Umekuna kunako..soma huu mkasa ulionikuta itakusaidia

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mimi ni mtu ambaye nilikuwa siamini katika kumuoa single mother ila baadaye nikajikuta nimekutana na single mother nikaona nitengue msimamo wangu ila kwa hili msimamo wangu narudi kuiheshimu.

Mnamo mwaka huu mwezi wa January, nimekutana na mdada mmoja ambaye tulimaliza naye chuo, na kwa bahati nzuri nilikuwa nasoma naye course moja na pia tulikuwa group moja kwenye discussion. Hivyo na mfahamu kwa kiasi alikuwa ni binti mwenye msimamo kwenye mahusiano.

Kipindi hicho sikuweza kumtongoza kwasababu nilikuwa nipo kwenye stress kubwa wakati nasoma university.

Ila ilikuwa namkubali kubali kiasi, ila wakati tukiwa mwaka wa tatu akakutana na jamaa alikuwa ni graduate na anakazi. Jamaa akafanikiwa kumuweka kwenye himaya yake. Kwangu haikuniumiza sana kwa kwasababu sikuwahi kumtongoza akanitoe nje.

Siku zikaenda jamaa akaenda kujitambulisha kwa binti, ikapangwa mpaka siku ya harusi na vitu kwa hivyo.

Jamaa akawa anahairisha harusi mara kwa mara ila kafanikiwa kuzaa naye mtoto, ila baadaye wakaingia kwenye misuguano wakavunja uhusiano na sababu mwanamke anasema jamaa alikuwa na mwanamke mwingine na mpaka sasa eti jamaa anaishi naye na amezaa naye mtoto, anyway mwanamke akamchukua yule mtoto aliyezaa na jamaa akampeleka kwa wazazi wake.

Mpaka nakutanane naye ameachana na jamaa na kwa takribani miaka mitatu. Anyway baada ya kunieleza hayo kwa uchungu nikaanza naye mahusiano baadaye nikaona kwasababu ni mwanamke ambaye namfahamu kitabia tokea nikiwa chuo acha nifumbe macho nifanye haraku za kuweka ndani kwa heshima.

Anyway baada ya kuanza naye mahusiano akapata ujauzito nikaona ili nisimkweze na aone nipo sereous naye ngoja nikamtambulishe, nikampeleka home kwa utambulisho.

Nikawa nimebakiza kibarua ya kwenda kwao ambaye mpaka sasa sijaenda bado.

Sasa leo akanipigia simu akaniambia amepata msiba, nikamuuliza nani akasema baba mkwe wake wa zamani na waenda na dada yake. Anyway sikutaka kumcrash.

Ila nimeona nipate muda wakutafsiri hiyo picture na kujiuliza maswali mengi.

1. Binafsi najiuliza kama ametoka misri na ameamua kwenda Caana kwanini anarudi nyuma

2. Na kama wameachana na hawakufunga ndoa na ameshatambulishwa katika familia nyingine anaenda kule kama nani...?na kwasababu gani hasa...?

Binafsi nikaona huyu anacheza na akili yangu kwasababu kama yupo sereous
Apo Sasa alafu kwenye kuaga mwili wa marehemu ankwenda na wake wenzie(kundi la wakwe)
 
KWA NINI SINGLE MOTHER WANAOGOPWA KULIKO SINGLE FATHER?

Anaandika, Robert Heriel

Baadhi ya Wadada wamekuwa wakiniuliza iweje Single mother pekee Yao wanaogopwa na Vijana wakiume lakini Single father hawaogopwi na Vijana wakike? Aidha ni Kwa nini Mwanamke mwenye mtoto anapata changamoto kubwa Kupata Mwenza wa kumuoa ukilinganisha na Single father?

Kwa kuongezea, ni kwanini kijana akitaka kuoa single mother atapata upinzani mkubwa kutoka Kwa Wazazi na Ndugu zake na jamii Kwa ujumla? Maswali hayo leo tutaenda kuyajibu Kwa kifupi.

Single mother ni mwanamke mwenye mtoto au Watoto ambaye hajaolewa au aliyepewa Talaka. Huyo ndio single mother. Wakati Single Father ni Mwanaume mwenye mtoto au Watoto ambaye hajaoa au aliyekwisha kupeana Talaka.

Zifuatazo ni sababu za Kwa nini single mothers wanaogopwa zaidi kuliko Single Father;

1. Upendo
Wanawake asilimia 90 wanabeba mimba Kwa wanaume wanaowapenda iwe kwa upendo halisi au upendo wa Mali,
Mwanamke hawezi kuzaa na Mwanaume asiyempenda, Wakati Sisi wanaume suala la kuzaa halipo Chini ya maamuzi yetu.
Sisi wanaume tunaweza bebewa mimba na Mwanamke yeyote hata tusiyempenda, na bahati nzuri au Mbaya wale Wanawake tusiowapenda ndio wepesi kushika MIMBA.

Mwanaume anaweza kutelekeza Mama na mtoto Kwa sababu Hakumpenda Mama na bila Shaka mtoto hakuwa kipaombele chake. Mtoto hawezi kumfanya mwanaume ampende Mwanamke, Ila Kwa upande wa mwanamke mtoto anaweza kumfanya Mwanamke ampende Mwanaume.

Mwanamke analazimika kumpenda mzazi mwenza Kwa MASLAHI ya mtoto, Wakati Sisi wanaume hatunaga kitu kama hicho. Hatulazimiki kumpenda Mwanamke Kwa sababu ya Watoto.

Hii inafanya Single mother kuogopwa Kwa sababu bado wengi wao huwa na bond na Wanaume waliozaa nao Kwa MASLAHI ya mtoto.
Ni nadra Kwa mwanaume kumtafuta Mwanamke aliyezaa naye lakini ni Jambo la kawaida Kwa Wanawake single mother kutafuta Mababa wa watoto Kwa sababu nyingi tuu.

2. HUDUMA KWA MTOTO/WATOTO
SIngle mother wanaogopwa zaidi Kwa sababu wanakuwa wasumbufu kupiga piga simu Kwa wanaume waluowazalisha Kudai Huduma za Watoto. Lakini Hii ni tofauti na single father, mtoto akikaa na Baba yake atahudumiwa na Baba pasipo Mama yake kusumbuliwa.
Yaani haiwezekani single father adai Huduma ya mtoto Kwa mzazi mwenza.

Single mother wengi wanajua ni hasara kubwa kwao kumpa Mwanaume mtoto kwani watakosa mawasiliano na pili wapo wanaopatiemo huduma kupitia Watoto.

Wanawake wengi wanaoolewa na Single father hupendelea huwashauri Waume zao kuwachukua Watoto waishi NAO palepale nyumbani ili kukata mawasiliano baina ya mumewe na Mzazi mwenza, na kama atataka kuwasiliana na mwanae basi simu itapokelewa na atapewa simu mtoto aongee na mama yake.

3. SINGLE MOTHER WENGI KIPAOMBELE CHAO NI WATOTO.
Hii ni tofauti na Single father, wanaume wengi Watoto sio kipaombele Sana ikiwa tuu ataona Mkewe anamheshimu na kumtii. Ndio maana ni kawaida Kwa wanaume kutelekeza watoto. Hilo wala halina mjadala.
Mwanamke yupo connected na watoto wake automatically tofauti na Sisi wanaume.

Single mother wengi kipaombele Chao ni Watoto wao, kila kitu atakiangalia katika jicho la kumlinda mtoto wake, na yupo tayari kufanya lolote kwaajili ya mtoto wake. Hii ni tofauti na Single father, yeye atadili na Familia Kwa ujumla Kwa kumpenda Mkewe na kumpa kipaombele Mkewe kwani yeye ndiye mlezi wa watoto na familia Kwa ujumla.

Single mother hawezi kukupenda kama anavyompenda mtoto au Watoto wake Ila SIngle father anaweza akampenda Mwanamke/Mkewe Mpya kuliko anavyowapenda Watoto wake.

4. DRAMA
Single mother wanadrama nyingi mno ukilinganisha na Single father. Waliooa single mother wamekuwa Watu wanaoripoti visa na mikasa ya kusisimua na kushangaza, tofauti na wanawake walioolewa na single father.

Tabia ya mwanaume ni ileile haijalishi ni single father au sio single father. Haijalishi ni kijana au Mzee. Wanaume Tabia zetu ni zilezile.
Hii ni tofauti na wanawake, Wanawake wapo tofauti tofauti kulingana na umri, maumbile, Elimu, hadhi, mwenye Watoto n.k

I) Mwanamke Bikra hafanan na Mwanamke asiyebikra,
ii) Mwanamke single mother hafanani kabisa na Mwanamke asiyesingle mother, yaani ni jinsia moja lakini wapo tofauti kihisia, Kiakili, kimtizamo na kimaamuzi.
iii) Mwanamke mwenye umri wa miaka 15-25 hafanani na Mwanamke mwenye umri miaka 25-40 na pia hawafanani na Wanawake wenye miaka 41-60 linapokuja suala la mahusiano.

Lakini kijana wa miaka 15-25, 25-40, MTU mzima wa miaka 41-60 wanafanana linapokuja suala la mahusiano.

5. SINGLE MOTHER HUPENDA KUPEWA HESHIMA ILEILE UNAYOMPA MKEO HATA KAMA MMEACHANA. WAKATI SINGLE FATHER HUO MUDA HANA NA SIO AJABU AKAWATELEKEZA HATA NA WATOTO.

Ukioa single mother elewa kuwa kama aliyemzalisha anampa heshima yote kama Mkewe(Kwa jina la Mzazi mwenza) na akawa anawahudumia Watoto wake basi kazi yako kama mume Kwa huyo Mwanamke ni kubwa Sana. Utapata tabu Mno.

Elewa kuwa Mwanamke single mother ndio hulazimisha ukaribu wa mzazi mwenza naye Kwa mgongo WA mtoto. Ila ni ngumu mwanaume single father kutafuta ukaribu na Mwanamke aliyemzalisha. Hakunaga kitu kama hicho.
Ingawaje single mother wanaweza kukuambia kuwa hawasiliani na Mzazi mwenza lakini Kwa Sisi wakulungwa tunasema huo ni Uongo.

Lakini single father akikuambia hajawasiliana na Mzazi mwenza muamini kabisa Kwa sababu Sisi wanaume tunaathiriwa zaidi na MTU aliyekaribu kuliko aliyembali, sio ajabu Mwanaume anauwezo wa kukaa hata mwezi au miezi sita bila kuwasiliana na Wazazi wake lakini Kwa Mwanamke ni tofauti.
Sasa ikiwa mwanaume anauwezo wa kukaa muda mrefu bila kuwasiliana na Mzazi aliyemzaa sembuse Mwanamke aliyemzalisha au sembuse Mtoto?

Lakini Kwa Mwanamke hilo hataweza tena akijua Mwanaume aliyemzalisha anauwezo wa kiuchumi.

Eid Mubarak

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Wewe ni mbaguzi na hoja zako.zimejaa.chuki eitha unataka au hutaki single mother wengi tumeolewa na kwa jinsi wale wenza wetu wa zamani walivyotutenda na kutukatili hatuna hata no zao za simu Wazazi wao ndo tunadeal nao kuhusu watoto Acha kuharibia wengine .
 
Wanaume,
Tatizo kubwa na Wanaume wajinga wengi ni hupenda kujifunza kwa Vitendo(The hard way).

Huwa wanapenda kujiona wao wako special sana kuliko Wanaume waliowaacha hao Single Mothers.

Ila baadae huja kujua hao Wanawake ni Retired War Veteran, bed to bed midfielders. Wamebeba vitu vizito sana moyoni mwao ambavyo wewe huwezi kuvitatua. Leave them alone.

Be a Man.
 
Mahusiano yana mjumuiko wa mambo mengi, moja wapo lililo dogo kuliko ni sex.
Mahusiano yanagusa moyo fikra nasfi na akili.

Akili huhifadhi mambo mengi sana yawe mema au mabaya.

Mahusiano yanaweza kuvunjika kwa nje lakini akilia moyo na nafsi vikashindwa kuvunja, hata kama kulikua na kujeruhiwa kwa namna gani jeraha linapona, jeraha likisha pona akili hurudia kumbukumbu zake .

Ni ngumu sana kuachana moja kwa moja na mtu ulie mpenda kweli.
Ni ngumu kwa kiasi chake, kama sio leo kesho basi hata mtondogoo utamkumbuka tu, hata kama hauta kua na nia mbaya lakini utamkumbuka tu, upande mwingine wa akili ya mantiki ndio inakukumbusha huyu kaolewa au kaoa basi ndio unarudi nyuma , lakini kamwe alie pendwa hasauliki kwa urahisi.
Tuepuke kupenda kwa dhati , walao itapunguza wangi wa changamoto hizi.
 
Hakhj

Hapa umeongea jambo la maana sana .Hichi ulichoandika yapo kwenye ngoma ya mwanamuziki keri hilson inaitwa energy
 
Mahusiano yana mjumuiko wa mambo mengi, moja wapo lililo dogo kuliko ni sex.
Mahusiano yanagusa moyo fikra nasfi na akili.

Akili huhifadhi mambo mengi sana yawe mema au mabaya.

Mahusiano yanaweza kuvunjika kwa nje lakini akilia moyo na nafsi vikashindwa kuvunja, hata kama kulikua na kujeruhiwa kwa namna gani jeraha linapona, jeraha likisha pona akili hurudia kumbukumbu zake .

Ni ngumu sana kuachana moja kwa moja na mtu ulie mpenda kweli.
Ni ngumu kwa kiasi chake, kama sio leo kesho basi hata mtondogoo utamkumbuka tu, hata kama hauta kua na nia mbaya lakini utamkumbuka tu, upande mwingine wa akili ya mantiki ndio inakukumbusha huyu kaolewa au kaoa basi ndio unarudi nyuma , lakini kamwe alie pendwa hasauliki kwa urahisi.
Tuepuke kupenda kwa dhati , walao itapunguza wangi wa changamoto hizi.
Umeongea kitu cha kweli kabisa
 
Wewe nawe hebu lea mtoto wako huko. Unakuta anakutafuta mara kwa mara kukukumbusha kwamba una mtoto maana upo hai na mtoto wako analelewa kwa misaada kama yatima na wewe unadhani anakutafutia kupigana miti
Dear hannah
huyu mwanamke alikuja kwangu akiwa na mimba ya mtu mwingine. Sihusiki kabisa na huyo mtoto

tuliachana sababu ya vurugu za baba mkwe, tena katika hatua za mwisho akielekea kujifungua.

Nilimpenda sana pa1 na kwamba alikuja na mimba ya miezi kadhaa.
 
Back
Top Bottom