kuzoa taka

No Wikipedia entry exists for this tag
  1. BigTall

    Halmashauri ya Jiji imeshindwa kumsimamia Mkandarasi kuzoa taka kwa wakati Mitaa ya Kariakoo

    Hili siwezi kukaa nalo lazima niliseme maana alihitaji uelewa zaidi wa kibobezi. Mimi nafanya harakati zangu za kutafuta riziki mitaa ya Kariakoo sasa nina mwaka mmoja na miezi kadhaa lakini kuna jambo naomba nililete hapa jukwaani wana JF tusaidiane kulipazia sauti. Kama tunavyojua kwenye...
  2. JanguKamaJangu

    Hatimaye wazoaji taka wametimiza wajibu wao kwa kuzoa taka Mtaa wa Mzimuni - Kawe

    Yaani muda mfupi baada ya kuweka andiko langu hapa, jana hiyohiyo magari mawili ya kuzoa taka yalifika mtaani kwetu na kubeba taka zote zilizokuwa zimezagaa. Kumbe inawezekana, sasa walichokuwa wanasubiri ni nini? Wanataka hadi turipoti mitandaoni ndio hatua zinachukuliwa? Hii si sawa...
  3. A

    DOKEZO Dampo katika Soko la Stereo lililopo Temeke ni kero kubwa, Mamlaka ziongeze nguvu katika kuzoa taka

    Dampo lililopo kwenye soko la Stereo hapa Tekeme, Dar es Salaam ambapo ni sehemu kwa Wauzaji wa soko hili kuhifadhi takataka baada ya wao kufanya usafi kwenye maeneo yao, limekuwa ni kero kubwa kwa Wafanyabiashara na Wanunuaji wa bidhaa katika Soko hilo. Wafanyabiashara katika soko hili kwa...
  4. Anonymous

    Mkandarasi anatulipisha Tsh 50,000 kwa nyumba kila mwezi kuzoa taka Masaki (Dar) lakini huduma ni mbovu

    Mimi ni mkazi wa Masaki nimeona ripoti ya gharama za utoaji taka kuwa kubwa mitaa ya Mbezi Beach B (maarufu kwa jina la Mbezi Beachi ya Chini) nikaona nami nipaze sauti yangu kwa upende wetu wa Masaki ndani ya Jiji letu hili la Chalamila. Huku Masaki gharama ni mara mbili ya Mbezi, Mkandarasi...
  5. JanguKamaJangu

    Bei ya kuzoa taka Mbezi Beach inapangwa kutokana na uhalisia wa mazingira na kipato

    Siku chache baada ya malalamiko kuripotiwa kuhusu gharama za uzoaji taka kwenye makazi ya watu kuwa juu katika baadhi ya mitaa ya Mbezi Beach B, ikidaiwa kuwa kuna kampuni inayotoza Tsh. 15,000 kwa mwezi kwa nyumba badala ya Tsh. 3,000 hadi 5,000 kwa mwezi, ufafanuzi umetolewa. Malalamiko yako...
  6. BigTall

    Wananchi Tabata Kisukuru kero yetu kubwa ni kukosa gari la kuzoa taka na uhaba wa maji

    Mimi kero yangu au naweza kusema kero ya watu wengi huku mtaani kwetu Tabata Kisukuru ni kuwa gari la Taka halijaonekana muda mrefu na taka zimejaa kwenye nyumba nyingi mpaka zinanuka na kutengeneza wadudu. Kero nyingine ni kuwa maji ni ya shida sana yaani tunataabika kwelikweli, tupazieni...
  7. M

    Magari ya kuzoa taka yaadimika Manispaa ya Kinondoni

    Ni mwezi wa pili sasa magari ya kuzoa taka hayaonekani mitaani na badala yake wakusanya ushuru wa taka ndio wamezagaa kukusanya ushuru wakigonga milango na mageti ya wanamtaa! Hakuna taarifa yoyote kutoka kwa watendaji wa mtaa na mabwana/ mabibi afya wa kata juu ya sakata hili. Natambua uwepo...
  8. Mwanongwa

    Mbeya usafi ni kama anasa ndani ya jiji

    Jiji la Mbeya na vitongoji vyake suala la usafi limekuwa ni changamoto sana.Takataka zimezagaa kila kona ya mitaa ya jiji hilo . Wananchi wanatozwa pesa za taka na wanaambiwa taka hizo wazitoe majumbani zikiwa kwenye viroba kisha kuziweka barabarani kwaajili ya magari kubeba lakini matokeo yake...
Back
Top Bottom