Yanayojiri katika mahojiano ya Tundu Lissu Star TV leo Februari 16, 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu yupo Star TV muda huu akifanyiwa mahojiano kwenye kipindi cha The Big Ajenda. Fuatana nami katika uzi huu ambao utamulika baadhi ya hoja zinazoibuka:

TUNDU LISSU KUHUSU LOWASSA NA KESI YA UFISADI

DPP Hakufungua kesi ya Richmond ya Lowassa kwa sababu anazojua yeye
Kwa suala la Edward Lowassa kutokupelekwa Mahakamani ni kwamsingi wa taarifa ya Kamati Teule ambayo ilisema kwamba makosa ya Lowassa na sakata la Richmond ni kutowasimamia watendaji wake.

Huwezi ukatengeneza kesi ya jinai kwa msingi huo kwasababu hakuna kosa la jinai Edward Lowassa alilopewa bali ni kosa la kisiasa. Ambao Kamati ilipendekeza wachukuliwe hatua za kijinai hata wao hawakuchukuliwa hatua za kijinai kwasababu kwa mfumo wetu wa sheria mtu mwenye mamlaka ya kufungua na kuendesha kesi za jinai ni Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali DPP, Yeye ndiye anayeamua nani apelekwe Mahakamani na nani asipelekwe Mahakamani.

Kwahiyo kutopelekwa Mahakamani haina maana kuwa hawakufanya makosa ni kwamba DPP aliamua kwamba hatawapeleka Mahakamani kwasababu anazozijua yeye na hajawahi kuzitaja popote mpaka leo".

Lowassa aliwajibika kutokana na makosa yaliyofanyika
Mimi ndiye niliandika orodha ya Mafisadi na mimi ndiye niliyemuingiza Edward Lowassa kwa mkono wangu kwenye orodha ile. Sidhani kama nilikosea kwasababu nilichokisema kilikuwa na ushahidi wa taarifa ya Kamati ya Mwakyembe na Kamati hiyo ndiyo iliyosema amekosa kwa namna ambayo waliielezea, na wakasema anatakiwa kuwajibika kwa kujiuzulu Uwaziri Mkuu na alijiuzulu.

Kwahiyo mimi sikumuonea niliandika kutokana na Kamati ilivyosema na wakati nafanya naye kampeni niliyasema hadharani kuwa nilimtaja kwenye orodha ya Mafisadi kulingana na taarifa ya Kamati ya Mwakembe kwahiyo hakuna cha kujutia, hayo yalitokea na yatakabakia kwenye rekodi yake"-Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu.

Sababu ya Lowassa kugombea Urais kupitia CHADEMA
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu akijibu ni kwanini walimteua Lowassa kuwania Urais kupitia chama chao anasema:

Kufikia 2015 ilishafikia miaka saba tangu Edward Lowassa ajiuzulu Uwaziri Mkuu ambapo ni kutokea 2008-2015. Miaka saba ilishapita akiwa sio Mbunge, sio Waziri Mkuu na mimi nilikuwa naye Bungeni kuanzia 2010 mpaka 2015 na katika kipindi hicho cha miaka saba akiwa na hilo wingu la Richmond kwenye kichwa chake ukweli ni kwamba ushawishi wake wa kisiasa uliongezeka kuliko alivyokuwa Waziri Mkuu, na kabla hajawa Waziri Mkuu.

Ushawishi wake wa Kisiasa uliongezeka sana. Tulifanya utafiti wa masuala ya uchaguzi kwa kuwaajiri Wataalamu na kwa walivyoona wao suala la ufisadi halikuwa mwanzoni kwa Wananchi bali mwishoni hivyo hiyo ilituonyesha kuwa Watanzania hawatapiga kura kwenye Ajenda ya ufisadi bali Watapiga kura kwenye mambo mengine na hapo ndipo walitafiti kuona viongozi wanaoweza kugombea Urais na kuchaguliwa, katika utafiti wao jina lilijitokeza juu ya mengine ni Edward Ngoyai Lowassa.

Kuwa Mwanasheria Mbobevu sio sawa kuwa na Yesu ambaye anaweza akageuza maji kuwa Mvinyoa au Mfu kuwa mtu hai, hakuna miujiza kwenye sheria. Sijafanya yote hayo kwasababu mimi najua sheria za Tanzania na sio kwasababu nilisahau.

Ninafahamu kuna mambo hayawezekani kabisa kwa sheria za Tanzania. Hii ya 'Private Prosecution' kwenye sheria yetu ya mwenendo wa Jinai ni kweli kuna nafasi ya mtu binafsi kuendesha mashitaka ya jinai lakini katika miaka yote haijawahi kutokea mtu binafsi amefungua mashitaka akaendesha kesi mpaka mwisho haijawahi kutokea kabisa.

KUHUSU MARIDHIANO
Nilihudhuria vikao vya Maridhiano nikasema hapa ni ulaghai
"Mazungumzo ya Maridhiano yamekuja kuitwa ‘maridhiano’ baada ya Mwenyekiti Freeman Mbowe kutoka gerezani, lakini mazungumzo ya kitu gani kifanyike na tunaendaje mbele yalianza wakati Mwenyekiti akiwa gerezani.

Tumeitwa sisi kwenye vikao kuanzia Agosti 2021, Tumitwa kwenye vikao TCD, Baraza la Vyama, tukaitwa kwenye mkutano mkubwa ulifanyika Dodoma na tulikataa katakata tukasema hatuwezi kushiriki vikao mpaka mambo yafuatayo yashughulikiwe na Rais aliyashughulikia ndipo vikao vikaanza mimi nikiwa Ubelgiji na nimerudi nchini nikakuta yalishafanyika hivyo katika vikao vyote vya maridhiano mimi nilihudhuria vitatu lakini nikaona kuna ulaghai kwenye maridhiano na kuna uongo ulikuwa unaendelea ambapo nilisema ndipo baadaye wakaja kutugeuka kwenye majibu yao ya mwisho".

CHADEMA NA MAANDAMANO

Tutaendelea mpaka madai ya Wananchi yatakapotekelezwa
Lissu alikuwa anajibu swali la mtangazaji Aloyce Nyanda aliyetaka kujua hatima ya Maandamano yao anasema:

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antipas Lisu amesema wataendeleza na Maandamano hadi pale madai yote ya Wananchi yatakapotekelezwa na Serikali.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu amesema kabla Lowassa hajahamia kwenye chama chao walifanya Utafiti kwa kutumia kampuni ya Kimataifa kuona mgombea gani kwa vyama vyote ana ushawishi mkubwa

Matokeo yalipokuja Edward Lowassa alionekana ndiye mwenye Ushawishi mkubwa kuliko wanasiasa wote nchini

Baadae wakasikia CCM kuna mvurugano na kuna kampeni za kumzuia Lowassa asigombee hivyo chama Chini ya ofisi ya katibu kikaanza kumfuatilia na kumkaribisha Chamani

Hivyo Dr Slaa ndiye mtu aliyeratibu ujio wa mh Edward Lowassa Chadema

Source: Star tv
 
Tuhuma bila ushahidi ni uzushi , TL anadai ana ushahidi ,kwanini CHADEMA kwanini wako kimya ?

Amekiri mwenyewe kuna uwezekano wa kufungua kesi leo tar 16/2/2024 big AGENDA star TV .

Cc kwa wale waliosema polisi tu ndio wanaruhusiwa .
PXL_20240216_192026976.jpg
 
Tuhuma bila ushahidi ni uzushi , TL anadai ana ushahidi ,kwanini CHADEMA kwanini wako kimya ?

Amekiri mwenyewe kuna uwezekano wa kufungua kesi leo tar 16/2/2024 big AGENDA star TV .

Cc kwa wale waliosema polisi tu ndio wanaruhusiwa .View attachment 2906318
Wewe unafuatilia kweli hii interview ya Tundu Lissu?

Mbona una-portray picha tofauti??
 
Tuhuma bila ushahidi ni uzushi , TL anadai ana ushahidi ,kwanini CHADEMA kwanini wako kimya ?

Amekiri mwenyewe kuna uwezekano wa kufungua kesi leo tar 16/2/2024 big AGENDA star TV .

Cc kwa wale waliosema polisi tu ndio wanaruhusiwa .​
yap kuna nyumbu walisema ni mpaka jeshi la polisi ndio lenye uwezo wa kufungua kesi.Lisu kakata mzizi wa fitna.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu amesema wataendeleza na Maandamano hadi pale madai yote ya Wananchi yatakapotekelezwa na Serikali

Lisu alikuwa anajibu swali la mtangazaji Aloyce Nyanda aliyetaka kujua hatima ya Maandamano yao

Source: The Big Agenda Star tv
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu amesema wataendeleza na Maandamano hadi pale madai yote ya Wananchi yatakapotekelezwa na Serikali

Lisu alikuwa anajibu swali la mtangazaji Aloyce Nyanda aliyetaka kujua hatima ya Maandamano yao

Source: The Big Agenda Star tv
Sawa. Shida wadanganyika vichwa mfu wanapelekeshwa tu kama ng'ombe na CCM
 
hahahaha baada ya muda itazoeleka na watu watarudi kufanya kazi kama kawaida
 
yap kuna nyumbu walisema ni mpaka jeshi la polisi ndio lenye uwezo wa kufungua kesi.Lisu kakata mzizi wa fitna.
Lissu hajakata mzizi wa fitina.........

Yeye amefafanua kuwa ni kweli katika maandishi, ruhusa hiyo ipo, lakini practically Hilo jambo haliwezekaniki.

Akaendelea kufafanua kuwa DPP amepewa madaraka makubwa ya kuweza kufuta kesi yoyote ile na Wala halazimiki kutoa sababu za kuifuta kesi yoyote.

Akatoa mfano wa kesi ya Gekul, aliyetuhumiwa "kumchomeka" chupa sehemu zake za siri kijana wake wa kazi, lakini DPP ameifuta kesi hiyo ya jinai, pasipo kutoa sababu zozote zile!
 
Back
Top Bottom