Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,815
- 4,565
UFAFANUZI KUHUSU HALI YA AJIRA ZA WATUMISHI KAΤΙΚΑ BANDARI YA DAR ES SALAAM
Ijumaa 22 Machi, 2024 DAR ES SALAAM
Jumatano tarehe 20 Machi, 2024 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilitoa taarifa kwa Watumishi wake kuhusiana na mabadiliko ya uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, Gati namba sifuri (RoRo) hadi Gati namba saba.
Mabadiliko hayo yanatokana na Mkataba kati ya TPA na Kampuni ya DP World ya Dubai kuhusu uendeshaji na uendelezaji wa Gati namba 0-7 za Bandari ya Dar es Salaam kwa kipindi cha miaka thelathini (30) kuanzia tarehe 22 Oktoba 2023.
Kutokana na mabadiliko hayo katika usimamizi na uendeshaji wa maeneo tajwa, Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam walitakiwa kuchagua ama kubaki TPA au kusitisha mkataba wa ajira na TPA na kuajiriwa na DP World papo hapo.
Menejimenti ya TPA ilitoa taarifa hiyo kwa Watumishi baada ya kukamilisha pro- gramu maalum ya kuwaelimisha na kutoa ufafanuzi wa kina na taarifa sahihi kuhusiana na mabadiliko tajwa kwa Watumishi wake.
Katika taarifa ya Menejimenti, Watumishi watakaoridhia kujiunga na DPW kwa hiyari walielekezwa kuwasilisha taarifa zao (Notice) katika Ofisi zilizopo ghorofa ya 32 katika Jengo la Makao Makuu ya TPA (One Stop Centre) kabla au ifikapo tarehe 29 Machi, 2024. Aidha, Watumishi ambao hawatapenda kujiunga na DP World watabaki TPA kwa kuwa Mamlaka itaendelea kuhitaji Watumishi watakaotoa huduma katika Bandari zake zinazoendelea kuboreshwa katika maeneo mbalimbali Nchini.
Kwa kuzingatia ufafanuzi hapo juu, Menejimenti ya TPA inapenda kuujulisha Umma kwamba, taarifa inayosambaa ilitolewa kwa ajili ya Watumishi na TPA ilifanya hivyo ili kukamilisha taratibu za kuhamisha huduma kwa DP World.
TPA inauhakikishia Umma kwamba, itaendelea kuwathamini Watumishi wake ambao ni rasilimali muhimu zaidi katika Mamlaka na katika utekelezaji wa zoezi hili, maslahi ya pande zote husika yatazingatiwa kikamilifu kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Masoko na Uhusiano,
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (ΤΡΑ)
Habari zaidi, soma: