Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Kutokana na Mgogoro ambao umemhusu Mbunge wa kibamba Mhe John Mnyika nimebaini Pasipo na shaka kuwa Job Ndugai ambae ni Spika, hana uwezo kabisa wa kuongoza chambo kikuu cha maamuzi kama Bunge.

Japo kuwa ni Spika Tayari lakini tunatakiwa kujua kuna watu ni Marais lakini hawana sifa za kuvaa uhusika hivyo hivyo Ndugai hafai kuwa Spika na Wala tusitegemee jipya lolote kutoka kwenye Bunge analoliongoza yeye na msaidizi wake Tulia Ackison.

Nimesema hivyo hana sifa yoyote ambayo imetokana na Nadhalia za uongozi ususani skill model of Leadership.

Na hizi ndio sifa za Job Ndugai ambazo zinamfanya kukosa sifa za kuwa Spika japo ni Spika na kwa maana hiyo Bunge la sasa ni Dhaifu sana.

1)-Anajaziba, kutokana na hii sifa siku zote hawezi kutoka maamuzi sahihi sifa hii inaonekana pale alipompiga Mgombea mwezake wa ndani ya chama chake.

2)-Ni Mtu wa kujipendeza, na hii inafanyika ili atete kiti chake cha uspika ndio maana anatumia nguvu nyingi kuwaonea wapinzani ili amfurahishe Rais ambae ndio Mwenyekiti wa chama.

3)-Nimkurupukaji, kutokana na sifa hii inamfanya afanye maamuzi na atoe kauli za kitoto ambazo zinalifanya Bunge kuwa dhaifu sababu linaogozwa na watu dhaifu.

Mfano aliposema Lusinde wewe ni kiboko yao mpaka wote wameondoka hii nikauli ya kitoto haikupaswa kusemwa na mtu kama Spika.

4)- ni kigeu geu, sio mtu wa kuamini au kupanga nae mambo makubwa na hii inasababishwa na yeye kuwa mtu wa kujipendekeza.

5)-Anaongozwa na Mhemko, Hana Busara wala Hekima kwa Suala la Mnyika hajatumia Busara wala Hekima Mropokaji.

Kutokana na madhaifu yake yote hayo mzee Chenge ameonyesha uwezo mkubwa kuliko yeye pamoja na msaidizi wake Tulia Ackison.

Kutokana na wabunge kuonewa katika kipindi chake na Serikali au na yeye Mwenyewe pamoja na Msaidizi wake wamefanya ubunge kutokueshimaka kabisa na watu.

Nilikuwa sijawahi kusikia Kwamba Mbunge anaweza kuwekwa ndani mwezi 4 na hajaua ni kipindi cha Ndugai kwa maana hiyo pale amekaa kuziba nafasi isiwe wazi na sio kuliongoza Bunge kupitisha maamuzi sahihi kwa maslahi ya nchi yetu kama lilivyokuwa Bunge la 2005- 2010 kila mtu alitamani kuwa Mbunge.

Ni Mhere Mwita.
 
Wale wafia chama la kupokea takataka kutoka upande wa kwanza naona wameshaanza yao.....ila hongereni sana mataputapu
 
Bavicha sijui mnakula nini.Ni mwezi uliopita tu mlimsifia spika kuwa amejitambua kwa sasa yupo vizuri na sifa chungu nzima
 
Back
Top Bottom