Naweza kuongea kama utani lakini huu ndio ukweli wenyewe ni suala la muda tu. Sababu kuu za wananchi kumnyima Magufuli kura pamoja baadhi ya miradi mikubwa aliyofanya

1. Polisi kupiga mabomu wananchi.
Hakuna wananchi wa kuchagua serikali inayopiga watu mabomu bure.

2. Ubabe wa Serikali
Serikali ya Magufuli kutumia ubabe katika kila kitu, siyo kufanya siasa siyo kwenye mazao ya wakulima. Ubabe hadi kwa wafanyakazi wa umma

3. Maisha magumu
Hii serikali imeondoa pesa mtaani wananchi hata kupata mlo mmoja ni shida. Walidhani sifa sasa watakiona cha mtema kuni
4.Ubabe kwa Wanufaika wa mikopo elimu ya juu.
Wanafunzi mikopo ya elimu ya juu wanaingia mikataba na bosi wakatwe 13% baada ya kumaliza masomo, lakini kibabe wanakatwa 18% bila ridhaa zao

5. Huduma mbovu za Afya na Elimu.
Hospitali nyingi za serikali bado kinamama wanaenda na vifaa vya kujifungulia. Kwa wakazi wa DSM Nenda pale Temeke hospitali,Mwananyamala,Zinaa na Zakhiem uone hali ilivyo.

Kuhusu elimu sasawalimu wanalia mafungu yanayopelekwa ni madogo hayakidhi mahitaji ya wanafunzi. Shida tupu. Madawati hayatoshi wanafunzi wanakaa chini maeneo mengi tu

6. Uhuru wa vyombo vya habari.
Kwa sasa kila mtanzania anajua kundi hili lilivyonyong'onyea, yaani wanaandika taarifa zao kwa kuvizia vizia kwa kuogopa kutishwa.

7. Viongozi wa dini kutishwa
Viongozi wa watu wansokemea maovu wanatumiwa uhamiaji kuhojiwa uraia ilihali wameishi miaka yote bila kukutana na bughuza zozote. Kwa Serikali hii watu wa Mungu wanasumbuliwa bila sababu.

8. Usumbufu kwa wafanya biashara.
Serikali hii inatakiwa yenyewe kufanya biashara zaidi kuliko watu binafsi, umekandamiza makampuni mengi binafasi na malalamiko watu wengi wanayadikia. Makampuni ya Manji Tanzania mengi yamefungasha virago, kulikua makampuni za ndege kama Fst jet sijui imefia wapi awamu hii.


Suala la kujiuliza ni je Magufuli atapata kura kwa kundi gani lenye mapenzi naye?
 
Kama utabahatika kuulizwa swali "Unataka Haki zipi na Uhuru upi ili kutokana na hiyo Haki na Uhuru uweze kupata Maendeleo unayohitaji na nchi kama nchi inufaike pasina kuvunja Katiba na Sheria za nchi.

Me nimeulizwa mpka sahivi natafuta jibu kama naweza nikacopy na kupaste mnisaidie
 
Kuna Safu ndefu Sana ya wanaomtaka Lissu awe rais kwenye uchaguzi wa oct.28. Miongoni mwa hizo safu Ni Kama ifuatavyo
1. Wana wa Kagera kwenye tukio la tetemeko, Sasa amepatikana mfariji mkuu
2. Wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi, Sasa amepatikana atakayeongeza mishahara na kupandisha vyeo. Wewe Magufuli ulisema "hukuchaguliwa ili upandishe mishahara"
3. Wale watumishi uliowafukuza kazi baada ya uhakiki, Sasa wamempata rais wa mioyo yao atakayewapa kifuta jasho
4. Wafanyabiashara waliofungiwa Biashara na kufilisiwa mitaji, Sasa wamempata rais atakayewasikiliza na kupanga nao Kodi.
5. Wakulima wa chai, korosho, alizeti na kahawa, Hawa wamempata rais atakayewatafutia soko na kamwe siyo kuamrisha jeshi kuteka korosho yao na kuingilia taratibu za mauzo.
6. Wanaosaka ajira, Hawa wamempata rafiki mwema atakayesimamia sekta binafsi na siyo kubuni vitambulisho visvyo na tija
7. Wanahabari, Hawa wamempata rais anayekubali kuhojiwa na kuelezea makusudio yake juu ya nchi na nje ya nchi' bila kuwatishia, kuwafungia vyombo vyao na kuwapoteza
8. Wote waliobaguliwa kutopewa maendeleo kwa kuwa walichagua vyama vya upinzani, maendeleo hayana vyama ukipenda utakutana na vitu 3, Uhuru, Haki na maendeleo
9. Wanafunzi wanaolilia mikopo ya kujiunga vyuo vikuu na wale waliomaliza lakini Kodi imepandishwa kwenye mikopo yao
10. Wanaowalilia ndugu zao kwa kutekwa, kuumizwa na kuuliwa na watu wasiojulikana
11. Wafugaji waliotaifishiwa mifugo yao
12. Wavuvi waliochomewa nyavu na kuharibiwa zana za kuvulia samaki
Meza Ni ndefu, yawezekana listi Ni ndefu. Lakini Hawa ndio hawstakichagua CCM na badala yake kamwe kura yao watapeleka kwa lissu
 
BREAKING NEWS
LISSU , MBOWE HALI SI SHWALI CHADEMA

Habari kutoka vyanzo vya ndani zinaeleza kuwa mambo sio shwari ndani ya CHADEMA kufuatia Mwenyekiti Freeman Mbowe kushawishi Kamati Kuu ikubali hukumu ya Kamati ya Maadili kinyume na mapendekezo ya Lissu aliyetaka CHADEMA isikubaliane na itangaze mgogoro.

Wadadisi wa mambo wanadai kuwa chama hicho kwasasa kinasumbuliwa na mambo mawili; kwanza ni Mbowe anahofia umaarufu wa Lissu kwa upande mmoja na Lissu kutokumuamini Mbowe kwa upande wa pili kiasi ameshindwa kumweleza wadau wa nje wanaoleta pesa za kampeni ni akina nani kitu ambacho Mbowe anaona nikama anazungukwa kama Mwenyekiti.

KIBARUA KIMEANZA KUOTA NYASI

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
*Mbowe kwa hili la vyama, unafanya ukaburu*

Na Mwandishi wetu

CHADEMA ni chama kinachojinasibu kwamba kinatetea uhuru wa kujieleza, kwamba ni chama ambacho kikiigia madarakani kitadumisha demokrasia, na kimekuwa mstari wa mbele kushutumu serikali kwamba inaminya hiyo demokrasia wanayoitaka na kuahidi kuitetea.

Lakini Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, akiongea na waandishi wa habari kuhusu adhabu ya mgombea wao kusimamishwa kampeni kwa siku saba, amesema kwa ujasiri kabisa kwamba kati ya vyama 15 vyenye wagombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu, vyama vingine vya upinzani vinamnyima haki mgombea wake wa urais, kwa sababu vyama hivyo havina msingi wala sababu ya kuwepo.

*_”Msijaze akilini mwenu kwamba kuna vyama vya siasa hapa, ni vitaasisi vinavyotafuta maslahi kupitia jukwaa la siasa, ndiyo wanaovuruga demokrasia katika taifa hili ni maadui wa demokrasia. Vinatupa shida kupanga ratiba yetu, tunaweza kuomba mgombea wetu (Tundu) Lissu arudi Morogoro tunaambiwa pale kuna chama cha TADEA, mnataka kwenda Iringa mnaambiwa kuna chama kinaitwa SAU. Vyama hivi vinamyima haki mgombea wetu mwenye mamilioni ya wafuasi.”_*

Wakati Mbowe akisema haya, Ilani ya Chadema ya mwaka 2020, katika utangulizi wake imenukuu moja ya vipaumbele ni kusimamia utekelezaji wa madhumuni ya chama hicho kama yalivyoainishwa katika Ibara ya 4.1.4 ya Katiba ya Chadema kwamba;

*_”Kuendeleza na kudumisha Demokrasia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kujenga utamaduni wa demokrasia katika jamii kwa kutambua haki za wengi katika maamuzi; na pia kutambua haki za wachache kusikilizwa, kuheshimiwa na kulindwa, sambamba na kukubali ushindani huru, wa haki na wa wazi katika uchaguzi.”_*

Kauli ya Mbowe inazungumzia demokrasia gani kuhusu vyama vingi? Kwamba kwa Chadema demokrasia ya vyama vingi ni haki kwa chama chao na mgombea wao, vyama vingine vyote havina haki hiyo?

Inatisha kidogo wakati madhumuni ya Katiba ya Chadema yaliyofanywa kipaumbele kwenye ilani ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu inasema kudumisha demokrasia, kutambua haki ya wengi na haki ya wachache kusikilizwa, kulindwa na kuheshimiwa,
*_ameonyesha rangi zake halisi wasivyo na uvumilivu na walio kinyume chao._*

Mbowe na Chadema tafsiri yenu ya kuhesmimu na kulinda haki za wachache ni ipi? Mlitaka nini! Tume ya Uchaguzi isivipangie vyama hivi ratiba ya kampeni wakati vina wagombea walioomba nafasi ya kugombea kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa.

Najaribu kufikiria serikali ya Chadema ingekuwa na uvumilivu kiasi gani katika mfumo huu wa vyama vingi, sasa hivi mkiwa wapinzani tayari mnaona mna haki zaidi kuliko vyama vingine vyote, itakuwaje mkionja mamlaka?

Kwa maana nyepesi kabisa Mbowe anatuambia kuwa wanachama wa Chadema ndiyo Watanzania wenye haki zaidi kuliko wa NCCR – Mageuzi, CUF, TADEA na wasiokuwa na vyama.

Huu ni ukaburu kama ulivyo ukaburu mwingine, ni ubaguzi hatari kwa taifa letu, ambao hauna nafasi katika taifa hili.

*Magufuli mitano tena*
 
MJADALA UNGELITAKIWA UWE KUMUONGEZEA MUDA JPM NA SIO KUOMBANA KURA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kuna siku niliwaambia wenzetu huko nje wakiona wamepata kiongozi mwenye maono huwa hawamwachii kwa haraka.

Niliwahi kuwaambia kuwa Urusi wao kwa kutambua Mchango wa Putin waliamu kubadilisha katiba yao badala ya Putin kustaafu 2024 walimuongezea muda mpaka 2036. Bunge la Urusi lilipitisha kipengele hicho Cha kumuongezea muda Putin kwa kishindo. Warusi wanaona kuwa ili maono ya Taifa lao yakamilike lazima pale juu awepo mtu mbishi Kama Putin na asiyeyumbishwa na mataifa Mengine.

China wao mwaka 1990 kwenye katiba yao walipitisha kuwa kila Rais atastaafu baada ya miaka 10 akiwa madarakani. Lakini mwaka juzi waliamua kubadilisha kipengele hicho kwa kuhofia kumpoteza Xi Jinping wameamua kugusa Katiba yao na Sasa atakaa madarakani Hadi Kifo kitakapomchukua. Jinping alikuwa astaafu 2023 kwa mujibu wa katiba kabla hawajaigusa.

Nimekuwa nikiwaleta maajabu ya Serikali ya awamu ya Tano kila Mara leo tuguse kipengele Cha Elimu kwa miaka mitano Nini kimefanyika.

1. Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani iliamua kufuta kabisa ada kwa wanafunzi wote wa kuanzia awali Hadi kidato Cha nne. Mpaka kufikia February 2020 Serikali ilikuwa imeshatoa shilingi trilioni 1.01 kugharamia Elimu bure. Ni nchi pekee kwenye ukanda wetu huu iliyoweza kutoa Elimu bure.

2. Serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kuongeza shule za primary toka 16,899 zilizokutwa 2015 Hadi kufikia 17,804.

3. Kwa upande wa Shule za Sekondari zimeongezwa Kutoka 4,708 Hadi 5,330.

4. Serikali imefanya Ukarabati wa shule kongwe 73 Kati ya 89. Ukarabati huu kila pembe ya nchi mnauona unavyitafuna mabilioni ya shilingi.

5. Serikali ya awamu ya tano imefanya Ujenzi wa mabweni 253 ya shule za Serikali.

6. Serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kufanya Ujenzi wa Maabara 227 katika shule mbalimbali nchini

7. Serikali ya awamu ya tano imetoa vifaa vya Maabara zipatazo 2,956.

7. Madawati JPM aliyokuta yalikuwa 3,024,311. Ameyaongeza Hadi kufikia 8,095,207 sawa na asilimia 200 ya ongezeko.

8. Vyuo vya ualimu 18 vimejarabaitiwa. Vyuo hivi vilielekea kuwa magofu. Hii Ni kazi ya Serikali ya awamu ya tano.

9. Vyuo viwili vimejengwa upya Murutunguru na Kabanga. Kazi hii imefanyika ndani ya miaka mitano.

10.Zimegawanywa computer 1,550 kwenye vyuo 35 vya ualimu nchini.

11. Vyuo vya ufundi VETA vimeongezwa toka 672 mwaka 2015 Hadi 712 mwaka 2020

12.Bajeti ya mikopo ya Elimu ya juu imeongeza toka Bilioni 348 kwa mwaka Hadi Bilioni 450.

Sisi tunaoelewa Nini kimefanyika usituulize kwa nn tunataka JPM aongezewe Muda.

Usituulize kwa nn tunataka JPM achaguliwe Tena.

Narudia Yale mazuri ya Upinzani yatachujuliwa na ikiwezekana wale wenye uwezo mkubwa kichwani wanaweza kuchukuliwa wakalijenge Taifa lao.

Duniani hakuna nchi ambayo imewahi kumaliza Changamoto zake zote. Lakini mnapopata mtu wa kupambana nazo Kama JPM sio wa kumwachia haraka.

Ole Mushi
0712702602.

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Kama hafai mbona mwenye chama alimwamini kugombea?. Kura alizopata lowasa, Lissu hata nusu hata pata.
Lissu niseme wazi leo umegusa maisha ya Watanzania walio wengi.

- Bima ya afya kwa Watanzania wote.

- Hakuna tena kuibia wafanyabiashara maskini kwa kuwatoa elfu ishirini kila mwaka.

- Hakuna tena kukatwa asilimia 15 kisa mkopo. Tutakatwa asilimia tatu tu.

- Elimu ya maarifa, kubadili kabisa falsafa ya Elimu. Elimu ya kutatua matatizo ya maisha yao. Big point here Baba.

In General leo sasa umeongea kama Rais.

Viva Lissu, Viva Tanzania yenye Uhuru, haki na maendeleo ya watu.

====
Zt
 
Ukimsikiliza Lissu. Ukiendelea kumsikiliza Lissu ni wazi utaona kwamba Lowassa 2015 hakuwa mgombea bali alikuwa mzugaji. Huyu jamaa wa sasa ana akili iliozidi, the man is genius. Katika press release yake ya leo Arusha aisee huyu ndio mgombea tuliokuwa tunamwitaji. Mimi ni CCM damu damu but namkubali Lissu na anavyosaidia kunyosha mambo...
mim sina chama ila toka nianze kumsikiliza sijaskia mahala zaidi ya kubishana na kujifanya ujuaji.sisikii sera yoyote zaidi ya uhamasishaji wa vurugu.
 
Kwako mh Tundu Lissu

Ni vyema uwakumbushe na kuwatahadhalisha Watanzania wakati wa kampeni zako kukwepa kuwarudisha madarakani watu wanaosaka madaraka kwa njia za ulaghai.

Mathalani kuna hii ahadi ya mwaka 2015 ya mgombea wa CCM ya kutoa sh milioni 50 kwa kila kijiji ambayo haijatekelezwa hadi leo. Watanzania tumwamwini tena kwa lipi mtu mwenye ahadi kama hizi?

Sasa leo amenukuliwa akitoa ahadi za jumla jumla zenye mfananio na hii ya 50M (check screenshot hii hapa chini).

Utakapo resume kampeni zako hapo kesho, hususani maeneo ya huko vijijini, hii spana unatakiwa kuipiga sana ili wapiga kura wasimchukulie serious tena mgombea wa CCM kwa ahadi zake mpya ambazo ni dhahiri anazitoa kwa ajili ya kuombea kura tu, na baada ya hapo wakifanya kosa kumchagua atarudi kwao na vijembe na kejeli kama kawaida yake.


1602245872648.png
 
Maneja kampeni wa Lissu pamoja na kwamba mgombea urais anaendelea kufanya vyema nakuomba umkumbushe aongelee na vifaa vya ujenzi mfano, siment, bati, nondo hazishikiki kwa bei ni kubwa sana na wananchi tunahangaika sana.
Hii ndiyo sababu ya chadema kushindwa kujenga ofisi ya chama?
 
Maneja kampeni wa Lissu pamoja na kwamba mgombea urais anaendelea kufanya vyema nakuomba umkumbushe aongelee na vifaa vya ujenzi mfano, siment, bati, nondo hazishikiki kwa bei ni kubwa sana na wananchi tunahangaika sana.
Lisu anajua hayo yote
 
Maneja kampeni wa Lissu pamoja na kwamba mgombea urais anaendelea kufanya vyema nakuomba umkumbushe aongelee na vifaa vya ujenzi mfano, siment, bati, nondo hazishikiki kwa bei ni kubwa sana na wananchi tunahangaika sana.
Swadakta
 
Back
Top Bottom