Magari ya kuzoa taka yaadimika Manispaa ya Kinondoni

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,659
6,910
Ni mwezi wa pili sasa magari ya kuzoa taka hayaonekani mitaani na badala yake wakusanya ushuru wa taka ndio wamezagaa kukusanya ushuru wakigonga milango na mageti ya wanamtaa!

Hakuna taarifa yoyote kutoka kwa watendaji wa mtaa na mabwana/ mabibi afya wa kata juu ya sakata hili.
Natambua uwepo wa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, bwana afya wa manispaa na mkurugenzi wa manispaa pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam hapa jukwaani.

Niwatake wahusika watoe taarifa kwa wananchi wanaoteseka na uvundo wa takataka kwenye majumba yao na tayari taka nyingine zimeanza kutupwa kwenye barabara na maeneo ya shule.

Hali hii ikiachiwa itasababisha magonjwa ya kuhara na kipindupindu na hatimaye vifo.

Wananchi walio wengi walishalipia huduma ya kuzolewa taka na wanatafuta zilipo ofisi za mwenye kandarasi ya kuzoa taka wadai pesa zao Jambo ambalo litazua tafrani. Mitaa ya Tegeta na Kunduchi taka ni nyingi mno.
 
Back
Top Bottom