Waziri Makamba amekuja na kampeni ya kutembelea vijijini na kuhimiza matumizi ya gas na umeme badala ya kuni.
Waziri makamba ni kweli hajui hali waliyonayo wanakijiji huko? Kwa data za world bank(benki ya dunia) watanzania milioni 27.6 ni maskini Sana.
Watu milioni 27.6 ni nusu ya watanzania...
Nauli kutoka Mwanza kwenda Bukoba au kutoka bukoba kwenda mwanza imepanda na itaanza kutumika jumatatu ya tarehe 4 July mwaka huu.
Daraja la chini ilikuwa 16000, itakuwa 21000
Daraja la Kati ilikuwa 30000, itakuwa 40000
Daraja la Juu ilikuwa 45000, itakuwa 55000
Naipongeza sana Serikali...
Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali, na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF).
Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi.
====
RAIS, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja...
Bei ya Umeme yapanda na kuwa sh.357 kwa unit 1. Naipongeza serikali kwa hatua hii
Ni miaka mingi imepita bei ilikua haijapanda, huku gharama za uendeshaji zikiongezeka maradufu.
Pia hii sh. 357 ni ndogo sana, Serikali ilipaswa kuweka sh 700 kwa unit 1 ili kuweza kuleta tija kwenye shirika hili...
Kuna maandamo ya Kumpongeza Raisi leo Dodoma yaliyoratibiwa na mkuu wa mkoa.
Mabango ya kila aina yenye picha kubwa za Raisi, wasanii na vijana waliopewa t-shirt zenye picha ya raisi.
Naona ujumbe wa katibu mkuu wa chama ulifika vizuri.
Kuna siku tunafikiria tuwe kama Europe? Lakini hataa hapa...
Leo waziri wa habari Napa wakati akisoma bajeti ya wizara amesema wizara imetenga bajeti ya kuchapisha picha ya raisi nakala 12794.
Si Jambo baya Ila kwa wakati huu sjo sahihi, serikali mara kadhaa imekiri kuwa mambo bado na Kuna baadhi ya sehemu wananchi wamekua walichangia baadhi ya miradi...
Leo huko kwenye mkutano wa raisi naona kila waziri anasema eneo lake ila kila baada ya sentensi wanamshukuru raisi kwa kibwagizo Cha tokea Uhuru haijawahi kutokea.
Huwa mara zote najiuliza raisi anakubaliana na hizi? Sasa kwa Tanzania ya leo yenye wananchi zaidi ya mil 60 bajeti itakuwaje sawa...
Leo muda huu Kuna mahojiano ya Raisi Samia na mtangazaji Tido mhando.
Raisi ameulizwa swali kuhusu kushushwa uchumi wa Kati wa chini, na amesema bado tupo uchumi wa Kati wa chini.
Ila nakumbuka alisema tumeshushwa, ukawa mjadala.
Mafuta yamepanda tena Bei, Dar Lita ya petrol kuanzia kesho ni 3148, dizeli 3258
Bei za mafuta kuanzia April 4, 2022
Bei ya petrol kwa Dar itakuwa ni Tsh 3,148 kwa lita. Kwa watu wa Tanga watanunua kwa Tsh 3,161 na kwa watu wa Mtwara kwa 3,177 kwa lita.
Dizeli itauzwa Tsh. 3,258 kwa lita kwa...
Kuna kitu kidogo nimeona kama hakipo sawa au ndio sielewi.
Mama Samia akiwa Marekani alikuwa akisalimiana na viongozi wa huko kwa kushikana mikono(picha namba 1,2,3) , Ila le baada ya kuja Tanzania leo hawakushikana mikono na viongozi wa hapa makamu wa raisi, waziri mkuu na makamu mwenyekiti wa...
Waziri Nape ameanza ziara nchi nzima kwa kutumia helikopta kuhamasisha zoezi la anuani ya makazi.
Sio jambo baya ila linafanywa kwa wakati ambao sio sahihi. Kwa nini? Kwa sababu hili zoezi linafanyika na watu hawana tatizo nalo, shida kubwa ni pesa tu za kuwalipa wanaofanya zoezi ndio tatizo...
Serikali kupitia BOT imepunguza riba ya hati fungani. Leo la hii huwa ni kudiscourage watu kununua sana hizi bonds. Ili watu wabaki na pesa, lakini kwa kipindi hiki Cha hyper inflation ni hatari kwa kuwa itaongeza zaidi Inflation.
Kabla na baada
2 yrs ilikua 7.82 na Sasa ni 7.6
5 yrs ilikua...
Hii bongo kuna matukio yanatokea unabaki mdomo wazi tu.
Jana Kariakoo mgambo walikuwa wakifukuza wale wamama wafanyabiashara ndogondogo Kariakoo.
Basi bwana wakafika kwa mama mmoja hivi baada ya kummwagia vitu yule mama akapandisha mori na kuanza kuvua nguo hadharani, mara ghafla akanya. Baada...
Raisi Samia Samia amewahi kutueleza pale tunapoona Serikali imekosea basi tuikosoe kwa staha na tushauri nini kifanyike.
Hivyo kwa staha naomba kuishauri Serikali juu ya hili ombi kwa wafanyabiashara kuchangia pesa kwa ajili ya anuani za makazi(postcode).
Sasa hivi Hali iliyopo inaonekana wazi...
Waswahili wanasema hata kama humpendi sungura basi sifia hata mbio zake.
Ukweli ulio wazi CHADEMA wanaziongoza sana siasa za Tanzania. Vyama vyote vimeshiriki hadi chama tawala lakini mkutano wa leo (Aprili 5, 2022) wa TCD umepoa sana na hata waliopo huko hawana hamasa ni kama wanapigishana...
Binafsi nilipenda sana utaratibu wa uwasilishaji wa report ya CAG kwa mwaka jana mwezi wa 4.
Aliwasilisha report na baada ya siku mbili aliita waandishi wa habari ikafanyika press ya kuchambua report yote ya CAG na nchi nzima walikua wanaelewa nini kilitokea kwa serikali yao.
Utaratibu ule...
Mradi wa NHC Morocco square utaanza kuuza nyumba, hivyo ni fursa kwa vijana tuwahi nyumba hapo kwa Bei nafuu Sana.
Nyumba ya vyumba vitatu ya bei ya chini sana ni Mil 592.
Msije kusema baadae zimeisha Mara hatukujua, changamkia fursa hiyo.
Wale watumishi wa serikali chukueni mkopo fasta...
Mara nyingi sana nimeona hii hofu na imekua ikionyeshwa sasa hadharani.
Leo wote wanazungumzia 2025, na jinsi walivyojipanga na wanavyotakiwa kuendelea kujipanga.
Binafsi bado sioni sana kama kuna ushindani mkubwa kihivyo hadi kuhofu 2025, maana Kuna mambo yakitokea hapo nyuma yalidhoofisha...
Mangula ameachia nafasi ya umakamu mwenyekiti CCM, kaona isiwe tabu.
Ila hii Ni Mara ya Pili mzee anawekwa pembeni, sijajua ana tatizo gani na wenzio huko.
Nafasi imechukuliwa na Kinana
Membe karudishwa CCM
===
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula leo...
Rais anapoteua wasaidizi, hateui wawe kazi yao kumsifia na kumpamba kupitiliza. Bali huwateua kwa lengo la kumsaidia kazi na kuleta maendeleo.
Amos Makalla kwa muda mrefu amekuwa akitumia nguvu na sifa kwa Rais na pengine hata Rais mwenyewe hafurahishwi na hilo Ila tu hawezi kusema. Ili Rais...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.