Kwa sera anazomwaga Tundu Lissu usipompa kura utakua na lako.

1: Maendeleo ya watu
Wote waliodhurumiwa na kuvunjiwa sehemu za makazi bila compensation watafidiwa

2: Atakuza uchumi na shughuli za maendeleo kwa kupunguza utitiri wa kodi
Toka utitiri wa kodi 15 hadi 1 tu, ambayo ni 10%ya bidhaa ulizoagiza.

3. Kitambulisho cha machinga kutolewa bure

4: Wafanyakazi kutoongezewa mshahara itakuwa mwiko - ataanza kwa kufidia miaka 5 ambayo hawajaongezewa Mshahara.

5. Watumishi waliofukuzwa kazi kwa sababu zisizo na mashiko itaangaliwa namna ya kuwafidia.

6. Mafao ya kustaafu yatalipwa kwa wakati

4: Ataboresha kwa kuongeza wigo wa mikopo ya wanafunzi wa chuo kikuu. Pia ataondoa ongezeko la 15% la marejesho ya mikopo kwa wanufaika

Bado anatema cheche.
 
Huyu wa Leo ndo Lissu ninayemfahamu mie. Hongera sana Lissu. Leo umetugusa vizuri sana watanzania. Na huu ndo uwe mwendo
Kweli kabisa. Watanzania wanataka mazingira bora ili wachape kazi kwa moyo mmoja. Siyo unachafuka chalk,kuandaa materials mwisho wa mwezi unaishia laki nne tena mfululizo miaka mitano hata mia haijapanda.
 
Asilimia tatu nayo ikushinde kulipa ?Halafu usipofanya kazi utaishi vipi ?On top of that Kaka wewe umesomeshwa,somesha wengine pia. Lipa mkopo.
Sasa si nitafanya ujasiriamali.

Sio ulazima wa kulipa mkopo ambao silazimishwi kulipa, ambao kulipa ni mpaka niwe na ajira.
 
Back
Top Bottom