inatoa ajira za kutosha na wananchi wanafaidi matunda ya kazi zao.

Waziri Dkt. Ndumbaro amesema hayo Septemba 12, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa bodi za taasisi hizo zinajishughulisha na sekta ya Sanaa nchini na kuongeza kuwa wajumbe wa bodi hizo ni wawakilishi wa Serikali katika taasisi hizo.

“Wizara hii ina dhamana kubwa na watekelezaji wa kazi zake ni taasisi zinazosimamiwa na Bodi, kazi yenu ni kuhakikisha taasisi mnazozisimamia zinakua kiuchumi ili kukuza Pato la Taifa na uchumi wa wadau wa sekta yetu ya Sanaa ambayo imekua kwa asilimia 19 ”amesisitiza Waziri Dkt. Ndumbaro.

Awali akimkaribisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro kuzindua Bodi hizo, Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma amewahimiza wajumbe wa bodi hizo kutekeleza wajibu wao ili kuleta uhalisia na utofauti wa utendaji wa kazi wa taasisi hizo kabla ya uteuzi na baada ya kuingia madarakani.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Saidi Yakubu amesisitiza kuwa sekta ya Sanaa nchini imekuwa na Tanzania ni ya pili Afrika ambapo inazalisha filamu 2000 kwa mwaka sawa na wastani filamu sita kwa siku.

Ameongeza kuwa Sekta hiyo imefanikiwa kuzalisha wingi wa filamu na kuwahimiza wajumbe hao kushirikiana na taasisi wanazoziongoza ili kujikita kuzalisha kazi bora ambazo zitakuwa chanzo adhimu cha mapato kwa wasanii na taifa kwa ujumla.

Aidha, Bw. Yakubu amezitaka Bodi hizo kuhakikisha Taasisi zinaongeza ukusanyaji wa mapato kutoka nje ya nchi kupitia kazi za Sanaa ambazo zinazooneshwa katika nje ya mipaka ya Tanzania na kuongeza ushirikiano na Taasisi zenye majukumu yanayofanana nayo.

Wakizungumza kuhusu uzinduzi wa Bodi hizo, Mwenyekiti wa Bodi ya Hakimiliki Tanzania (COSOSTA) Bw. Victor Tesha na Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Dkt. Mona Mwakalinga wamesema watahakikisha linakuwepo jukwaa ndani la kuonesha na kusambaza kazi za Sanaa ndani na nje ya nchi kama ilivyo majukwaa mengine na kusisitiza watasimia kuongeza ubora katika filamu za Tanzania ili zipate soko kubwa zaidi duniani.

WhatsApp Image 2023-09-12 at 15.23.37.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 15.28.17.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 15.26.43.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 15.25.14.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 15.20.26.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 15.06.00.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 15.14.09.jpeg
 
Back
Top Bottom