Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Fuatilia yanayojiri kutoka Ikulu kwenye Halfa ya utiaji saini wa Mikataba mahsusi 3 ya uwekezaji Bandari ya Dar es salaam, leo Oktoba 22, 2023.


View: https://www.youtube.com/live/N6izYMjIOaI?si=O_YQZdZcwAOJWWpD

MKURUGENZI MKUU WA TPA, PLASDUCE MKELI MBOSSA

Uwekezaji huu wa Serikali kupitia TPA utaongeza ufanisi kwa huduma za meli na shehena, kupunguza muda kwa bandari katika kuchakata nyaraka, kuongezeka kwa mapato ya serikali, kupungua kwa udanganyifu, kuimarisha nafasi ya ushindani kwa bandari, kuongeza ajira na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo kuja bandari ya Dar es salaam.

Aidha, muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka mashariki ya mbali utapungua kutoka siku 30 hadi 15.

Haitegemewi kufungwa kwa biashara zozote za wazawa zinazofanyika bandarini.

Aidha, Mkeli Mbossa amefafanua kuwa wastani wa meli kukaa nangani ikisubiri huduma ni siku 5 hadi 10 huku bandari ya Mombasa ni siku 1.25 na Bandari ya Durban ikiwa ni wastani wa siku 1.6. Hii inatokana na kukosekana kwa uwekezaji mkubwa wa muda mrefu ambao ungepelekea kuongezeka kwa namba za gati. Pia, gharama za kusafirisha makasha ni kubwa, jambo linalofanya kupanda kwa bei ya bidhaa kwa mtumiaji wa mwisho.

Mikataba inayosainiwa leo ni baina ya Nchi mwenyeji, mkataba wa ukodishaji na uendeshaji wa gati namba 4-7 lakini pia kutakuwa na sehemu ambayo gati 0-3 zitaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TPA na kampuni ya DP World kwa shughuli za kibiashara na shughuli za kiserikali.

Mikataba hii haihusishi eneo lote la bandari wala bandari zingine za Tanzania. Upande wa gati namba 8-11, mchakato wa kumpata mwendeshaji mwingine umeshaanza kufanyika na akipatikana mwekezaji mwingine mwenye sifa atakabidhiwa na sio DP World.

Katika mikataba hii, Serikali itakuwa inapata ada na tozo kutoka DPW ambazo zitaongeza mapato na kupunguza gharama za uendeshaji.

Mkataba huu utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wa DPW utakuwa unapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100. Watumishi wa sasa wa TPA watakuwa na nafasi ya kuchagua kubaki TPA au kuhamia kampuni ya DPW.

Pia, mwekezaji atalipa kodi zote za Tanzania kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, sheria za Tanzania ndio zitatumika katika kutekeleza mkataba huu na serikali itakuwa na haki ya kujiondoa kwenye mkataba ikiona inafaa.

SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Rais Samia amesema haikuwa rahisi kufikia makubaliano haya lakini walisikiliza na kufuatilia maoni na hoja za kila mtu hivyo hakuna kundi au sauti ambayo imepuuzwa ambao Serikali iliunda jopo la wataalam kufuatilia maoni hayo.

Kwa ujumla na kipekee kabisa, Rais Samia ameshukuru watanzania wote waliotoa maoni kwani linapokuja jambo jipya ni lazima watu wawe na maoni tofauti.

Amewakaribisha watu wengi zaidi kuja kuwekeza Tanzania ili kuinua uchumi na kupunguza umaskini wa watu.

Mawazo ya wawekezaji wa ndani kupewa bandari ni mazuri na ya kizalendo lakini yapo mbali na uhalisia. Katika kusiani mkataba huu, maslahi mapana ya nchi yamezingatia maslahi mapana ya nchi.

Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
 
Back
Top Bottom