Tundu Lissu hana tofauti na Magufuli, anatumia propaganda za serikali ya Magufuli kumchonganisha Samia na wananchi

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,922
18,994
Wanaharakati wengi naona wamemgeuka Tundu Lissu kule X (Twitter) X ambayo ndio strongest base ya Chadema, iligeuka chungu baada ya clip ya maneno ya kibaguzi ya Lissu kupostiwa kule

Ni sahihi kukosoa Muungano wetu, ni sahihi pia kukosoa makosa ya serikali ya Samia

Lakini kisicho sawa ni kusema au ku imply makosa yanyofanywa na serikali ya Samia yanatokana na yeye kuwa Mzanzibari

Ndicho ambacho Tundu Lissu alikuwa anawaaminisha wananchi

Tundu Lissu anatumia mbinu zilezile za kuwa vilify washindani wake wa kisiasa kama sio watanzania halisi na ndio maana wanafanya makosa (wanayoyaona wao ni makosa) wanayosema wanayafanya

Ni mbinu ile ile iliyotumiwa na Magufuli ambaye ndiye Lissu alikuwa akisema ni rais mbovu na wa ajabu kuwahi kutokea kupambana na washindani zake wa kisiasa

Wakosoaji wa Magufuli walikuwa wakisakamwa uraia wao, kuporwa paspoti na kuitwa vibaraka wa mabeberu ambao hawana upendo na Tanzania

Na ndio hicho hicho lissu anakifanya kwa Samia kumuonyesha kama mamluki fulani asiyejali lolote kuhusu Tanzania

Kuna wengine watasema Katiba ya Zanzibar inawatambua kama Wazanzibar na sio Watanzania, lakini huu muungano haukuwa designed na Samia, na ndio maana nikasema ni sawa kuukosa Muungano na Katiba yetu
 
CCM na serikali, leteni katiba moja na bora, mumalize kidomo domo cha wapinzani, maneno yamekuwa mengi sana, waTanzania wanataka kuondoa matatizo yao ya Muungano. Sasa ni wakati muafaka kuyamaliza maana jiwe limetupwa gizani - sote tunaruka ruka na kukanyagana. Tumalize hizi habari za Tamganyika na Zanzibar. Tuacheni tupumue, CCM na serikali yenu, malizeni tatizo hili, maneno ni mengi- acheni tupambane na kikotoo.
 
Wanaharakati wengi naona wamemgeuka Tundu Lissu kule X (Twitter) X ambayo ndio strongest base ya Chadema, iligeuka chungu baada ya clip ya maneno ya kibaguzi ya Lissu kupostiwa kule

Ni sahihi kukosoa Muungano wetu, ni sahihi pia kukosoa makosa ya serikali ya Samia

Lakini kisicho sawa ni kusema au ku imply makosa yanyofanywa na serikali ya Samia yanatokana na yeye kuwa Mzanzibari

Ndicho ambacho Tundu Lissu alikuwa anawaaminisha wananchi

Tundu Lissu anatumia mbinu zilezile za kuwa vilify washindani wake wa kisiasa kama sio watanzania halisi na ndio maana wanafanya makosa (wanayoyaona wao ni makosa) wanayosema wanayafanya

Ni mbinu ile ile iliyotumiwa na Magufuli ambaye ndiye Lissu alikuwa akisema ni rais mbovu na wa ajabu kuwahi kutokea kupambana na washindani zake wa kisiasa

Wakosoaji wa Magufuli walikuwa wakisakamwa uraia wao, kuporwa paspoti na kuitwa vibaraka wa mabeberu ambao hawana upendo na Tanzania

Na ndio hicho hicho lissu anakifanya kwa Samia kumuonyesha kama mamluki fulani asiyejali lolote kuhusu Tanzania

Kuna wengine watasema Katiba ya Zanzibar inawatambua kama Wazanzibar na sio Watanzania, lakini huu muungano haukuwa designed na Samia, na ndio maana nikasema ni sawa kuukosa Muungano na Katiba yetu
Watanzania wengi akili zenu ni mbovu. Hivi kweli kwanini hamsapoti upinzani wakati hali za maisha yenu ni ngumu na mnajua wazi kuwa CCM ndio tatizo lenu, au hamjui?!
 
Ieleweke kwamba, kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, Samia suluhu Hassan ni mZanzibar. Mtu akisema Samia ni mZanzibar hajakosea. Tatizo ni aina hii ya muungano unaolazimishwa na wanasiasa.
Wanasiasa wa ccm walazimisha kujenga ukuta juu ya msingi mbovu. Kama tuna nia nzuri kama taifa, tufanye kura ya maoni, na iwapo raia wa pande mbili wanapendelea muungano basi tuwe na serikali moja. Mambo ya kusema kizazi hiki hakijui historia ni hadithi ambazo hazisaidii chochote. Historia tunaisoma, lakini lazima tuishi kuendana na uhalisia wa leo.
 
Kweli kabisa unaweza kuunga mkono ccm kwa yote haya mabovu na unaamini Mungu atafurahishwa na wewe? Watanzania tuache ulimbukeni, kwanini mnapenda matatizo hivyo?!
Kwa akili yako unaamini Mbowe na Zito ni wapinzani?

Na unaamini wakipata madaraka wataondoa uozo uliopo?

Pole sana.
 
Back
Top Bottom