Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
24,212
56,894
Lissu niseme wazi leo umegusa maisha ya Watanzania walio wengi.

- Bima ya afya kwa Watanzania wote.

- Hakuna tena kuibia wafanyabiashara maskini kwa kuwatoa elfu ishirini kila mwaka.

- Hakuna tena kukatwa asilimia 15 kisa mkopo. Tutakatwa asilimia tatu tu.

- Elimu ya maarifa, kubadili kabisa falsafa ya Elimu. Elimu ya kutatua matatizo ya maisha yao. Big point here Baba.

In General leo sasa umeongea kama Rais.

Viva Lissu, Viva Tanzania yenye Uhuru, haki na maendeleo ya watu.

====

LISSU LEO UMEFURAHISHA WALIO WENGI, HONGERA SANA

Na, Robert Heriel

Siku ya Leo imeisha vizuri kwa waliowengi, hasa walioisikiliza Hotuba fupi ya Tundu Lisu. Ilikuwa Hotuba iliyobeba matumaini makubwa sana kwa kila mwenye akili.

Lisu amezungumzia mambo makuu yafuatayo;

1. Katiba Mpya
2. Maslahi ya Wafanyakazi
3. Elimu, kubadilisha falsafa katika elimu yetu.
4. Ajira
5. Uhuru katika maendeleo na wala sio utumwa katika maendeleo.
6. Kodi na biashara n.k.

1. Katiba Mpya
Katiba Mpya ile ya Warioba itarudishwa na kupitishwa. Mamlaka ya Rais yataangaliwa na kufanyiwa maboresho kwa kupunguza mamlaka. Katika hili amegusa Watanzania wote. Ni kusema Kila Mtanzania atakayesikia habari hii lazima amuunge Mkono. Labda awe mwendawazimu au mtoto mdogo asiyeelewa mambo ndio atapingana na Tundu Lisu. Katika hili Lisu angepewa Kura 99% na Watanzania kupitia hoja hiyo tuu, 1% wasingempa kura kwa sababu ya uelewa mdogo au wehu.

2. Maslahi ya Wafanyakazi
Lisu hapa angegusa kundi la watumishi wa serikalini, waalimu, manesi, madaktari, Polisi, n.k. Kundi hili lingemuunga mkono kwa 80%, 20% hawa wasingemuunga mkono kutokana na imani yao kuwa ndogo.
Lisu anasema kuwa wafanyakazi hawajaongezwa mishahara tangu 2015. Yeye kasema ataangalia namna ya kufidia ugumu huo, na serikali yake itajali maslahi ya wafanyakazi.
Pia habari ya mifuko ya kijamii, fao la kujitoa, mafao aligusia.

3. Elimu
Lisu hapa kawagusa Watanzania wote kwa ujumla. Hata wajinga hawapendi kuwa wajinga, wanapenda elimu. Hoja hii itaungwa mkono na makundi yote, kuanzia watoto wadogo, mpaka wazee.
Elimu yenye maarifa itakayomjenga mwanafunzi kukabiliana na mazingira pale amalizapo masomo. Sio elimu ya kukabiliana na mitihani shuleni huku kichwa kikibaki kopo

4. AJIRA
Amesema, atahakikisha sekta binafsi zinaendesha shughuli zake veyma kwa kupunguza kodi, na kuweka mazingira rafiki kwa kila atakayetaka kuwekeza mtaji wake huko.
Anafahamu serikali haiwezi kuajiri vijana wote lakini inachoweza kusaidia vijana ni kuwatengenezea mazingira rafiki hasa kwa upande wa kodi ili kuwapa vijana nafasi nzuri ya kujiajiri na kuajiriwa. Hapa kagusa vijana wpte na watu wenye umri wa kufanyakazi.

5. Uhuru Katika Maendeleo na sio Utumwa katika maendeleo
Moja ya mambo anayosisitiza Tundu Lisu ni pamoja na uhuru katika maendeleo. lisu anamtazamo kuwa Maendeleo yanayogusa uhuru wa watu hayo sio maendeleo bali ukandamizaji.
Watu wawe huru kutoa maoni yao, kila mtu awe sawa mbele ya sheria, pasiwepo miungu watu. Hapa kagusa maisha ya watu wote

6. Kodi na Biashara
Kutokana na muda kuwa mdogo Lisu hakuweza kuendelea na kujieleza vyema.

Tumefurahishwa sana na Hotuba yako ndugu Tundu Lisu. Umefurahisha watu wengi

MAMBO YA KUBORESHA

1. MUDA WA UWASILISHAJI
Chadema mjitahidi sana kurekebisha Ratiba zenu kusudi zisimbane sana Mgombea wenu. Angalau Tundu Lisu uanze hotuba zako saa 11:00 na kuzihitimisha saa 12:00. Uwe na Lisaa limoja la kuelezea wananchi kile ulichofanya leo.

2. UPANGAJI WA HOJA
Tundu Lisu jitahidi uanze na hoja zinazoamsha hisia za watu wengi zenye manufaa. Kwa mfano hoja ya Maslahi ya wafanyakazi, ajira, ulinzi na usalama, uhuru, biashara, kilimo n.k Hoja ya kubomolewa nyumba ni nzuri lakini haikupaswa iwe namba moja huku ukijua muda wako ni mdogo. Kumbuka Hoja zote ni muhimu lakini lazima uwe na mpangilio mzuri kulingana na uzito.

3. VYOMBO VYA HABARI
Watanzania sio wajinga, wengi wanafahamu hila mnazofanyiwa. Lakini ni lazima mjitahidi kutafuta utaratibu wa kuhakikisha mikutano yenu inaonekana. Nimeona mna CHADEMA Online Tv, nunueni drone kisha zichukue habari kwa namna ipendezayo.
Fuatilieni ni kitu gani kinafanya mnakata kata pindi mnapokuwa live. Ingawaje hila zinaweza kuhusika.

Hakikisheni mchukua Kamera anaonyesha mambo kwa lengo maalumu. Kamera isionyeshe sehemu moja, hii itaondoa tension ya watazamaji, na hata kamera ikihama hama basi kamareman ajue kwa nini anaihamisha.

4. MICHANGO
Kuna michango ya hali na mali. Mali mmefanya vyema kuwachangisha watu pesa, sasa lazima kwenye suala la hali, mtafute vijana werevu, wenye vipaji vya uhakika, wala sio vya kubeza, Kisha muandae namna ya kufungua mkutano.
Kwa mfano; Jumatatu mtakuwa Arusha, Mnaweza kutafuta vijana chipukizi wenye mapenzi na Chama chenu. Waandalwe kwa siku moja ku-perfome iwe ni igizo, iwe kichekesho, iwe nyimbo. waanze kufanya mambo hayo saa nane mpaka saa kumi. Kisha mambo ya kisiasa yaanze saa kumi mpaka 12. Muhimu hakikisheni mnafanya mambo kisomi, kama watu wenye akili, kwa utaratibu.
Vijana chipukizi ni muhimu kwa sababu kwao itakuwa uwanja wa wao kujitangaza na kuonyesha vipaji vyao,. Sio gharama sana.

5. WATAKAOSIMAMA JUKWAANI
Hakikisheni mnasimamisha watu wanaojua nini wanaongea kwa sababu gani. Kila atakayeongea hakikisheni anawatia hamasa watu, hakikisheni watu wanatamani aendelee kuongea. Kila atakaye ongea awe amebeba ujumbe mahususi, kisha atoe ujumbe wa jumla ambao ni msisitizo kwa kila atakayepanda.

Wasemaji muwagawe katika makundi yafuatayo
1. Watoa ujumbe mkali wenye kuamsha hisia
2. Wachekeshaji na wenye kutia moyo
3. Watoa takwimu na historia
4. Watoa hoja tuli zisizoamsha hisia lakini zinazoingia akilini.

Hakikisheni kila anayepanda anazingatia hivyo. Watu wasijikite kwenye mfumo mmoja tuu. Sio mzungumzaji wa kwanza kaongea kwa kuamsha hisia za huzuni na kusikitisha, na kamaliza hivyo hivyo kisha mzungumzaji anayefuata anaendelea vile vile, hapana, haiwi hivyo. Muweke mambo kimkakati, kama wa kwanza kaumiza hisia za watu, basi anayefuata atoe matumaini kuwa hayo yote yamefanyiika lakini huo ndio mwisho wake, sisi tutafanya a, b, c ......!

6. MASHAMBULIZI
Tumieni muda mchache kushambulia, yaani shambulieni 30% alafu 70% elezeni kwa nini ninyi bora. Kwa mfano mtoa hotuba mwenye lisaa limoja, hakikisha kila baada ya dakika kumi dakika mbili unashambulia adui kisha nane unaonyesha kwa nini wewe ni bora. Muda wa mashambulizi ndio kutupiana vijembe, kejeli, mizaha, mafumbo n.k

7. UMALIZIAJI
Hakikisha unamalizia hotuba zako kwa kuwatia watu changamoto, hasa ukiwaonyesha madhaifu ya adui yako. Kisha uwaachie homework ya kuwataka je hawataki kufanyiwa mambo bora na kuondokana na kadhia hiyo.

MADHAIFU
1. Hoja ya kubomolewa nyumba watu, umeshindwa kuielezea vyema.

Ulipata ukakasi na maelezo yako yalikuwa yanachechemea. Pengine ungeulizwa kwamba ni halali kujenga eneo la barabarani sijui ungejibu nini

2. Hoja ya kupunguza kodi ilikuwa na ukakasi pia
Ukipunguza kodi hasa kwa waagiza mizigo nje ya nchi, huku ukishindwa kueleza namna viwanda vya ndani vinavyozalisha bidhaa zetu vitawezaje kukua, hapo kidogo kuna ukakasi. Kodi na tozo hasa kwa bidhaa kutoka nje hujui ni mbinu ya kulinda viwanda vyetu vya ndani? Kwa upande wa kodi za ndani, hujaeleza ni kwa namna gani serikali yako itapata mapato kwa nji nyingine(vyanzo vipya vya mapato) ili ukipunguza kodi kwa wananchi serikali yako iweze kujiendesha. Umeeleza kwa hoja inayoteleza ubongoni.

3. Muda wako ni mdogo wa kuwasilisha, pengine ungeweza kujieleza katika madhaifu hapo juu kama ungekuwa na muda wa kutosha.
Msijikite kwenye malalamiko, zaidi mjikite kwenye namna mtakazokabiliana na changamoto zinazowakabili. Kama mlivyofanya kwenye suala la michango, hamkulalamika.

Mwisho niseme kuwa, sasa Kampeni ndio zimeanza, nimefurahishwa na Hotuba fupi ya Tundu Lissu.

Kesho nitaeleza Hotuba ya Mhe. Magufuli. Kisha nitatoa muelekeo wangu kuwa nani ninamuona anaweza kuwafurahisha Watanzania.

Zingatia: Sitapendelea mtu. Kile ulichoongea ndicho nitaki-judge na kukitolea muelekeo wangu. Sina Maslhai na chama chochote, sina maslahi na mgombea yoyote. Hakuna watakachoniongezea binafsi. Ninamaslahi na nchi hii. Sitakuwa mnafiki kwa yeyote, sina ninayemhofia.

Tuipende nchi yetu.

Acha nipumzike kwanza, leo sitaki maswali

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300

Kwa kweli tangu juzi kawe, jana segerea na Leo Arusha Tundu Lissu ameanza kutema sera kali kweli
Zinahusu maisha ya mwananchi mmojammoja na Taifa kiujumla
Uzuri wa sera zake kuna zile ambazo ziko specific kwa mji husika na kuna zile ambazo zinahusu nchi nzima

1. Lissu kazungumzia ugumu wa maisha ya mfanyakazi na jinsi atakavyoyaboresha kwa kulipa malimbikizo yote wanayodai na kuwalipa nyongeza zao za mishahara za kisheria(annual increments)

2. Amezungumzia uonevu wanaofanyiwa wafanyabiashara wetu na kwamba ataundoa

3. Amezungumzia kuhusu elimu bora na siyo bora elimu, amezungumzia kuhusu elimu ya ujuzi wa kazi siyo ya kukariri

4. Amezungumzia kuhusu viwanda na kuvutia mitaji ili kutoa ajira kwa vijana wetu

5. Amzezungumzia kuhusu diplomasia yetu iliyoshuka na jinsi atakavyorudisha mahusiano bora ya kimataifa

6. Amezungumzia bima ya afya kwelikweli siyo hii ambayo wazee wetu wakishastaafu wanaambiwa waongeze hela ili waweze kuwekwa kwenye bima ya magonjwa nyemelezi ya wazee

7. Amezungumzia kuhusu kuirejesha Arusha kuwa kitovu cha utalii

8. Amezungumzia kuhusu katiba mpya, ameonyesha ubovu wa katiba ya sasa ambayo imelinyima hata bunge uwezo wa kuanzisha hoja ya namna ya kutumia pesa za nchi isipokuwa tu kama hoja hiyo imeanzishwa na serikali.

9.Amezungumza kuhusu haki za watu, ametetea masheikh walio jela kinyume cha sheria, kwa mfano amesema Arusha peke yake kuna Masheikh 70 wako jela achilia mbali wale masheikh wa uamsho.

10. Amezungumzia kuvunjia wananchi nyumba kikatili etc

11. Kszungumzia mzigo mzito wa makato ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu na amesema atashusha makato hayo kwa mwezi kutoka 15% hadi 3% ya mshahara kwa mwezi

12. Amezungumzia kuhusu adha za vitambulisho vya kimagumashi vya wamachinga amesema ataondoa mzingo wa shilingi 20000 ya kitambulisho cha wamachinga pesa iliyoanzishwa na Bashite na Magufuli

13. Amesema ataanzisha sheria ya haki ya mlipa kodi "Bill of taxpayers rights" ili waweze kulindwa kisheria badala ya utaratibu wa sasa ambao wafanyabiashara wanaonewa sana na TRA na hawana pa kukimbilia, kila wanapokimbilia wameshafungwa minyororo

14. Amezungumzia kuhusu uhuru wa habari, kuwa ataondoa sheria kandamizi zilizotungwa na Magufuli kumlinda yeye badala ya kusaidia taaluma kukua

15. Amesema ataomesha matumizi ya hovyo ya pesa za serikali, siyo rais akiamka asubuhi anajenga uwanja wa ndege kijijini kwake ambapo ndege inatua mara mbili kwa mwaka siku anayoenda kula Christmass na pasaka

16. Lissu anazungumzia kuhusu UHURU, HAKI, MAENDELEO

Kwa kweli Lissu unatisha baba endelea kupiga spana mwana wa Tanzania
Kwenye mikutano yako boresha haya

A) Anza kuwakumbusha wananchi ulaghai wa CCM kwa jinsi ilivyotoa ahadi za uwongo kwa wananchi kwenye ILANI YAO ILIYOPITA NA MIKUTANO YAO YA KAMPENI na hivyo basi wananchi wawakatae kwa sababu hata wanayoahidi sasa hawatatekeleza

1) Wakumbushe wananchi jnsi CCM ilivyoahidi katiba mpya kwenye ilani ya mwaka 2015 lakini Rais Magufuli akakataa baada ya kuapishwa akadai eti hakuinadi kwenye kampeni wakati imo kwenye ilani yao-Waulize wananchi kama wanaweza kuendelea kuwaamini watoa ahadi za uwongo

2)Wakumbushe wananchi ahadi ya CCM iliyoko kwenye ilani yao ya 2015 kuwa watatoa milioni 50 kila kijiji—Mpaka sasa hawajatoa hata thumni, Waulize wananchi wana sababu gani za kuendelea kuamini watu waongo

3)Wakumbushe wananchi namna Magufuli alivyoahidi kugawa laptop kwa kila mwalimu ili imsaidie kuboresha ufudishaji—Waulize wananchi ziko wapi hizo laptop na pia waulize wananchi kwa vipi waendelee kuamini watu wasioishi neno lao?

4) Wakumbushe wananchi namna ilani ya uchaguzi ua CCM ya mwaka 2015 inavyozugumzia kuendelezwa kwa sera ya kilimo kwanza lakini Magufuli alipoingia tu miongoni mwa vitu alivyoanza navyo ni kuifutilia mbali sera hiyo licha ya kuwa ni mpango upo katika ilani yao ya mwaka huo

5. Wakumbushe wananchi jinsi Ilani ya CCM ya mwaka 2015 ilivyosema kuwa watoto watakaopata ujauzito serikali haitowafukuza shule—Wakumbushe jinsi Magufuli alivyoingia madarakani alivyokana ilani yake mwenyewe kwa kusema kuwa hao mabinti wakipata mimba atawafukuza shule za serikali kwa sababu hasomeshi wazazi.

B) Anza kuwaambia wananchi Ulaghai wa CCM ya sasa na hivyo Wasiiamini tena kuipa kura

1. Bashiru aliuambia umma kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu hawatotumia wasanii—Uongo mtupu, leo CCM wamegeuka waandaaji wakubwa wa disco za hadhara, juzi dodoma kulikuwa na wasanii zaidi ya 100. Kwa sababu CCM hawana sera za maana za kushawishi wananchi, wanasafiria nyota za wasanii

2)Wakumbushe wananchi kauli ya Magufuli mwanzoni mwa mwaka huu kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki—Lakini mpaka hivi sasa tangu njama za kuengua wapinzani na kuvuruga uchaguzi ili CCM ipate ushindi wa mezani inaonyesha namna kauli kutoka kwa viongozi wa CCM jinsi zisivyo za kweli.

3)Wakumbushe wananchi jinsi CCM ilivyojifanya kupiga mkwara kuwa haitopitisha watoa rushwa kwenye kugombea, lakini pamoja na hayo wameishia kuteua wagombea wengine waliokamatwa kwa rushwa waziwazi na badala ya TAKUKURU iliyo chini ya serikali kufanya kazi yake, nayo imeacha kutimiza wajibu wake kwa kuwafumbia macho—Waulize wananchi wana sababu gani ya kumuamini Magufuli wakati ameshindwa kusimamia kauli ya chama chake ya awali kuhusu watoa rushwa?. Pia waulize wananchi, iweje wachague chama kuunda serikali, chama ambacho wagombea wake wamepatikana kwa rushwa, Je chama hicho kitaweza kupambana na rushwa na ufisadi wakati hawahawa wanaotegemea kupigana vita hiyo wamepatikana kwa rushwa?

C ) Kila kituo cha kampeni utakachokwenda anza kupre-empt na kuneutralize Talk points za CCM
1. Tafuta rebuttal nzuri sana ya Ishu ya SGR hii usipinge ujenzi wake, pinga namna inavyojengwa, tafuta data za mikopo ya ujenzi wa reli hii na itaavyowatia umasikini watoto wetu kwa sababu ya deni la Taifa kupaa sana. Waonyeshe wananchi kuwa unaunga mkono ujenzi wa SGR ila kwa mpango mbadala (chukua ule mpango wa ACT wazalendo wa kujenga SGR kupitia PPP), na pia mataaluma ya reli tunaagiza nje, tunapeleka mabilioni ya dola nje badala ya kuboresha kwanza Liganga na mchuchuma ili chuma chetu cha ndani ndo kijenge mataaluma hayo, ili pesa hiyo ndefu na ajira zibaki ndani badala ya kuwapelekea wajapan dola hizo na ajira kwao

2. Kuhusu Stieglers, Usiupinge mradi bali pia kosoa namna ya ujenzi wa mradi huo, tafuta data unajengwaje, wananchi wananufaikaje, je kuna technology transfer au tunaishia kuwa wabeba zege na mafundi mchundo tu?. Waambie wananchi kuwa ukiacha Stieglers wewe utajenga Vinu vingine vya umeme kwa kutumia gesi ya Mtwara, umeme utakaokuwa mwingi kuliko utakaozalishwa na Bwawa la Stieglers. Stieglers itazalisha around Megawatts 2000 na ushehe, wewe plan yako ionyeshe utaleta umeme wa gesi mkubwa mara tatu ya huo

3. Kuhusu ndege, hiyo endelea kuponda, piga spana kwelikweli, ni mradi feki

4. Kuhusu kujenga uwanja wa ndege Chato, yaani hii usiiache kila mahali, piga spana, piga nyundo, siliba kwelikweli

5. Kuhusu Elimu bure, waambie wananchi juu ya uwepo wa waraka wa siri wa wakuu wa shule kuendelea kuwachangisha wazazi baadhi ya michango, waambie kuhusu michango ya baadhi ya mikoa wazazi kuambiwa kila mtoto anayeanza kidato cha kwanza aende na dawati lake mwenyewe!. Waambie hii Elimu ni elimu gani wakati mwanafunzi anaambiwa aende na dawati lake. Waambie wananchi kuwa wewe utakuja na mpango mzuri zaidi wa elimu bure tena siyo bure tu bali iliyobora na ikikupendeza mheshimiwa rais mtarajiwa ifanye iwe bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita!. Mpango wako wa Elimu uwe ELIMU BURE NA BORA KWA WOTE! (haya ni maoni yangu binafsi yakikupendeza yachukue)

D). Kwenye kutafuta kura kutoka kwa makundi maalum ya kijamii

1. Kwa waislamu, tumia kauli indirectly kuwa "Sitoteua watu kwa wingi kuliko wangine kwa sababu ni wa imani yangu bali nitateua kwa vigezo na vigezo ninavyovitska vipo kwa watu wa imani zote—Hapa utakuwa umemchapa Jiwe konzi moja nzito mno na Waislamu watakuelewa sana maana teuzi za Jiwe zinanuka udini mno na waislamu linawachukiza sana hilo

2) Endelea kuwasemea Masheikh waislamu, Jana umefanya kazi nzuri sana Arusha kwa kuwasemea Masheikh 70 wa arusha walioko ndani.
Pia endelea kuwasemea Masheikh wa Zanzibar (Usitumie neno Masheikh wa uamsho, hilo neno ni divisive, Tumia tu neno Viongozi wa dini ya kiislamu walioko jela), Wakumbushe waislamu kuwa Magufuli ameshasamehe wafungwa wa kila aina wakiwemo waliofungwa kwa ubakaji lakini anaona tabu kuwaachia Masheikh—Waambie wananchi kuwa ukichaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania utawaweka huru hao masheikh.
(Ukitaka kuwakong'a nyoyo waislamu zaidi, waambie utawalipa fidia hao masheikh kwa kuonewa, kupotezewa muda, kuathiriwa kisaikolojia na kuzitia umasikini familia zao kutokana na vichwa vya familia kuwekwa ndani miaka 6 bila kosa lolote—Kaka ukipiga hii, utapata kura za waislamu haijapata kutokea)

3) Kundi la wanawake, wakumbushe wananchi jinsi Magufuli alivyoteua wanawake wachache mno katika serikali yake kulingsnisha na Kikwete, hii itasaidia kuneutralize soft power ya uwepo wa makamu wa rais mwanamke katika tiketi yake.
Umefanya kazi nzuri kumsiliba Maguful kwa kauli zake tata juu ya wanawake, kauli ile ya jogoo usiiache, endelea kupiga spana, kauli ile ya kupiga mashangazi endelea kupiga nyundo kwelikweli.

Endelea kuwakumbusha wanawake kuwa mwaka 2015 Magufuli aliwaahidi kuwatua ndoo kichwani, yaani akimaanisha kuwaletea maji. Lakini badala ya kuwaletea maji kwa kasi ya kutosha yeye anachukua pesa ananunulia ndege na kujenga uwanja wa ndege Chato

E. Endelea kuwakumbusha wananchi juu ya Ufisadi

Ishu ya Trilion 1.5 zisizo na maelezo yenye mashiko bado ipo kwenye kumbukumbu za wananchi, japo waliunda kamati ya kuwasafisha, lakini maelezo yao hayana mashiko, Endelea kuwakumbusha wananchi juu ya utata wa Trilion 1. 5
Usisahau kuwakumbusha wananchi Jinsi CAG Assad alivyotimuliwa kwa kusimamia taaluma yake ya uhasibu na pia jinsi manunuzi ya ndege yasivyokaguliwa kutokana na Jiwe kuweka ishu za ndege chini ya ofisi ya rais ambayo haikaguliwi na CAG

F. Usisahau ishu ya Maji na Kilimo
Maji bado ni tatizo kubwa, hili umepwaya kidogo, hujaligusia kabisa katika hotuba zako
Pia Kilimo hujakizungumza in details, tafuta mpango mkakati wa kuuza sera zako za kilimo kwa wananchi, waambie wwnanchi serikali yako itakavyowatafutia soko la mazao yao kupitia balozi zilizo nje. Badala ya mabalozi kukaa huko nje na kuuza sura, waanze sasa diplomasia ya kiuchumi ikiwemo kuwatafutia wakulima wetu masoko ya mazao yao ya kilimo.

G. Usiache hata kidogo kuwakumbusha wananchi magumu ya kiuchumi waliyopitia, uwe unawauliza kwenye kia mkutano wako, Je wako tayari kuendelea na mifuko iliyokauka kwa miaka mingine mitano?. Waulize wananchi je bado wanataka kuendelea na vyuma kukaza?. Waulize wananchi kuwa wako tayari kuendelea kukamuliwa na trafiki buku tano tano ili zikang'arishe viatu vya Trafiki? —Waambie wananchi kuwa kama hawataki hayo basi wampige chini Magufuli wakuchague wewe ukarekebishe mambo.

H. Lissu baba, wakumbushe wananchi juu ya adha za faini ya tochi za Trafiki —Waambie wananchi kuwa hutogeuza tochi chanzo cha mapato, bali utaongeza hata speed limit kwenye barabara kuwa 80 hadi 100 kulingana na mahali husika, badala ya 50 hata sehemu zilizowazi kabisa.

Aisee kaka Lissu, Ukiendelea kumwaga sera zako ulizoanza kumwaga kisha ukaongezea na hizi CCM watatafutana!

Piga Spana kaka


HOJA HIZI NDIZO ZITAMUINGIZA LISSU IKULU

Lissu ni kama vile ameshashinda uchaguzi huu kwa hoja zake 7 ambazo zimepata nguvu na kuaminiwa na jamii. Na hii inajidhihirisha maeñeo mbalimbali ambayo amepita kufanya kampeni.

Lissu ni kama vile mhubiri wa injili, kila eneo analopita shetani anapoteza nguvu na neno linabaki mioyoni mwa watu. Maeneo ambayo bado hajapita ndio yamebaki kuzungumzia habari za CCM, lakini yatakapofikiwa na habari njema ya injili ya wokovu na ubatizo wa maji mengi na wao wataachana na CCM.

Hoja 7 ambazo Lissu zimemwongezea nguvu toka kwa makundi mbalimbali ambazo CCM wamekosa majibu yake

1. Vitambulisho vya wajasiliamali
Ni hoja ambayo imepokelwa vizuri na watamzania, kila kona.CCm wameshindwa kujibu hadi sasa, wamebaki tu kudema dema kwenye majibu yao kwamba magufuri anawapenda wamachinga, Mara vitambulisho sio lazima ,wakati wamevitungia na sheria tayari. Lissu shikilia hapo hapo kwa mpaka waeleze ni lini wamachinga walioomba wauziwe vitambulisho visivyo na picha wala jina

2. Maslahi ya watumishi, nyongeza ya mshahara
Hoja ambayo haijajibiwa hadi Leo, na ccm wamekosa majibu wakaeleweka kwa wananchi. . Nyongeza ya mshahara ni takwa la kisheria na sio takwa la mtu . Alisikika Mara moja akisema hajapandisha mshahara ila edhibiti mfumuko wa bei, na akapata majibu yake toka kwa Lissu kwamba bei ya sukari ya 2015 na Leo 2020 ipo sawa, ? "Wananchi hapana" Lissu " anatuambia nini. Baba shikilia hapo hapo wameshalegea na hawana majibu

3. Suala la pension na kiinua mgongo kwa wastaafu
Watu wengi walikuwa gizani na suala lakini baada ya kulitolea maelezo sasa nalo limepata hamasa miongoni kwa watanzania kwamba kuanzia mwakani wastaafu hawatapata pension zao zote baadala yake watapata nusu. Hilo limeonekana kuwa chuki kwa makundi hayo na CCM wameshindwa kutolea majibu ya kueleweka . Lissu shikilia hapo hapo wamesha nyooka tayari

4. Ujenzi wa uwanja wa ndege Chato na hifadhi ya wanyama
Hoja hapa sio ujenzi ,hoja inayoonekana hapa ni namna mradi unavyotekelezwa kwa ufisadi mkubwa wa kupeana tenda na Ndugu yake Mayanga . Mpaka Leo hoja hiyo Magufuli na CCM yake wameshindwa kuitolea majibu, kwa nini aingilie mchakato wa tender na kuagiza apewe ndugu yake na watu sasa huku wanasema ni kama mtu ameamua kupitishia di kwa ndugu yake. Amenipigia pasi kwa mbele ,na suala la hifadhi pia ndio hawana majibu kabisa .Baba Lissu shikilia hapo hapo wamesha nyong'onyea tayari

5. Suala la ununuzi wa ndege
Hii hoja ilianza kwa kasi mwanzoni kunadiwa na ccm lakini baada ya Lissu kuanza kushughurika Nayo wameshakimbia. Lissu amezungumzia masuala ya Faida na mchakato wa ununuzi wa midege hiyo imegubikwa na ufisadi mkubwa na kwamba anayejua ni Magufuri na mjomba wake Dotto James. CCM mpaka Leo wamepoteana na ajenda ya ndege sio ajenda yao tena kwenye kampeni zao. Lissu wabananishe hapo hapo kwenye kona washindwe pa kutokea.

6: Ukosefu wa Ajira kwa makundi mbalimbali
Eneo hili limepata uungwaji mkono mkubwa toka kwa makundi mbali mbali ya vijana. Tangu 2015 ajira zimetolewa kwa walimu wa sayansi na kada za afya. Kada nyingine hazijaguswa kabisa . Hoja yake hapa magufuri imebaki kuwa ni watu wajiajiri wakati yeye mtoto wake Jesca amemwajiri wizara ya mambo ya nje, mwingine amempa RAS iringa .hao walishindwa kujiajiri hadi awaajiri. Watoto wa wanyonge ndio wanaohimizwa kujiajiri. Hapo napo Lissu shikilia hapo hapo pana tija na kundi kubwa la wahanga

7: Waathirika wa vyeti feki
Hii ni hoja ambayo imepata kusemwa na Lissu, kwamba hao walio wa ajiri ni wao ccm na kinachozungumzwa hapa ni watu kufukuzwa kama mbwa bila kupewa mafao yao, ambayo wamechangia kwa miaka mingi halijulikani lilipo enda. Hao ni watanzania wenzetu na sio wakenya wala wamalawi, wamelitumikia na kutufundishia watoto wetu kwa miaka mingi hadi wengine wamekuwa maprofesa. Michango yao ipo wapi kama hawajapewa, Magufuri na ccm yao iliyojaa roho ya kuumiza watu waseme wamepeleka michango yao ya pension waliyokuwa wanachangia kwenye mifuko ya hifadhi

8: Magufuli amesambaza wasiojulikana kila kona
Hii inasababisha watu ukiikosoa tu serikali unakamatwa soon. Wasio julikana inafanya watu tunashindwa kunya wala kukojoa usiku

Nashauri Lissu sasa kwa kuwa kwenye miji yote na vijijini amefanikiwa kuiteka sasa ajikite katika kuwaaminisha watanzania ni namna gani walinde kula zao. CCM wamebaki na mbinu moja tu ya kuwategemea wakurugenzi na NEC, ili wawavushe hapo walipo kwenye tope kwenda nchi kavu. Katika hotuba zake sasa ajikite kuwahimiza wananchi kulinda kura zao, hii ngoma imeshaisha . Wakurugenzi na hawa watendaji kata ambao wamepewa maelekezo marafuku kuwatangaza wapinzani kwenye maeneo yao ndio imekuwa mwiba na Wapinzani wasipo jipanga vizuri mwishoni wataumizwa na hao watu.

Ushauri wangu Lissu sasa ajikite katika kulinda kura. Watendaji wa kata si wa kuchekewa na kuendelea kuachwa kwani kwanza ni watu wa chini mno, lakini ni watu ambao wameshapokea vitisho, hivyo inabidi kazi ya ziada ifanyike. Umati kwa umati Huo Huo wanaojaa kwenye mikutano yao wahimizwe pia wawepo hivyohivyo kwenye kulinda kulinda kura zao kwenye vituo vya kata na ofisi za wakurugenzi. Kwa umati ule wa mwanza wakifanikiwa kukaa kwenye kata na ofisi za wakurugenzi kazi itakuwa imeisha.

Kama una hoja nyingine ambayo unaona bado Lissu bado hajaizungumzia ambayo inaweza kuteka mioyo ya watu iweke hapa ,lakini pia unaweza kupendekeza mbinu sahihi ya kulinda kura

Chaaaaao, tuonane 28 oktoba

Lissu tumia sheria ya fao la kujitoa na ile ya kukata asilimia 15 ya mshahara kulipia deni la HESLB kuwashawishi wananchi wawakatae wabunge wa CCM

Jambo hili naomba leo niliseme kwa mara ya pili kwa faida ya Taifa letu na hasa Watanzania wanaoishi maisha ya kawaida(wenye vipato vya chini na kati) na ambao ndio wengi katika nchi yetu na ambao ndio waathirika wakubwa wa sheria hizi kandamizi.

Ni hivi ndugu zangu, wakati huu wa kampeni,ni muhimu kuwakumbusha Watanzania mifano ya sheria kandamizi zilizopitishwa na wabunge wa CCM kwa mtindo wao wa kusema "ndioooo" bila kujali madhara ya sheria wanazopitisha mradi tu wafanye kile serikali ya chama chao inachokitaka.

Nasema hivi kwasababu, kuna hatari ya watu kusahau mwenendo wa wabunge wa CCM wawapo Bungeni na wakadanganyika na umaarufu wa baadhi ya majina ya wagombea ubunge wa CCM wakati watu hawa wakiwa Bungeni, huwa hawana tofauti na wenzao linapokuja swala la kupitisha sheria zinazoletwa na serikali ya chama chao Bungeni.

Hoja yangu hapa ni kuwa, mbunge wa CCM hata awe ni tajiri au maarufu kiasi gani, huwa hawana ubavu wa kupinga miswaada inayoletwa na serikali ya chama chao Bungeni, bali hushiriki kuipitisha kwa style ya kusema ndioooo!

Hivyo, namuomba Tundu Lissu atumie mifano ya sheria kandamizi zilizopitishwa na wabunge wa CCM kama vile sheria ya kuongeza makato ya Bodi ya Mikopo kutoka asilimia 8 mpaka 15, Sheria ya Fao la Kujitoa, sheria ya Kikokotoo iliyowekwa pending mpaka mwakani(2021) kujenga hoja za kuwashawishi wananchi wawakatae wabunge wa CCM kwani ndio wanaopitisha sheria hizi zinazoumiza wananchi.

Kwa mfano, Lissu anaweza pia kutumia mfano wa Sheria ya Mafuta na Gesi iliyopitishwa kwa hati ya dharura mwaka 2015 kama sikosei wakati wa Bunge la Mama Makinda, kujenga hoja kwa wananchi kwanini wasiwachague wagombea ubunge wa CCM atapokuwa katika kampeni zake mikoa ya kusini.

Si Lissu tu, hata wagombea ubunge wote wa vyama vya upinzani watumie mifano ya sheria hizi kandamizi kujenga hoja na kuwashawishi wananchi wawakate wagombea ubunge wa CCM kote nchini kwani ndio wanatuponza kwa kupitisha hizi sheria kandamizi.

Tunapomuhusisha Magufuli na sheria hizi, tusiache kuwahusisha na wagombea ubunge wa CCM kwani ndio humuwezesha kupitisha sheria za aina hii Bungeni.
 
Ila kitu ambacho Chadema wanatakiwa wakishugulikie haraka Lissu asichelewe kuongea maana muda una kua mdogo na mambo mengi mkutano mwingine aanze kuongea saa 9 ikiwezekana kama atakua na pumzi akichoka apewe wa kumsaidia.

Umesema kweli. Lissu inabidi aongezewe muda, apewe dakika 45 hadi 50 badala ya kupewa dakika 30 tu
 
Back
Top Bottom