Aina ya single mother unayeweza kuingia naye kwenye ndoa

buzitata

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
1,997
7,068
Habarini na poleni na majukumu

Uzi huu nimeandika kutokana na mada mbalimbali nilizokutana nazo zinazohusu mahusiano ya kindoa juu ya single mothers

Kwanza kabisa inabidi nitoe sababu chache za kwanini mwanamke anakuwa single mother.

1. Baba mtoto kukataa mimba au mtoto. Kiukweli hakuna jambo ambalo mwanaume huwa analichukia na kulikwepa Kwa gharama yoyote ile kama kulea mtoto asiye wake ama kusingiziwa mtoto. Mwanaume hakatai mtoto bila sababu mara nyingi inatokana na mwanaume kuona mienendo isiyo mizuri au matukio Fulani kutoka Kwa mwenza wake.. mwanaume akishaona 50/50 za mtoto huwa ni ngumu sana kumkubali mtoto na wengi huwa wanasubiria mpaka pale mtoto atakapokuwa na umri flani Ili waweze kuangalia kama wanafanana nao ndo waweze kutoa maamuzi rasmi.

2. Kipato kutokidhi mahitaji ya mwanamke pamoja na mtoto wake. Mwanaume kama hawezi kutoa huduma stahiki mara nyingi hutelekeza wenza wao na kupelekea mdada kugeuka single mother (hapa nazungumzia wale wanaume ambao hawana jinsi zaidi ya kufumba macho na kuacha maji yajiendeshe yenyew kwenye mkondo wake)

3. Mimba zisizotarajiwa. Hapa naomba wadada watuelewe kidogo, sio Kila mwanaume anayekupenda ama kulala na wewe basi anamalengo na wewe, mwanamke unaweza kuwa mzuri lakini ukawa Bado sio chaguo la huyo mwanaume, kwaiyo uzuri na ndoa ni vitu viwili tofauti.... Zaa na mtu mwenye malengo na wewe. Ni ndoto ya Kila mwanaume kutembea na mwanamke mrembo ila ni wanaume wachache sana ambao Wana ndoto za kuoa wanawake warembo.

3. Historia mbovu ya mwanamke, kama wewe unajijua unahistoria mbovu jitahidi sana usizae, kwasababu huyo mtoto ndo atakua kithibitisho chako Cha tabia mbovu(hapa Kila mtu anaelewa).

Sasa nije Kwa aina ya single mother ambaye wewe mwanaume unaweza kufumba macho na kumuoa japo ubao utakua inasoma 1-0

Single mother ambaye Kwanza mtoto wake amefikisha umri kuanzia Miaka mitano, huyu tunasema tayar mzizi wa upendo na mzazi mwenzake umeanza kulegea ukielekea kukatika kabisa

2. Single mother ambaye hakupewa mimba na mume wa mtu(hapa Sina maelezo ila akili kumkichwa)

3. Jihidi kumjua mzazi mwenzake na ujifananishe naye Ili kuangalia ni vitu gani amekuzidi(wanawake hurudi walipotokea wakikosa vitu ambavyo wanavikosa kwenye mahusiano mapya)...rangi, kimo, uchumi, tabia, pumzi(code)

4.mawasiliano ya single mother na mzazi mwenzie ni mwiko na hayaruhusiwi kama wanataka kujadiliana habari za mtoto kwanini wasingeishi pamoja Ili walee mtoto wao vizuri? Vunja mawasiliano yao ikishindikana waache waendelee na maisha yao, haiwezekani gari Moja lilazimishe kupita Barbara ya mwendo Kasi


5.ikitokea umetoa single mother basi jitahidi kumkalisha fasta fasta Ili kumvuruga akili kwasababu kisaikolojia tunajua mwanamke anakumbuka wanaume wawili tu hapa duniani(aliyemtoa bikra na wakwanza kumkalisha). Rejea Kwa wazee wa zamani ukiona mama aliolewa akiwa na mtoto bas kinachofuata ni kulishwa Kwa haraka mno Ili kukata ule mzizi wa kula tunda kimasihara( zalisha kuanzia watoto watatu ndo unamuacha apumue)

Hayo yote juu hayawahusu masingle mother ambao wakipata ujauzito Kwa kubakwa
 
Kama wewe sio singo baba, tuachie sisi hawa singo maza , kijana mdogo haujua ata kama mbegu zako zimekomaa sawasawa unaangaika na singo maza wa kazi gani ??

Asha kum si matusi lakni
 

Mbona tunawaonea sana single mama? Vipi kuhusu hao waliowazalisha? Maana kuna wanaume wenzetu wana kazi ya kusambaza mbegu tu kama majogoo, wengine wana watoto ila hawafahamu wapo wapi na wanaishi vipi.
 
Back
Top Bottom