Tundu Lissu: Tume ya Uchaguzi sio Huru, ni Tume ya Rais

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,455
8,292

“Ukiangalia taarifa ya watazamaji wa uchaguzi wa kitaifa na kimataifa tangu mwaka 1995 wote wamesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru, na wamesema siyo huru kwa sababu, moja ni tume ya Rais kwa maana kwamba wajumbe wake wote ni wateule wa Rais , mtendaji wake mkuu ni mteule wa Rais, watumishi wake wote ni watumishi wa serikali,"

"Kwa Katiba yetu watumishi wa serikali ni wateule wa Rais au wanafanya kazi kwa niaba ya Rais na Rais ndiye mamlaka yao ya nidhamu. Kwa hiyo wote waliotazama uchaguzi, wa kimataifa na kitaifa wamesema kwa kigezo hicho cha kwanza cha mamlaka ya uteuzi hii siyo tume huru'

"Tume ya Warioba ilifanya kazi kubwa sana ya utafiti kwenye hili suala la Tume ya Uchaguzi, kuna juzuu nzima ya Tume ya Warioba kuhusu masuala ya uchaguzi wa nchi yetu na ililiangalia hili suala kwa undani sana, na tume ya Warioba vilevile ilisema hii tume siyo huru kwa sababu ni tume ya Rais , wajumbe wake wote ni watumishi wa Rais , Mtendaji Mkuu ni mtu wa Rais, watumishi wote ni watu wa Rais na katika utendaji wake haina uhuru wowote”- Tundu Lissu."

“Watumishi wa tume, wajumbe wa tume wote na watumishi wake wote kuanzia msimamizi wa kituo mpaka Mwenyekiti wa Tume mamlaka yao ya nidhamu ni Rais, wasimamizi wote wa chaguzi (Wasimamizi wa uchaguzi ni wale wanaotangaza matokeo kwenye majimbo), wakurugenzi wote ni wateule wa Rais na wanaondolewa na Rais, kwa hiyo kwenye suala la uwajibikaji wa wajumbe na watumishi hii si tume huru ni tume ya Rais, na mwisho kwenye masuala ya fedha tume huru inakuwa na utaratibu tofauti wa kupata fedha zake kutoka serikalini, tume inakuwa na bajeti yake yenyewe na hiyo bajeti ikipitishwa, tume inakuwa na mamlaka kamili na ya kipekee ya kutumia hizo fedha tume, haiendi kupanga foleni kwenye ofisi ya TAMISEMI au Ofisi ya Waziri Mkuu au Ofisi ya Rais kupata mgao ili iendeshe uchaguzi au iandikishe wapiga kura, inatakiwa isimamie fedha zake kama zilivyopitishwa kwenye bajeti bila kutegemea mamlaka nyingine"

“Kwa mujibu wa katiba yetu tume ina uwezo wa kutengeneza majimbo ya uchaguzi lakini lazima ipate ridhaa ya Rais, kwa maana nyingine ni kwamba Rais asipotoa ridhaa tume haina uwezo wa kutengeneza majimbo ya uchaguzi, sasa kwa wasiofahamu wanaweza wasielewe umuhimu wa suala hili, chaguzi huwa zinaanza kushinda au kushindwa kwenye utengenezaji wa majimbo, kuna ‘uchafu’ mwingi kwenye utengenezaji wa majimbo ya uchaguzi katika nchi yetu na haya ni maneno ya waangalizi wa uchaguzi zetu tangu mwaka 1995, tume haina uhuru wa kutengeneza majimbo , kimsingi majimbo yanatengenezwa na Rais na watu wake kwa sababu, Rais asipotoa ridhaa hakuna kinachofanyika"

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara Tundu Lissu amezungumza hayo Ijumaa, 12 Aprili, 2024 katika kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na kituo cha habari cha Clouds FM.

====================================

The Warioba Commission conducted extensive research on the issue of the Electoral Commission. There is a whole volume of the Warioba Commission dedicated to the electoral matters of our country, and it examined this issue in great detail. The Warioba Commission also stated that this commission is not independent because it is the President's commission. All its members are presidential appointees, the Executive Director is appointed by the President, and all its staff are presidential personnel. In its operations, it lacks any independence. - Tundu Lissu.
 
Chadema ni waramba asali mara munamsifu mama na kumtukuza, hamuishi vikao na Samia Ikulu, mulisema Chadema hatapiga magoti kwa serikali ya ccm, hatimae Tundu Lissu alimualika mama belgium bila kuweka wazi hadi leo waliongea nini belgium, lakini mbowe alipotoka jela breki ya kwanza Ikulu, alibadilisha koti na tai akiwa Ikulu ndio akaenda nyumbani kwake sasa mnalalamika nini.

Mmeramba asali sasa wanaoumia ni wananchi, Tundu Lissu haya anaongea sio kutoka moyoni ni kama anamfurahisha mfalme, chadema sasa ni CCM B hawaeleweki, Zamani chadema ikitetea Zanzibar huru sasa wanawatukana wazanzibari waziwazi baada mama kuwa Rais, Chadema haieleweki

Nafkiri Tanzania vyama vya upinzani hasa Chadema kimekosa muelekeo, Watanzania wanahitaji upinzani mpya usio na unafiki ndani yake, Chadema muda wake umekwisha, Mbowe sasa anakazia suruali tu muda wote Ikulu hana tena habari ya Katiba wala Tume huyu ya Uchaguzi. Mbowe siye tena yule wa zamani kwisha habari yake.
 
Anapofanya vizuri sio vibaya akasifiwa na kutiwa moyo ili afanye vizuri zaidi.

Chadema sio wanafiki akifanya vibaya wanamkumbusha tena kwamba hapa Mama sio poa.
Na huo ndio uungwana
 
“Ukiangalia taarifa ya watazamaji wa uchaguzi wa kitaifa na kimataifa tangu mwaka 1995 wote wamesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru, na wamesema siyo huru kwa sababu, moja ni tume ya Rais kwa maana kwamba wajumbe wake wote ni wateule wa Rais , mtendaji wake mkuu ni mteule wa Rais, watumishi wake wote ni watumishi wa serikali,"

"Kwa Katiba yetu watumishi wa serikali ni wateule wa Rais au wanafanya kazi kwa niaba ya Rais na Rais ndiye mamlaka yao ya nidhamu. Kwa hiyo wote waliotazama uchaguzi, wa kimataifa na kitaifa wamesema kwa kigezo hicho cha kwanza cha mamlaka ya uteuzi hii siyo tume huru'

"Tume ya Warioba ilifanya kazi kubwa sana ya utafiti kwenye hili suala la Tume ya Uchaguzi, kuna juzuu nzima ya Tume ya Warioba kuhusu masuala ya uchaguzi wa nchi yetu na ililiangalia hili suala kwa undani sana, na tume ya Warioba vilevile ilisema hii tume siyo huru kwa sababu ni tume ya Rais , wajumbe wake wote ni watumishi wa Rais , Mtendaji Mkuu ni mtu wa Rais, watumishi wote ni watu wa Rais na katika utendaji wake haina uhuru wowote”- Tundu Lissu."

“Watumishi wa tume, wajumbe wa tume wote na watumishi wake wote kuanzia msimamizi wa kituo mpaka Mwenyekiti wa Tume mamlaka yao ya nidhamu ni Rais, wasimamizi wote wa chaguzi (Wasimamizi wa uchaguzi ni wale wanaotangaza matokeo kwenye majimbo), wakurugenzi wote ni wateule wa Rais na wanaondolewa na Rais, kwa hiyo kwenye suala la uwajibikaji wa wajumbe na watumishi hii si tume huru ni tume ya Rais, na mwisho kwenye masuala ya fedha tume huru inakuwa na utaratibu tofauti wa kupata fedha zake kutoka serikalini, tume inakuwa na bajeti yake yenyewe na hiyo bajeti ikipitishwa, tume inakuwa na mamlaka kamili na ya kipekee ya kutumia hizo fedha tume, haiendi kupanga foleni kwenye ofisi ya TAMISEMI au Ofisi ya Waziri Mkuu au Ofisi ya Rais kupata mgao ili iendeshe uchaguzi au iandikishe wapiga kura, inatakiwa isimamie fedha zake kama zilivyopitishwa kwenye bajeti bila kutegemea mamlaka nyingine"

“Kwa mujibu wa katiba yetu tume ina uwezo wa kutengeneza majimbo ya uchaguzi lakini lazima ipate ridhaa ya Rais, kwa maana nyingine ni kwamba Rais asipotoa ridhaa tume haina uwezo wa kutengeneza majimbo ya uchaguzi, sasa kwa wasiofahamu wanaweza wasielewe umuhimu wa suala hili, chaguzi huwa zinaanza kushinda au kushindwa kwenye utengenezaji wa majimbo, kuna ‘uchafu’ mwingi kwenye utengenezaji wa majimbo ya uchaguzi katika nchi yetu na haya ni maneno ya waangalizi wa uchaguzi zetu tangu mwaka 1995, tume haina uhuru wa kutengeneza majimbo , kimsingi majimbo yanatengenezwa na Rais na watu wake kwa sababu, Rais asipotoa ridhaa hakuna kinachofanyika"

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara Tundu Lissu amezungumza hayo Ijumaa, 12 Aprili, 2024 katika kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na kituo cha habari cha Clouds FM.
Kweli hongera sana Mh.Lissu.
 
Chadema ni waramba asali mara munamsifu mama na kumtukuza, hamuishi vikao na Samia Ikulu, mulisema Chadema hatapiga magoti kwa serikali ya ccm, hatimae Tundu Lissu alimualika mama belgium bila kuweka wazi hadi leo waliongea nini belgium, lakini mbowe alipotoka jela breki ya kwanza Ikulu, alibadilisha koti na tai akiwa Ikulu ndio akaenda nyumbani kwake sasa mnalalamika nini.

Mmeramba asali sasa wanaoumia ni wananchi, Tundu Lissu haya anaongea sio kutoka moyoni ni kama anamfurahisha mfalme, chadema sasa ni CCM B hawaeleweki, Zamani chadema ikitetea Zanzibar huru sasa wanawatukana wazanzibari waziwazi baada mama kuwa Rais, Chadema haieleweki

Nafkiri Tanzania vyama vya upinzani hasa Chadema kimekosa muelekeo, Watanzania wanahitaji upinzani mpya usio na unafiki ndani yake, Chadema muda wake umekwisha, Mbowe sasa anakazia suruali tu muda wote Ikulu hana tena habari ya Katiba wala Tume huyu ya Uchaguzi. Mbowe siye tena yule wa zamani kwisha habari yake.
Kwani kuonana na Rais wako ni dhambi?Hivi vilaza ninyi mtaelimika lini?Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania ni Rais wa Watanzania bila kujali vyama vyao,dini zao.makabila yao,koo zao,itikatidi zao.Hili jambo la uadui kwenye siasa alileta Magufuri na ndiyo maana hakudumu kwenye kiti cha Urais kwa sababu Amani na Mshikamanao ndiyo nguzo ya taifa hili.
 
View: https://youtu.be/ljxewLnNRZY?si=tkKVfn11d4uoRAHH

Wenye tume yao wameipachika jina la Kingereza wakidhani ndio itakuwa huru😂😂

Tume Huru ya UchaguziTz, ni huru na itaendelea kua hivyo regardless ya maoni na mtazamo wa wachache wanaona sio huru 🐒

daima maoni yao yataheshimiwa huku yale ya wengi ambayo ndio katiba yenyewe sasa, ikiendelea kutekelezwa bila kuinajisi hata sheria moja 🐒

Katiba ni ya waTanzania, taasisi za uma ni za waTanzania na zinafanya kazi kwa kutokana na matakwa ya wengi kwa maslahi mapana ya wanainchi walio wengi, lakini kwa maslahi mapana ya waTanzania wote. wachache wanabaki kuskizwa na kuheshimika sana 🐒
 
Tatizo lako unahangaika na neno Huru baadala ya sifa za kuwa huru. Acheni uchawa kwenye mambo ya msingi.
 
Chadema ni waramba asali mara munamsifu mama na kumtukuza, hamuishi vikao na Samia Ikulu, mulisema Chadema hatapiga magoti kwa serikali ya ccm, hatimae Tundu Lissu alimualika mama belgium bila kuweka wazi hadi leo waliongea nini belgium, lakini mbowe alipotoka jela breki ya kwanza Ikulu, alibadilisha koti na tai akiwa Ikulu ndio akaenda nyumbani kwake sasa mnalalamika nini.

Mmeramba asali sasa wanaoumia ni wananchi, Tundu Lissu haya anaongea sio kutoka moyoni ni kama anamfurahisha mfalme, chadema sasa ni CCM B hawaeleweki, Zamani chadema ikitetea Zanzibar huru sasa wanawatukana wazanzibari waziwazi baada mama kuwa Rais, Chadema haieleweki

Nafkiri Tanzania vyama vya upinzani hasa Chadema kimekosa muelekeo, Watanzania wanahitaji upinzani mpya usio na unafiki ndani yake, Chadema muda wake umekwisha, Mbowe sasa anakazia suruali tu muda wote Ikulu hana tena habari ya Katiba wala Tume huyu ya Uchaguzi. Mbowe siye tena yule wa zamani kwisha habari yake.
Punguza stress. Zitakuua.
 
Tatizo lako unahangaika na neno Huru baadala ya sifa za kuwa huru. Acheni uchawa kwenye mambo ya msingi.
kwahivyo kua na mihemko ndio unaona sifa?

uhuru ni pamoja na kuzira, kususa au kugomea uchaguzi kwan kuna shida gan,

au umelazimishwa kuamini uhuru wa hiyo tume 🐒

yaani wewe ukishinda uchaguzi ndio tume inakua huru, ukishindwa uchaguzi ndio inakua sio Huru 🤣

useless and none sense
 
Chadema ni waramba asali mara munamsifu mama na kumtukuza, hamuishi vikao na Samia Ikulu, mulisema Chadema hatapiga magoti kwa serikali ya ccm, hatimae Tundu Lissu alimualika mama belgium bila kuweka wazi hadi leo waliongea nini belgium, lakini mbowe alipotoka jela breki ya kwanza Ikulu, alibadilisha koti na tai akiwa Ikulu ndio akaenda nyumbani kwake sasa mnalalamika nini.

Mmeramba asali sasa wanaoumia ni wananchi, Tundu Lissu haya anaongea sio kutoka moyoni ni kama anamfurahisha mfalme, chadema sasa ni CCM B hawaeleweki, Zamani chadema ikitetea Zanzibar huru sasa wanawatukana wazanzibari waziwazi baada mama kuwa Rais, Chadema haieleweki

Nafkiri Tanzania vyama vya upinzani hasa Chadema kimekosa muelekeo, Watanzania wanahitaji upinzani mpya usio na unafiki ndani yake, Chadema muda wake umekwisha, Mbowe sasa anakazia suruali tu muda wote Ikulu hana tena habari ya Katiba wala Tume huyu ya Uchaguzi. Mbowe siye tena yule wa zamani kwisha habari yake.
Hivi wewe zinakutosha kweli,eti Lissu alimualika Rais kwenda Ubelgiji,hii ni akili au matope,yaani mtu yuko uhamishoni then amuite rais wa nchi aliyotoka na huyo rais aje kweli?
 
Tume Huru ya UchaguziTz, ni huru na itaendelea kua hivyo regardless ya maoni na mtazamo wa wachache wanaona sio huru 🐒

daima maoni yao yataheshimiwa huku yale ya wengi ambayo ndio katiba yenyewe sasa, ikiendelea kutekelezwa bila kuinajisi hata sheria moja 🐒

Katiba ni ya waTanzania, taasisi za uma ni za waTanzania na zinafanya kazi kwa kutokana na matakwa ya wengi kwa maslahi mapana ya wanainchi walio wengi, lakini kwa maslahi mapana ya waTanzania wote. wachache wanabaki kuskizwa na kuheshimika sana 🐒
Huwezi kuiita Tume Huru ya Uchaguzi kwenye nchi yenye mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa lakini Wakurugenzi na Watendaji wakuu 100% wanatoka chama Tawala na asilimia kubwa ni wateule wa Rais aliyep madarakani.Sifa ya neno HURU inapotea pale tu ambapo asilimia kubwa watendaji wake na wasimamizi wake ni wa chama kimoja cha siasa tena chama dola.
 
kwahivyo kua na mihemko ndio unaona sifa?

uhuru ni pamoja na kuzira, kususa au kugomea uchaguzi kwan kuna shida gan,

au umelazimishwa kuamini uhuru wa hiyo tume 🐒

yaani wewe ukishinda uchaguzi ndio tume inakua huru, ukishindwa uchaguzi ndio inakua sio Huru 🤣

useless and none sense
Kuzira,Kugoma na Kususa ni ubinadamu wa hali ya juu pale mtu anayekuzidi nguvu anapoamua kukugandamiza makusudi huku akijua fika kuwa anachokitenda si hali.Ni hali ya uzalendo kupinga dhuluma kwa vitendo,kupinga kunyanyaswa.Soma Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977 ibara ya 13(5)
 
Back
Top Bottom