Wananchi wana hasira mitaaani,maana maisha ni magumu
Kuna waliofukuzwa kwa vyeti feki,ila waliitumikia serikali

Kuna wale ambao biashara zao zimekufa na wamefunga mitaji imekata baada mdororo wa uchumi aliuleta JPM.

Kuna wale ambao kila kukicha polisi wanawamata na kuwabambikizia kesi,huku JPM na Simbachawene hawachukui hatua.

Acha waliobomolewa nyumba zao.

Wote hawa wanaenda kupiga kura za hasira na kama uchaguzi,utakuwa huru na haki tutegemee matokeo ambayo wakata miuno wa Tot watashangaa.
 
Nadhani wapenda haki watapenda kujua remedy ya hao ambao kwa namna moja au nyingine mahakama haikuwatendea haki kutokana na shinikizo la wenye madaraka ya mahakama na serikali/nchi! Mfano akina Fatuma Karume and many others affected persons!
 
Awali nilitangaza kumchagua Magufuli kwa hoja hizi:-
1. SGR
2. Nyerere dam
3. Barabara za mikoa iliyotengwa kama kigoma kwetu ambapo bado km 180 hivi kuunganishwa na lami
4. Kuhamia dodoma

Miradi yote hii mikubwa naamini ni Magufuli pekee ameianzisha na naamini ndiye ataikamilisha kwa ufanisi.

Hata hivyo, kwa kuwa Magufuri ni muumini wa siasa za fujo ama kwa kujua au kutokujua na kupelekea yafuatayo:-

1. Misafara ya Lissu kukosa coverage kama Magufuli
2. Misafara ya Lissu kunyimwa fursa sawa na Magufuli. Magufuli anasimama popote, bila kujali ratiba, Lisu kajaribu kafungiwa
3. Misafara ya Lissu kupigwa mawe, wagombea ubunge kupigwa mawe na wengine kuumizwa, mara nyingi vurugu hizi huratibiwa na ma DC
4. Na manyanyaso yote wanayofanyiwa wasio wa CCM.

Nimeghairi sasa ntawachagua hawa watu. Lengo ni:-
1. Tuone sera zao kwa miaka mitano
2. Katiba mpya
3. CCM na wao wawe chama cha upinzani waone taabu za kuwa wapinzani. Najua chadema wametangaza kutolipiza kisasi.
5. Serikali kamili za majimbo, zinazopatikana kwa ridhaa ya wanachi na siyo maamuzi ya mtu mmoja.
 
Mapendekezo ya tume ya Nyalali ya mwaka 1992 kwa kiasi kikubwa hayakutekelezwa.

Moja ya masharti hayo ni pamoja na CCM kurudisha serikalini mali zote walizokuwa nazo ili mfumo wa vyama vingi uanze vyama vyote vikiwa sawa lakini CCM walikataa kuzirudisha.

Kwahiyo, anza na hilo pamoja na mengine ambayo hayakutekelezwa.
 
Chagua Tundu Lissu Chagua Chadema kwa manendeo yako na ya watanzania wote kwa ustawi wako mfanyakazi, mfanyabiashara na. mhitimu wa Chuo
IMG_20201023_111643.jpg
IMG_20201023_110859.jpg
IMG_20201023_111649.jpg
 
Wakuu salamu ziwafikie popote mlipo.

Uzi huu uwe maalum kwa wote tulioanza kumsapoti Mgombea uraisi Tundu Lisu tangu awali alipoanza kampeni mpaka sasa anaenda mwishoni mwa kampeni.

Uzi huu uwe ni ahadi kwamba tutamalizia kile tulichokianza ambacho ni kumpigia kura huyu jasiri mzee wa uhuru haki na maendeleo.

Binafsi siku hiyo nitatoka kigamboni ninapoishi sasa kwenda hadi kawe nilipojiandikisha ili kuweka vema kwa Tundu Lisu.

Karatasi ya kura majina ya chini kabisa weka vema kunja karatasi weka kwenye boksi . Mungu bariki Uchaguzi, Mungu bariki ushindi wa Tundu A. Lisu, Amen.
Karibuni tujumuike hapa wote.
 
Watumishi wanadai fedha nyingi serikali,lakini licha ya watumishi kumwongelea sana na kumwona kama mwokozi, lakini kutokana na miradi tuliyonayo, pia mipango mengine ya maendeleo.

Je anawezaje kulipa kwa mkupuo na huku akatimiza ahadi za maendeleo na huku kukamilisha miradi tuliyoianza kwa kuingia mikataba wenyewe kwa serikali iliyopita? Tunamjua ni mwanasharia nguli na anajua madhara ya kuvunja mikataba.
 
Back
Top Bottom