Mwenda pole wahenga waliotuambia hajikwai, alijikwaa, aliwekewa jiwe kubwa, akaliona lakini akasema kwa mwendo wake atavuka salama, akajipa moyo na kujiamini. Ahhh akaingia kingi, akajikwaa kweli kweli safari hii kujikwaa ikawa kuanguka, hakuamka tena! Hawana hata habari, sababu hakupita kwenye njia rasmi alipoanza safari yake, alitumia njia za panya. Ndo maana kila siku wanasema hawajui chochote kuhusu jiwe walilomwekea kumtega. Taarifa ni kwamba, methali ilishabadilika maana kitambo sana...