Anonymous
Senior Member
- Feb 3, 2006
- 125
- 321
Mimi ni mkazi wa Masaki nimeona ripoti ya gharama za utoaji taka kuwa kubwa mitaa ya Mbezi Beach B (maarufu kwa jina la Mbezi Beachi ya Chini) nikaona nami nipaze sauti yangu kwa upende wetu wa Masaki ndani ya Jiji letu hili la Chalamila.
Huku Masaki gharama ni mara mbili ya Mbezi, Mkandarasi hutoza kuanzia kiasi cha Tsh. 40,000 mpaka Tsh. 50,000 kwa nyumba, ajabu ni kuwa kwa mwezi gari la kukusanya taka hupita mara moja tu likijitahidi saana litapita mara mbili kwa mwezi.
Kuna wakati baadhi ya maeneo hufika mpaka miezi miwili hadi mitatu hatujapata huduma wakati Mkandarasi anakuletea invoice na unalipishwa kinguvu, ukikataa unapelekwa kwenye Vyombo vya Sheria, vinakuhukumu ilipe hata kama hujapata huduma, mbaya zaidi ukimhoji Mkandarasi unajibiwa Halmashauri zinataka mapato lazima tu ulipe.
Jamani kama sio uonevu ni nini? Tunaonewa naombeni Vyomba vya Habari mtusaidie kufikisha malalamiko yetu kwenye mamlaka husika tafadhali.
Pia soma: