Jiji la Dodoma kuwaomba wafanyabiashara kuchangia pesa kwa ajili ya anuani za makazi (postcode) haijakaa sawa

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,965
Raisi Samia Samia amewahi kutueleza pale tunapoona Serikali imekosea basi tuikosoe kwa staha na tushauri nini kifanyike.

Hivyo kwa staha naomba kuishauri Serikali juu ya hili ombi kwa wafanyabiashara kuchangia pesa kwa ajili ya anuani za makazi(postcode).

Sasa hivi Hali iliyopo inaonekana wazi tu kuwa mambo hayajakaa sawa kutokana na huu mfumuko wa Bei unaoendelea na hata wafanyabiashara wameathirika sana na hili na juzi hapa mh.raisi alisema gharama yuingiza kontena imepanda kutoka dola 1500 hadi dola 8000.

Hivyo kwa mfanyabiashara ambae mwanzo ilibidi atumie bil 1 kuingiza makontena yake kadhaa, Sasa hivi itahitaji atumie bil 8 kuingiza makontena hayo kadhaa. Hivyo nae kwa sasa atahitaji pesa nyingi kuagiza mzigo mkubwa kutokana na kupanda sana bei

Lakini pia hili zoezi bajeti yake ilishatengwa, Ila Kama haitoshi basi niwaombe serikali mnaweza kulisogeza mbele.

20220405_132945.jpg
 
Zoezi lenyewe la kibwege

Wamejazana watendaji wa kata na maafisa wa serikali

Alafu vp hawakuwa na bajeti ya kukamilisha hilo nini kiliwafanya walianze
 
Kimsingi Jiji la dodoma limeamua kwenda mbali zaidi kwa kuweka vibao vya mitaa moja kwa moja, hili zoezi lionaloendelea ni kusajili makazi yote n kutoa anuani ya makazi ila haihusishi kubandika vibao vya mitaa mara moja.

Hivyo kiutendaji budget haiwezi kukidhi shuguli kama hii na ndio maana Jiji la dodoma limeamua kuomba msaada kwa wahisani/wafanyabiashara mbalimbali. Hakuna ubaya ni swala la hiari tu. Bilioni 5 kwa halmashauri ni nyingi kwa sababu kumbuka dodoma mapato yake yako chini hayawezi kukidhi shughuli zote.

Sent from my SM-G935U using JamiiForums mobile app
 
Kimsingi Jiji la dodoma limeamua kwenda mbali zaidi kwa kuweka vibao vya mitaa moja kwa moja..hili zoezi lionaloendelea ni kusajili makazi yote n kutoa anuani ya makazi ila haihusishi kubandika vibao vya mitaa mara moja. Hivyo kiutendaji budget haiwezi kukidhi shuguli kama hii na ndio maana Jiji la dodoma limeamua kuomba msaada kwa wahisani/wafanyabiashara mbalimbali. Hakuna ubaya ni swala la hiari tu. Bilioni 5 kwa halmashauri ni nyingi kwa sababu kumbuka dodoma mapato yake yako chini hayawezi kukidhi shughuli zote.

Sent from my SM-G935U using JamiiForums mobile app
Makusanyo Sasa hivi si yameongezeka maradufu na rekodi zimevunjwa? Inakuwae bil 5 iwe shida?
 
Makusanyo Sasa hivi si yameongezeka maradufu na rekodi zimevunjwa? Inakuwae bil 5 iwe shida?
5 bil kwa halmashauri siyo swala dogo pia Kumbuka haikiwepo kwenye bajeti 2021/22. Pia halmashauri ya Jiji la dodoma haina vyanzo vya kutosha vya mapato kuweza kufanya yote hayo. Ndio maana imeomba msaada kwa wahisani si jambo baya kwa sababu ni jambo la maendeleo ambayo yanarudi kwa wananchi husika.

Sent from my SM-G935U using JamiiForums mobile app
 
Kimsingi Jiji la dodoma limeamua kwenda mbali zaidi kwa kuweka vibao vya mitaa moja kwa moja..hili zoezi lionaloendelea ni kusajili makazi yote n kutoa anuani ya makazi ila haihusishi kubandika vibao vya mitaa mara moja. Hivyo kiutendaji budget haiwezi kukidhi shuguli kama hii na ndio maana Jiji la dodoma limeamua kuomba msaada kwa wahisani/wafanyabiashara mbalimbali. Hakuna ubaya ni swala la hiari tu. Bilioni 5 kwa halmashauri ni nyingi kwa sababu kumbuka dodoma mapato yake yako chini hayawezi kukidhi shughuli zote.

Sent from my SM-G935U using JamiiForums mobile app
Tuliwahi aminishwa enzi za Jiwe kuwa jiji la Dodoma linaongoza katika ukusanyaji wa mapato, wakati huo mkurugenzi wa jiji alikuwa Kunambi vipi sasa mambo yamegeuka?
 
Tuliwahi aminishwa enzi za Jiwe kuwa jiji la Dodoma linaongoza katika ukusanyaji wa mapato, wakati huo mkurugenzi wa jiji alikuwa Kunambi vipi sasa mambo yamegeuka?
Ni kweli lakini kipindi kile dodoma ilikua inakuzwa kisiasa. Japokua bwana Kunambi alikua the best Director kwa sababu ni mtu mbunifu sana. Aliweza kubadilisha taswira ya Jiji kwa muda mfupi sana. Kwa hali ya sasa hivi haiwezekani.

Sent from my SM-G935U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom